Naombeni msaada wa kuchangiwa Bima ya Afya (NHIF) ili kuokoa maisha yangu

Pole sana mr John lakini mimi nashauri kama vipi ukachukue bima ya resolution ofisi zao zipo Victoria Makumbusho jengo la accacia kwa ghalama ya 86,000 ikusaidie kwanza
Asante...bima tayari wakuu wamenichangia humu, nikachukua ya NHIF ile kubwa ya Sh 1.5M.
Naitumia kwa huduma zote kasoro kwenye kusafisha damu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu kwa dialysis ya mwezi wa tatu bado nahitaji Sh 310,000.
Nimepata Sh 30,000 ya kesho Jumatatu baada ya hapo sitakuwa na salio kwa dialysis zijazo.
Namba zangu ni 0679047446 (Tigo Pesa) na 0767157788 (M-Pesa)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamani habari za jioni

Narudi tena kwenu kuna watu waliotoa ahadi za kumsaidia ndugu yetu huyu kwa ajiri ya dialysis, tunakuomba utimiza ahadi yako kwani ndugu yetu yuko katika uhitaji mkubwa wa hela ya dialysis ya mwezi February kiasi kinachotakiwa ni laki 340 pesa alizonazo ni elf 26..pls msaada wako ni muhimu
Sorry naomba kuuliza...ina mana hiyo dialysis hainaga mwisho???
Yani ndo itakua maisha yake yote?


Sorry kwa kuuliza maana mara yangu ya mwisho kuumwa ilikua 1997...sijawai kuumwa tena hata malaria mpaka leo hii...na mara yangu ya mwisho kwenda hospital kumcheki mgonjwa ilikua 2010......

aiseee toka siku ile niliheshimu sana kitu kinaitwa "afya njema". It was terrifying.
 
Sorry naomba kuuliza...ina mana hiyo dialysis hainaga mwisho???
Yani ndo itakua maisha yake yote?


Sorry kwa kuuliza maana mara yangu ya mwisho kuumwa ilikua 1997...sijawai kuumwa tena hata malaria mpaka leo hii...na mara yangu ya mwisho kwenda hospital kumcheki mgonjwa ilikua 2010......

aiseee toka siku ile niliheshimu sana kitu kinaitwa "afya njema". It was terrifying.
Mwisho wa dialysis ni pale figo zako zitakapo kubali kufanya kazi au utakapo badilishiwa figo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu naombeni mchango wenu wa kifedha.
Dialysis ya mwezi huu wa tatu imekuwa ngumu sana kwani mpaka sasa nimesaliwa na Sh 30,000 tu kati ya 340,000 na mwezi haujaisha.
Kuna session 1 ya kufunga mwezi inadai Sh 55,000

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwenye kampuni ya ujenzi (majengo) class one au two tuwasiliane nimpe kazi.
Kampuni itoke Dar es Salaam
.
Simu: +255679047446
WhatsApp: wa.me/255767157788
 
Huyu mtu ni tapeli jamani, futeni tangazo lake anasema ajenga nyumba za halmashauri ya namtumbo
 
Huyu mtu ni tapeli jamani, futeni tangazo lake anasema ajenga nyumba za halmashauri ya namtumbo
Sasa akisema anajenga nyumba za almashauri ndiyo amekutapeli?
Je angekuomba pesa ungesemaje?
Kwa nini mnakimbilia kuchafua watu pasipo kujiridhisha?
Nilidhani naongea na mtu wa maana kumbe mbugila mmoja hivi
 
Wanalipa kwa wakati? au ndio ile unazika hela zako,kipindi cha kudai malipo mnaanza kukimbiana
 
Mbona maelezo yako yanajichanganya au unataka nikuwekee maongezi yako uliyokuwa unajichanganya, nenda ukawaibie hukohuko lkn kwa waelewa huwezi kuwapata,
 
Kwa mchango wowote wasiliana nami kwa +255679047446 (Tigo) / +255767157788 (Voda) au siku za Jumatatu na Alhamisi fika Muhimbili, Kitengo cha figo (jengo la watoto) ulizia ofisi za ustawi (social work) hapo ofisini ulizia mgonjwa 'John Manyama'

Habari wana jamvi wa JF,
Naitwa John. Nina miaka 41. Ni mgonjwa wa figo (Chronic Kidney Disease) ninaye fanyiwa usafishaji wa damu (Dialysis) kwenye hospitali ya taifa Muhimbili kwa takribani mwaka 1 na miezi 6 sasa.

Mwanzo gharama za usafishaji na dawa nilizimudu kutokana na akiba yangu niliyo ilimbikiza kutokana na shughuli za usimamizi wa ujenzi wa nyumba na miundombinu. Pia jamaa na marafiki nao michango yao ilihusika sana japo kwa sasa nimebaki peke yangu.

Pamoja na michango mbalimbali na akiba yangu, sikuweza kufikisha pesa (TSh 1,500,000) ya kulipia bima ya afya (NHIF).
Kilichonisukuma kuja kwenu ni kukosa namna ya kumudu gharama za usafishaji figo kwa wagonjwa wa kulipia (public) ambazo zimepanda kutoka TSh 50,000 kwenda TSh 90,000 kwa dialysis moja, wiki tatu zilizopita.

Kawaida mgonjwa wa kulipia anatakiwa afanye dialysis 2 kwa wiki. Japo awali nilipewa kiwango cha msamaha cha Sh 30,000 kwa kila dialysis lakini sikuweza kumudu kulipia zote 2 kwa wiki.

Naamini wana JF ni wasikivu na jamii ya ushirikiano. Kumbuka mgonjwa wa figo hasubiri. Akikosa matibabu wiki moja tu maisha yake yanakuwa mashakani.

Naombeni michango yenu ya bima ya afya na dialysis. Mwenyezi Mungu awabariki
.
.
.
_November 2018 UPDATE
Wakuu mpaka sasa mchango wa bima ya afya uliopatikana kutoka kwa members hapahapa JF ni TSh 730,000. Almost tumefikia nusu ya lengo.
Lengo ni kupata TSh 1,500,000.
Nikipata bima, itanisaidia upandikizwaji wa figo. Tayari nimepata donors wa kunipa figo hivyo nawaomba muendelee kunichangia ili tufikie lengo.
.
Pia watakaopenda kunichangia pesa ya kusafisha damu (TSh 30,000 kwa session) nitashukuru. Session ziko 2 kwa wiki. Unaweza kuchangia hata 1 kadri ya uwezo wako.
Gharama ya kusafisha damu (dialysis) sasa nimepunguziwa kutoka TSh 90,000 mpaka 30,000 kwa session.
.
Jamii moja, huzungumza lugha moja
Asanteni
.
.
.
NOVEMBER 28 2018 UPDATE
Wakuu leo nimetoka kulipia bima ya afya (NHIF) iliyotokana na michango yenu.
Napenda kutoa shukurani zangu za dhati kwa wote mlio fanikisha zoezi hili. Mpo wengi na wengine hawakupeda kutajwa hapa lakini wote kwa umoja wenu nasema asante.
.
Kwa sasa nasubiri kadi ya bima itoke. Itachukua siku 21 za kazi kutoka.
Kadi ikitoka itanisaidia kwenye matibabu yote ikiwemo vipimo kwa ajili ya transplant na madawa baada ya trasplant (ikiwa ntapandikizwa) isipokuwa haitaweza kunihudumia upande wa kusafisha damu (dialysis) pamoja na dawa za ku-boost damu mpaka baada ya mwaka mmoja ntakapo renew.
Hivyo kwa sasa ntaendelea kulipia dialysis mpaka pale ntakapo pandikizwa figo au baada ya mwaka ntakapo renew bima
.
Natumai tutazidi kushirikiana na kupeana updates.
Naomba mwenyezi Mungu atuongoze na kutubariki wakati tukiendelea kutimiza majukumu yetu.
.
Jamii moja, huzungumza lugha moja
.
.
.
JANUARY 2019 UPDATE_
Wakuu, heri ya mwaka mpya. Namshukuru Mungu kwa kuendelea kunipa pumzi ya uhai na kufanya historia ya maisha yangu kuingia mwaka 2019.
.
Nimewaletea taarifa kuwa ile kadi ya bima ya afya niliyo kuwa nikiisubiri kwa ule muda wa siku 21, sasa iko mikononi mwangu, nina maana nimesha ichukua toka mfuko wa bima wa taifa (NHIF)
.
Nawashukuru sana kwa kazi kubwa mlio ifanya.
Mwanzo ilionekana ni kitu kama hakiwezekani hivi, kumbe inawezekana.
Niliwaamini ndo maana nilileta ombi langu kwenu. Kuna mitandao mingi ya kijamii lakini mi niliona Jamii Forum ndo ina watu wenye ukweli kwa maana kwamba mtu akisema ndiyo inakuwa ndiyo kweli, akisema hapana inakuwa hapana kweli.
Mitandao mingine imetawaliwa na maroboti. Roboti linaweza ku-like au ku-comment post yako, ukasema ni mtu kumbe ni roboti.
.
Narudia kuwashukuru kwa hapa tulipofikia.
Jambo la nyongeza, napenda kukumbushia kwa wale watakao wiwa kunichangia pesa ya kusafisha damu (dialysis) kwa mwaka huu 2019 wakati nikisubiri bima ikomae, nawakaribisha.
Hili nililieleza kwenye update ya November 28 2018, unaweza kupitia ukasoma.
.
Mwenye mchango anaweza pitishia kwenye namba hizi:
0767157788 (M-Pesa) au 0679047446 (Tigo Pesa) Jina litakalo tokeza ni John Makanga
.
Jamii moja, huzungumza lugha moja.
Nenda kwa Mwamposa ukapone,
 
71 Reactions
Reply
Back
Top Bottom