Ten reasons to expect revolution! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ten reasons to expect revolution!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by jmushi1, Jan 6, 2012.

 1. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #1
  Jan 6, 2012
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,583
  Likes Received: 1,944
  Trophy Points: 280
  Nimejaribu sana kuangalia na kufuatilia sababu za kuwepo na mapinduzi kwenye nchi nyingine duaniani.

  Hivi majuzi hapa, ndugu mmoja member humu anayeitwa mtoa habari alisema jambo moja ambalo liliniumiza sana na sitoweza kulisahau mapema...

  Kwamba sanduku la kura halitaweza kuwaondoa mafisadi, bali nguvu ya umma peke yake...!

  Ni maneno yanayochoma lakini yenye ukweli.

  Yana ukweli kwasababu haya tayari yameshatokea nchini kwetu, kuwa sanduku la kura halituchagulii viongozi.

  Hilo lenyewe ni justification ya uwepo wa mapinduzi.

  Najuwa wengi wetu wanasema hilo kwa watanzania haliwezekani.

  Je kusema haiwezekani inamaanisha kitu gani?

  Kwamba tuombe tu Mungu wawe na huruma siku moja hao mafisadi?

  Ama ina maana kuwa wengi wetu sasa hatujali tena kuhusu yanayotokea kwenye Taifa letu?

  Je ni kweli hatuwezi kufanya mabadiliko tunayoyataka?

  Mimi binafsi sidhani kama inawezekana hata siku moja kuwa hawa watu watabadilika na kuieletea nchi maendeleo!

  Ni wazi kwamba wengine ni lazima tujitolee muhanga kama ni kweli tuanataka mabadilko.

  Binafsi pia naamini kuwa ni lazima kuwepo na "wakombozi" watakaokubali kuingia "Msituni" kuwa trained na kulikomboa Taifa.

  Nje ya hapo hakuna kitu na mnaweza kumark ma words on this...

  Kama kuna ambao wameshaanza, tafadhali ni PM.

  Kama wewe ni usalama usijisumbue kuni PM

  Nataka kujiunga na wale waliojitolea muhanga kulipigania Taifa hili, kwasababu na mimi nimejitolea, ila sijui pa kuanzia na siju nani mkweli yupi, na nani si mkweli.

  Ila atakayeuona ujumbe huu, na kwamba ana connection ya wenye mawazo sawa na yangu, basi tafadhali ni PM.


  Hapo chini, ni sababu 10 za kutarajia mapinduzi...


  Ten reasons to expect revolution

  1. As Marie Antoinette found to her cost, any ruling oligarchy can only take the piss so much. Right now they may be sitting on a socially explosive time bomb.

  2. In the past people have been bought off by different politicians, but today as dissatisfaction spreads nobody is voting, joining or selling papers, the party's over. We know that the Bolsheviks led to the gulag, the National Socialists led to the holocaust and the Labour Party led us up the garden path. No more illusions, no more compromises, no more leaders. This time we're going to do things ourselves.

  3. Revolutionary epochs are times when history speeds up, nobody ever sees them coming.

  4. Capitalism's traditional justification, that it leads to an increase of total wealth, is increasingly inadequate as it becomes obvious that our problem is not a shortage of wealth but that our wealth is not shared equally. The promise of endless economic growth is unsustainable and, since it is us who have to make all the extra stuff, undesirable.

  5. In desperation capitalist politicians have invented another justification- that capitalism guarantees freedom. From their perspective this is a very dangerous claim since capitalism has always ultimately rested on violence. Simultaneously, we see an increase in public awareness of US foreign policy, or, the policing of global capital. The protest movement against the invasion of Iraq was the biggest the world has ever seen. The invasion of Iraq was a very bad thing but it cannot be said to have been worse than other US exploits in Chile or Guatemala, for example. In an age of global communications and increasing public awareness of the role our governments perform in the world, slaughters on behalf of the economy will become less and less palatable. There is no reason to think capitalism can survive without them in the future.

  6. Every generation believes that their socio-economic situation is somehow natural and inevitable. Every generation believes they stand at the end of history. Capitalism will fall like the Eastern Bloc, like feudalism and all that came before it. We are in the waning days of Babylon.

  7. Everywhere today we see an increase in repression and a rise of nationalism and fascism. This can only mean one thing; capitalism as we know it has got problems.

  8. It may seem absurd to talk about revolution but all the alternatives assume the continuation of the present situation, and that is even more absurd.

  9. "If the workers take a notion, they can stop all speeding trains; every ship upon the ocean they can tie with mighty chains. Every wheel in the creation, every mine and every mill, fleets and armies of the nation, will at their command stand still."- Joe Hill

  10. None of this means our emancipation is inevitable. So the most important reason to look forward to a brighter future is that we are here and we are going to concentrate our efforts of heart and arm and brain, to democratise and collectivise our world.
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Jan 6, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  ungeiweka yooote kwa kiswahili....
   
 3. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #3
  Jan 6, 2012
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,583
  Likes Received: 1,944
  Trophy Points: 280
  Nimekupata Bawse, ngoja nitajitahidi mkuu kuona kama nitaweza kupata tafsiri nzuri, ila tusaidiane pale inapowezekana.
  Hii namba nne iko wazi kabisa...
  Hii hapo juu tungekuwa na viongozi wenye akili, basi wangeiona mapema sana...
   
 4. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #4
  Jan 6, 2012
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,583
  Likes Received: 1,944
  Trophy Points: 280
  Kwa mfumo tunaoufuata, haitowezekana kamwe kuwa eti mafisadi wataridhika siku moja na kuanza kuwajali masikini...

  Watanzania fungukeni macho!

  Ubepari tuliourithi sisi hauwajali masikini hata kidogo! Na msije mkajiliwaza kuwa kupiga kura kutawabadilishia viongozi na kudhani kuwa mtawapata viongozi watakaowajali ndani ya system hii!

  Mataifa makubwa yenye kufuata ubepari yana wasaidia masikini wao kwa njia ya social services, un eployement, welfare nk.

  Kwahiyo hata mh Rais aliposema tatizo letu hatuna wawekezaji wa kutosha, basi msidhani hata wakipatikana hao anaodai watatosha basi ndo ufisadi utaisha ama tutapata maendeleo, hilo si kweli! Ukweli ni kwamba wao ndo watazidi kuneemeka!

  Kama viongozi walishindwa kukaa chini na kuamua ni direction gani taifa letu itaifuata, basi ujuwe hakutakaa kuwepo na mabadiliko as long as watandelea kujineemesha kwa mgongo wa masikini.

  Na masikini walio wengi wa bongo ndo kamahivyo, pilau tu, yani fisadi anazaa mtoto, anakuwa, anaendelea kugawa pilau na kukabidihiwa uongozi wa nchi.

  Kuna wengine hilo tumekataa!
   
 5. ubun2

  ubun2 Senior Member

  #5
  Jan 6, 2012
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 145
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Rising against the Oligarchy who have exploited and stolen ppl's lives and futures happening all over the globe. Sign of the times. The ppl of the country of the great writer Chinua Achebe are leading the way against oppression, stolen futures right now in their fight against corruption, bad rulers in their country. The Arab spring, OccupyWallStreet, Anna in India, and the year 2012 begins with Africa Rising against corruption. Enough is enough!!
  If anyone wants to know more about OccupyNigeria follow hashtag #occupynigeria on twitter. This revolution is on Twitter.
  If anyone interested in conversations on endemic corruption in Tanzania, should be on twitter discussing it.
   
 6. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #6
  Jan 6, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Tujivunie amani tuliyo nayo na kamwe tusikubali watu wachache kutuingiza katika maisha ya sintofahamu usalama wangu na familia yangu kila kukicha. Tuangalie mapinduzi yaliyofanyika katika nchi za kiarabu na tutafakari manufaa waliyoyapata wananchi wa kawaida baada ya mapinduzi hayo.
   
 7. Mwali

  Mwali JF-Expert Member

  #7
  Jan 6, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 7,032
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Mi nimeipenda kweli na nikaanza kuhisi moyo wa Che Guevara au Mao unaijia ila nilipofika hapo kwenye kiingereza ukaendelea na safari, mi nikabaki nyuma. lol
   
 8. Kibona

  Kibona JF-Expert Member

  #8
  Jan 6, 2012
  Joined: Sep 16, 2010
  Messages: 1,021
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Tukifikia hatua ya waarabu itakuwa ni maendeleo sana. Sie tuko nyuma mno Kenge! tukiamka tutaelekea waliko waarabu na waafrika magharibi. Usijidanganye kuwa kuna amani Tanzania, hakuna amani inayokuja bila haki. Kilichopo hapa ni usingizi wa pono, wee unadhani nani amepiga hatua kati ya aliyeamka akatambua kuwa kuna mtu anamwibia na akaanza kukabiliana nae, na mtu yule ambaye amelala usingizi na anaibiwa halafu anayemwibia anazidi kumpulizia dawa ya usingizi ili asiamke?
   
 9. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #9
  Jan 6, 2012
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,178
  Likes Received: 1,182
  Trophy Points: 280
  Acha uoga wewe au na wewe ni mnufaikaji wa mfumo hu wa kundi la wala bila kunawa tena kwa mikono miwilimiwili?
   
 10. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #10
  Jan 6, 2012
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,178
  Likes Received: 1,182
  Trophy Points: 280
  Kuogopa kufa nao ni ubinafsi wa hali ya juu kabisa,ambo umejikita kita katika vichwa vya wasomi wengi hapa tz. tukumbuke jinsi tunavo zidi kuwachekea hawa mafisadi ndivo tutakavo zidi kuyavuna mabua.
   
 11. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #11
  Jan 6, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Hizi ndio akili na mitazamo ya watu wetu walio wengi huku mtaani......
   
 12. p

  plawala JF-Expert Member

  #12
  Jan 6, 2012
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 627
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inawezekana yeye ana uhakika na huo usalama na familia yake,huu ndio udumavu wa akili
   
 13. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #13
  Jan 6, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  anza wewe kujitoa muhanga wengine tutafuata
   
 14. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #14
  Jan 6, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  wengine tuna watoto na familia kwenda msituni hapana, tuingie kwenye meza ya mazungumzo
   
 15. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #15
  Jan 6, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  kama Nyerere aliweza kutuletea uhuru kwa mazungumzo bila kumwaga damu, miaka hamsini baada ya uhuru kwa nini tukimbilie msituni au kujitoa mhanga
   
 16. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #16
  Jan 6, 2012
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,178
  Likes Received: 1,182
  Trophy Points: 280
  Mkuu nauita ubunafsi ulovuka mipaka.
   
 17. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #17
  Jan 6, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  magaidi utawajua tu kwa hitimisho lao katika kupata SULUHU YA migogoro katika jamii... haya ni mawazo ya uharamia wa kisomali
   
 18. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #18
  Jan 6, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  nani kakudanganya kwamba bunduki iliwahi kuleta amani ya kudumu duniani,
   
 19. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #19
  Jan 6, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  anayetaka kwenda msituni hatangazi you are not serious, huwezi kuchukua madaraka kwa tangazo la kujitoa mhanga hapa jf
   
 20. BONGE BONGE

  BONGE BONGE JF-Expert Member

  #20
  Jan 7, 2012
  Joined: Oct 19, 2011
  Messages: 3,399
  Likes Received: 1,524
  Trophy Points: 280
  ........hakuna amani ya kujivunia kwa sababu hatuna amani; usiposikia milio ya risasi, sio tafsiri ya amani hiyo, sema tubaki na woga wetu na sio amani yetu!!!!
   
Loading...