Ten Hag anyoosha mikono, ataka Ronaldo aondoke Man United

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,458
CR7.jpg

Kocha wa Manchester United, Erik ten Hag inadaiwa kuwa amebadili mawazo yake na anataka Cristiano Ronaldo aondoke klabuni hapo baada ya awali kunukuliwa akisema kuwa Mreno huyo yupo kwenye mipango yake

Taarifa za ndani ya klabu hiyo zinaeleza kuwa imekuwa ngumu kwa Ten Hag kufanya kazi na Ronaldo ambaye amekuwa akipishana mitazamo na baadhi ya watu klabuni hapo kiasi kwamba kuna siku anaamua kula chakula cha mchana akiwa amejitenga pindi wanapokuwa klabuni

Aidha, inadaiwa Ronaldo amekuwa akipinga mbinu za kocha wake mara kadhaa mazoezini. Inakumbukwa pia baada ya filimbi ya mwisho katika mchezo uliopita dhidi ya Brentford, Ronaldo alikataa maelekezo ya Kocha Msaidizi Steve McClaren kwenda kuwashukuru mashabiki wao licha ya kufungwa magoli 4-0.

-------------------------

Erik ten Hag 'has changed his mind and is now open to letting Cristiano Ronaldo LEAVE Man United... with wantaway star eating alone at Carrington and arguing against high-pressing approach'

Erik ten Hag has reportedly had a change of heart regarding Cristiano Ronaldo's future at Manchester United and is now open to letting the wantaway forward to leave.

The 37-year-old's future at Old Trafford has been up in the air ever since he declared his intention to quit the club earlier in the summer following their failure to qualify for the Champions League.

Ten Hag - who became the club's first manager in 101 years to lose his first two games following their 4-0 hammering at Brentford on Saturday - has remained adamant throughout the transfer window that Ronaldo remains part of his plans for this season.

Reports claim his difficult reintegration into the United squad is behind his change of heart

But The Athletic claim the 52-year-old has now changed his mind and is open to letting Ronaldo leave, citing his difficult reintegration back into the squad after he missed most of pre-season due to family reasons.

The report claims that since returning to the fold, there have been days where Ronaldo sits by himself during lunch at the canteen at their Carrington training ground.

The same outlet reports there have also been instances of him flapping his arms about in training and trying to argue against the high-pressing approach implemented by Ten Hag.

Sportsmail understands that while Ronaldo is said to be training well, he exchanged words with Ten Hag's No 2 Steve McClaren at the final whistle after refusing to applaud United's travelling fans, and there is a feeling that his mood is having a negative effect on the dressing room.

Source: DailyMail
 
Amechelewa sana kufikiria hivyo, Ronaldo pekee haitoshi pamoja na Rashford ambaye alianza kuleta jeuri kipindi cha Jose Mourinho huyo naye awe miongoni mwao yaani kwa ufupi Man U haitakiwi iwe na staa maana jina lake la Man U tu latosha yaani mcheza bora atokee kwa maelekezo ya kocha.
 
Ana haki mwacheni aondoke. Timu linafungwa tu. Linamzuia kuondoka aisee 😂😂😂
 
Na bado wanakutana na liver mechi ijayo lazima watunguliwe kama kawaida.

Sijui siku wakikutana na hii arsenal ya moto watabondwa ngapi hawa wateja wa arsenal.
 
Yule kocha aliepita alishauri kuwa kuna wachezaji kama 10 inabidi waondolewe kabisa hapo Man U ila wamepuuza
 
Unapokua kocha afu umetokea timu ndogo, wachezaj wenye majina makubwa lazima wakusumbue TU.

Angalia trend ya makocha waliopita psg,
 
Back
Top Bottom