Tembosa
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 3,938
- 3,211
Wana MMU,
hasa wale wanaofuatilia hili jambo langu
Kwa ukaribu, niendelee kuwashukuru sana kwa
Ushauri ambao mmeendelea kunipa,
Wengine mlinishauri moja kwa moja na wengine
Mlidiriki kuja hadi PM kuonyesha kuguswa kwenu
Na mambo yanayoendelea katika maisha yangu,
na asanteni sana
Kwani mliniambia kuwa nimo kwenye maombi yenu.
Pia naomba kwa wale ambao mlishauri na sikuweza kufuata ushauri wenu
Msiache kendelea kunishauri, ninawaomba..
Kama nilivyowaahidi kuwa Jumapili nilipanga kwenda kuonana na
Mama Vane ili anisaidie katika ushauri na niliamua kuuvaa moyo wa ujasiri
Kweli kweli kwani hili halikuwa jambo dogo kwangu.
Sasa ile jumamosi nilifikiria sana ningewezaje kuonana na
Huyu mama kwani sikuwa na mawasiliano naye.
Nilifikia maamuzi niende kusali kanisa la nyumbani pale mtaa wa Neema
kwani na wao husalia hapo na mimi niliwahi kusali sana hapo kipindi sijaanza kujitegemea,
nikiamini ningeweza kukutana na Mama V kwa urahisi,
sema rohoni nilipata shida sana kuwa nitamwanzaje na isitoshe lazima angekuwa na mume wake pale kanisani.
Nilipiga moyo konde na kujipa ujasiri kuwa I have to do this,
kama nilivyowaambia mwanzo,
ni lazima nitafute suluhu ya hili walau basi na mimi niishi kwa amani hata kama siyo kwa furaha,
nikiwa na amani at least ingesaidia na ningeweza kufanya mambo mengine ya kimaisha.
Basi nikampigia simu
Yule cousin wangu (niliyekuwa naishi naye pale home kipindi kile),
hope Tyta na watu8 mnamkumbuka.
Nikamweleza kuwa kesho(jumapili) nitakuja kusali Neema ibada ya kwanza
ambayo huwa inaingia saa moja asubuhi.
Akaniambia hamna shida na nikaribie,
sikumweleza kabisa dhamira yangu ya kwenda kusalia pale hiyo jumapili,
kwani tokea nihame sijawahi kabisa kufanya hivyo.
Jumapili asubuhi ikafika na nilijitahidi sana kuwahi kuamka ili niwahi Mbezi,
sikuwa na Gari so ilinilazimu
Nikapande daladala,
na nilifanya kila kitu kwa wakati,
Nilifanikiwa kufika maeneo ya kanisa na ibada ilikuwa bado haijaanza
Sasa nikawa nasalimiana na baadhi ya waumini pale,
ambao nilikuwa nawafahamu
Hapo bado sijawa stable kabisa,
sijui ujasiri wangu uliishia wapi,
nikajiona kama mtoto kidogo niahirishe lile kusudio langu,
Wakati naendelea kusalimiana na wale waumini ambao walikuwa hawajaingia kanisani gafla nilisikia mtu akiniita, nilishtuka sana alikuwa Mama yake Vanie,
alikuwa yupo na kijana mmoja mdogo na kasichana kengine kadogo dogo tu!
Nikamsogelea nakumsalimia,
akaniuliza habari za siku nyingi?
Nikamwambia ni nzuri tu!
Mama huku anatoa sadaka kuwapa wale watoto akamwambia
Yule wakiume akamtafutie Bahasha yake.
Wakaenda,
mimi bado nimesimama pale
Enhee kijana bado unafanya kazi kule Temeke?
Nikamwambia ndiyo mama,
Ahaa! Akaniuliza unahabari kuwa Vanessa alikuwa amelazwa hospitalini?
Nilishtuka kidogo,
kalazwa!!
Akaniambia ndiyo alilazwa kama siku 3 hivi pale Muhimbili,
nikauliza tatizo ni nini?
Kabla hajanijibu akaniuliza kwani baada ya ibada unashughuli gani?
Nikamwambia nilipanga kwenda kuwasalimia wazee wangu,
akaniuliza kwa hiyo leo utashinda Mbezi au?
Nikamwambia ndiyo nimepanga kufanya,
akaniambia kabla hujaondoka naomba upite pale nyumbani tuongee kidogo..
Muda wa ibada ulikaribia kabisa ilibidi tuanze kuingia kanisani,
nikamwambia mama Vanessa nitaenda kwake mchana.
Hapa tayari akili ilianza kunikaa vizuri kwani nilijua Huyu Mama kuna kitu kashaambiwa na mtoto wake .

Last edited by a moderator: