Tembo wetu wanaangamia, waziri kagasheki chukua hatua kali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tembo wetu wanaangamia, waziri kagasheki chukua hatua kali

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ICHONDI, Oct 25, 2012.

 1. I

  ICHONDI JF-Expert Member

  #1
  Oct 25, 2012
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 588
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Hii habari imetokea National Public Radio ya Marekani leo asubuhi saa za marekani. Niko ziara ya kikazi nchini Marekani na mwenyeji wangu akafungulia NPR kweney gari hii habari ikanishitua sana.

  Biashara ya pembe za ndovu imeshamiri Tanzania, majuzi contena lililosheheni pembe za ndovu toka Tanzania lilikamatwa huko Hong Kong. Chadema na wapenda wanyama wote tusimame kidete kupigia kelele huu unyama wa kuangamiza tembo wetu na Raisi JK utangaze kuwa tembo sasa ni endangered animal ili wapewe ulizni wa kutosha
  Please listen the video clip in the link below, is very disturbing

  http://www.npr.org/
   
 2. baina

  baina JF-Expert Member

  #2
  Oct 25, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 221
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu mwana jf hata husijisumbue hawa mawaziri wa mr. dhaifu hawana lolote zaidi ya kuendekeza wizi. kagasheki yupo bukoba anasimamia chaguzi zenye kunukia rushwa huko bkb.
   
 3. M

  Mthuya JF-Expert Member

  #3
  Oct 25, 2012
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 1,415
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Tanzania Ni sarakasi tupu kila mtu mwizi
   
 4. I

  ICHONDI JF-Expert Member

  #4
  Oct 26, 2012
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 588
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Wanabodi wenzangu hii issue ni nzito tuichangie jamani wahusika wasikie
   
 5. Baba V

  Baba V JF-Expert Member

  #5
  Oct 26, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19,507
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  Mkuu usidhani kuwa wahusika hawajui, la hasha wanajua vizuri sana,kitakachowaumiza vichwa hapa ni kwa nini mimi na wewe tumejua, jk sio kwamba hafahamu haya, alimuweka Maige pale ili acheze muziki atakaopiga yeye jk. nchi imekwisha hii. utaona hatua ambayo serikali yetu itachukua. Our LOVELY CORRUPT CHEAP GOVERNMENT!
   
 6. m

  masomo JF-Expert Member

  #6
  Oct 31, 2012
  Joined: Oct 25, 2012
  Messages: 208
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Huu ufisadi wa kuwauwa tembo katika hifadhi zetu utatufikisha mahali ambapo tembo wote wataisha na itakuwa kama faru ambao waliuliwa hadi kwisha.hali hii ya tembo kuuliwa kwa wingi sana nimebahatika kuona baada ya kubahatika kufanya kazi pembezoni na maeneo ambayo yamepakana na hifadhi ya selous pamoja na kufanya kazi ndani ya hifadhi hii.Mara nyingi nikiwa ndani ya hifadhi pamoja na game scouts tulishuhudia tembo wengi wameuliwa katika maeneo mbali mbali ndani ya hifadhi na pia tuliwahi kukutana na vitisho vya majangili hao na hata kuwaona na kukimbizana nao.wapo watu ndani ya hifadhi wanafanya shuguli ya kuchimba madini ya dhahabu,watu hawa kwa asilimia kubwa ni moja ya mahangili na ni vema serikali ingepambana nao na kuwaondoka ndani ya hifadhi haraka iwezekanavyo.

  Kitu nilichojifunza ni kwamba wakubwa wengi ndiyo wanaojihusisha na ujangili kwa kuwatumia vijana maskini wanaotoka jirani na hifadhi, na pia nilijifunza kuwa hakujakuwa na dhamira ya kweli kupambana na ujangili huu.Nilijifunza ni rahisi sana kuwakamata majangili iwapo serikali ingekuwa na dhamira ya kweli.Mimi binafsi naona hii ni kazi rahisi sana.
  Kama serikali inadhamira kukomesha ujangili inatakiwa sasa iwajibishe viongozi wake woke katika kanda na kuweka viongozi ambao watatakiwa waukamate mtandao wa majangili ndani ya hifadhi zetu.Kama watashindwa hao viongozi basi wapeleke jeshi la wananchi likapigane nao.
   
 7. Tetty

  Tetty JF-Expert Member

  #7
  Oct 31, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 25,630
  Likes Received: 16,583
  Trophy Points: 280
  Naomba ni kusahihishe kidogo,siyo sahihi kusema KUULIWA au WALIULIWA unatakiwa kusema WALIUAWA,Badala ya HAKUJAKUWA nadhani ni sahihi kusema HAKUNA .
   
 8. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #8
  Oct 31, 2012
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Unajua,matatizo haya ni ya kimfumo,so unless mfumo ulio-institutionalize mambo haya unakuwa dismantled hayataisha.Sasa serikali yenyewe ni sehemu ya mfumo huo,and infact only a very small part of it.This is a world wide network of Mafia style people of the NWO wanting to make themselves rich by any possible means so as to advance their NWO agenda.Unluckily enough kama nilivyosema, our government is part of that agenda.
   
 9. COURTESY

  COURTESY JF-Expert Member

  #9
  Oct 31, 2012
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 2,018
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Hii nchi ni kama shamba la bibi acha watu wajisevie mkuu!!
   
 10. N

  Nero Member

  #10
  Oct 31, 2012
  Joined: Apr 24, 2012
  Messages: 93
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Binafsi nimshkuru mleta mada, Watanzania wenzangu jambo hili tulichukulie very seriously hakika tembo wetu wanatoweka. Wanyama hawa wanawindwa zaidi na majangili ktk mapori ya akiba, mapori tengefu ambazo nyingi zipo chini ya Halmashauri za wilaya na maeneo ya wazi (open areas).

  Watu wengi wamekuwa wakitupa lawama kwa wale tuliowapa dhamana ya kulinda & kutunza rasilimali zetu hasa kwa ngazi za Halmashuri (District Game Officers).

  Mabwana hawa wanakabiliwa na changamoto nyingi kama vile ukosefu wa vitenda kazi (gari kwa ajili ya doria, silaha, mafuta na uhaba wa watumishi hususan askari ktk (H) nyingi), idara hii muhimu imebaki kuwanafaisha wachache hasa wa ngazi za juu, na hata miradi hizi za ujangili wanaweza kuhusika.

  Ili kunusuru rasilimali zetu napendekeza mfumo wa usimamizi wa wanyamapori ubadilishwe kwa maana ya kwamba watumishi wote idara ya wanyamapori kwa ngazi za halmashauri wahamishiwe serikali kuu na usimamizi wa wanyamapori wilayani ziwe chini ya serikali kuu pengine changamoto zile zinaweza kupungua.

  Nauliza mchakato ule wa kuanzisha Wildlife Unity imeishia wapi?au ilitoweka na Maige? Pendekezo lingine ni iangaliwe pia mchango wa mashirika ya umma m.f NCAA na TANAPA katika kulinda rasilimali zetu zilizopo nje ya hifadhi za Taifa.

  Au tuanzishe chombo kimoja pekee nchini ya kutunza wanyamapori wetu mfano mzuri hiyo Wildlife Unity. Natengemea mchango zaidi kutoka kwa wataalam wa idara ya Wanyamapori.
   
 11. C

  Chongombili Member

  #11
  Oct 31, 2012
  Joined: Oct 26, 2012
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni mawazo mazuri sana ndugu Nero, Asante sana kwa mchango wako unojaribu kutoa way foward, tusubiri labda wataalam kutoka idara hiyo wanatuambiaje. Kweli watanzania hii ni aibu kubwa lazima tuchukue hatua.
   
 12. S

  SJUMAA26 JF-Expert Member

  #12
  Oct 31, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 611
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  It is a widely accepted quote, IF YOU CANNOT DEFEAT THEM, JUST JOIN THEM! Hivi nyie mnadhani tuna serikali ya kupambana na ujangili huu? Hii serikali imeshazidiwa, haina uwezo tena. Kama Sheikh Ponda Mali tu anaweza kuiyumbisha nchi kiasi hiki, sembuse huo mtandao mnene namna hiyo? Dawa ya moto ni moto, kama wanaiba na wewe ukipata nafasi piga, hapo heshima ndio itakuwepo! Ukijifanya hupigi wakati wenzio wanamega itakula kwako. Tukishamaliza kila mtu atabaki anakula alichoiba. Sasa kama wewe huibi na wenzio wanamega baadaye vikaja kuisha wewe utakula nini? Wakati wenzio watakuwa wanakula walivyojisevia mwanzo, wewe utaanza kulala barabarani ukipandamana! Nani atakusikia? Chezea Chama cha Majambazi (CCM) wewe?
   
 13. T

  Topi Member

  #13
  Oct 31, 2012
  Joined: Feb 7, 2012
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naona wengi wanakata tamaa bcoz ya serikali dhaifu na fisadi ya CCM. Bado tuna nafasi watanzania ya chukuakua hatua na kunusuru Tembo wetu. Tusikate taama ndugu zangu.
   
 14. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #14
  Oct 31, 2012
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Majangili haikosi wanashirikiana na Maaskari wa Hifadhi pamoja na Mabwananyama. Iweje kila mara KINAPA, Serengeti, Manyara, Tarangire, Yaeda Chini n.k. kila siku wanyama wanauawa na hakuna hatua madhubuti zinazochukuliwa huko Wahifadhi Wakuu wanatembelea viyoyozi.

  Kagasheki anatangazia udhaifu wetu kwa mataifa ya nje. TANAPA wenyewe wanaunga mkono barabara kuu ipitie katikati ya hifadhi. Ni dhahiri kuwa hawana nia ya dhati ya kuhifadhi.

  Je, tunahifadhi au tunahafidhi?
   
Loading...