Tembo waua sita, wajeruhi saba katika kipindi cha miaka miwili

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,010
9,874
1609758151806.png

WANANCHI Sita wameuawa na wengine saba kujeruhiwa vibaya kwa kushambuliwa na Tembo katika Kijiji Cha Makuyuni wilaya ya Monduli ,Mkoani Arusha katika kipindi cha miaka miwili na kusababisha wakazi wa Kijiji hicho kuishi kwa hofu.

Aidha Tembo hao wanadaiwa kuvamia pia mashamba ya wananchi hao na kufanya uharibifu wa mazao yao jambo lililosababisha wakose chakula katika kipindi Cha miaka miwili na kuishi maisha ya tabu.

Hayo yameelezwa jana na Mwenyekiti wa Kijiji Cha Makuyuni, wilayani humo Ngayoo Measi katika mazishi ya Mkazi mmoja wa Kijiji hicho, Ester Sindiyo (55) aliyeuawa na Tembo Desemba 21 mwaka huu wakati akiokota kuni na kuiomba serikali kusaidia kuwaondoa Tembo hao.

Amesema Vifo hivyo na majeruhi vimetokana na makundi ya Tembo yanayovinjari Kijijini hapo nyakati za usiku huku kukiwa hakuna jitihada zozote zinazochukuliwa na serikali katika kuwadhibiti wanyama hao wanaotoroka kutoka hifadhi ya Tarangire na Manyara kusaka malisho.

Mwenyekiti huyo aliwataja marehemu waliouawa na Tembo kwa nyakati tofauti kuwa ni Janeth Silla, Mamalai Kakuyu, Lemomo Lenguriny, Kastuli Jumalei, Emanuel Leroo na Ester Sindiyo wote wakazi wa Kijiji hicho.

Pia aliwataja majeruhi wa tembo hao kuwa ni Lobulu Mollel, Julius Thobias, Saiguran Mika, Mnyak Lenguriny,Mjomba Soingei bado amelazwa katika hospital ya rufaa KCMC, Lobikyeki Sanare na Kalai Lomayani wote wakazi wa Kijiji cha Makuyuni na kwamba taarifa za matukio hayo wamekuwa wakizitoa katika ngazi mbalimbali.

Naye diwani wa kata hiyo Elius Odupoi aliwataka wananchi kuchukua tahadhali ya kujilinda wenyewe na kuacha kutembea nyakati za usiku ikiwemo kufanya shughuli za kijamii majira ya usiku.

"Watu wetu wanauawa na Tembo na wengine wanajeruhiwa tunaendelea kuikumbusha serikali iongeze nguvu ya kudhibiti Hawa Tembo ,na sisi wananchi tupunguze kufanya shughuli zetu nyakati za usiku na suala la ulinzi linaanza na sisi."alisema Diwani.

Mmoja ya mwananchi wa Kijiji hicho, Peter Laisangai alimeiomba serikali kuongeza fidia kwa wahanga wa wanyamapori kwani kiasi cha Sasa kinachotolewa na serikali cha sh.500,000 kwa aliyejeruhiwa na shilingi 1,000,000 kwa aliyefariki ni kidogo.

"Tunaiomba serikali kupitia upya kiasi kinachotolewa kama kifuta jasho kwa waathirika wa wanyamapori kwani hakiendani na thamani ya mwananchi anayelinda rasilimali hizo."alisema Leisangai

Naye afisa wanyamapori wilaya ya Monduli, Seraphino Mawanja aliyehudhuria mazishi hayo alisema katika kipindi cha miaka miwili maeneo hayo yamekuwa na changamoto kubwa ya ongezeko la Tembo ambao walihama kutoka hifadhi ya Tarangire baada ya mvua nyingi kunyesha na maeneo yao kujaa maji.

Alisema serikali imekuwa ikichukua hatua kadhaa kuwaondoa Tembo hao wanaovamia maeneo ya makazi kwa kuweka askari wa doria.

Hata hivyo alisisitiza kuwa serikali inajitahidi kufidia wananchi wanaoathiriwa na Tembo kwa kutoa kifuta jasho cha shilingi Milioni moja kwa aliyeuawa na Tembo na Tsh. laki tano kwa majeruhi.
 
Nimekaa sana Monduli, kuna kijiji wanakiita Loksale. Poleni wafiwa.

Ninasikia tembo wana tabia ya kutosahau njia yao hata kama waliipita miaka 3 nyuma.
 
Ifike mahali wanyama pori wakiumiza wananchi nje ya mapori yao waathirika walipwe fidia kubwa maana ni serikali chini ya TAWA imeshindwa kutekeleza majukumu yake ya ulinzi wa wananchi na mali zao.

Mwananchi akijeruhiwa nje ya hifadhi fidia iwe not less than 50m/= kutegemea na kiwango cha athari alizopata; akiuliwa warithi walipwe not less than 350m/=. Akiharibiwa mazao shambani iwe not less than 3m/=; akivunjiwa nyumba au mali nyinginezo kama magari, n.k. fidia iwe sawa na thamani ya mali iliyoharibiwa + 25% maana hata bima do not cover such incidents.

Ni kwa utaratibu huo wahusika/serikali itawajibika. Wananchi sio kwa ajili ya wanyama bali wanyama kwa ajili ya wananchi.

Huwa nikipita pale Mikumi nikiona fines wananchi wanazotozwa kwa kumgonga digidigi aliyeingia barabarani lakini mwananchi akiuliwa na mnyama nyumbani kwake hakuna fidia yoyote nakereka sana.
 
Back
Top Bottom