Tembo wameniathiri baada ya kuvamia mazao. Naomba ushauri wa biashara

PANTHERA LEO

JF-Expert Member
Jan 25, 2019
2,307
3,431
Habari wakuu?

Natumaini mko poa!, Mimi ni kijana naishi kijijini baada ya mipango ya kazi kubuma. Kijiji ninachoishi zamani tulikuwa tunalima na kufanya ufugaji ila miaka miwili iliyopita shuhuli zote zimekwama kutokana na kuvamiwa na tembo. Ni miaka miwili sasa hakuna kilimo na ufugaji ni wa shida sana.

Sasa basi ninafanya kazi ya ufundi ambayo kazi huwa zinapatikana kwa msimu, pia najitaidi kufanya na ufugaji wa mbuzi kidogo kidogo. Hapa kwenye kata yetu watu sio wengi sana ila kuna huduma zote muhimu.

Nilikuwa naomba wazo la biashara ambayo nitaweza kufanya bila kuathiri shughuli zangu nyingine. Mtaji usipungue milioni 1 au kuzid milion 6.

Kutoka hapa hadi mji mdogo nauli ya gari ni 3000/= hadi mji mkubwa ni 7000!=

Kuna watu hapa wamewekeza kwenye kukodisha mziki, maturubai, viti na sufuria za sherehe. Kwa hiyo yani nataka kitu kinachofanana na biashara hiyo ambacho hakitaathiri shuhuli zangu
 
Siyo lazima utafutie kijijini kwenu hama, tafuta mahali penye mzunguko mkubwa wa pesa anza biashara hapo lkn huko usangini na ugwenoni kutoboa ni ngumu kwasbb wapo nguli ambao wnana kujua abc zako
 
Siyo lazima utafutie kijijini kwenu hama, tafuta mahali penye mzunguko mkubwa wa pesa anza biashara hapo lkn huko usangini na ugwenoni kutoboa ni ngumu kwasbb wapo nguli ambao wnana kujua abc zako
Sio kwetu.. Mkuu sio usangi ni tambarare
 
Back
Top Bottom