Tembo Wa India Hupandwa Mgongoni Tembo Wa Bongo Kwanini Hawapandwi?

UMASIKINI BWANA

JF-Expert Member
Oct 17, 2013
942
566
Wadau Nimeona Clip Moja Ya Ndoa Za Kihindi Bi Harusi Na Bwana Harusi Wamepanda Mgongoni Mwa Tembo Vp Hawa Wa Kwetu Tunaweza Fanya Hivyo?
 
Wadau Nimeona Clip Moja Ya Ndoa Za Kihindi Bi Harusi Na Bwana Harusi Wamepanda Mgongoni Mwa Tembo Vp Hawa Wa Kwetu Tunaweza Fanya Hivyo?
Ng'ombe wa India kwann hawaliwi.... ila wa hapa bongo wanaliwa

Nipe jibu hapa kisha ntakujibu swali lako
 
Yule inaonekana huwa anaandaliwa akiwa bado mtoto kabisa.
Wanacheza na psychology yake kwa kumfunga kamba shingoni tangu akiwa mdogo...
 
Wadau Nimeona Clip Moja Ya Ndoa Za Kihindi Bi Harusi Na Bwana Harusi Wamepanda Mgongoni Mwa Tembo Vp Hawa Wa Kwetu Tunaweza Fanya Hivyo?
India hata nyati wanatumika kulima mashambani wakikokota plau za kulimia hapa kwetu ulikutana na nyati lazima ukimbie na kujisaidia haja kubwa. Tembo india kwao huwatumia Kama punda waweza kuta wanakokota mzigo wa tofali karibu lori zima wanapeleka eneo la ujenzi toka kwenye eneo la matanuru. Wahindi unaweza kutana naye anaswaga nyati kama mia na tembo Kibao Kama mifugo ya kawaida.
 
Wale tembo wa india ni specie tofauti na tembo wa africa hivyo hata tabia zao zinatofautiana. Ukitaka kugundua jaribu kutafuta picha zao alafu linganisha ukubwa wa vichwa, masikio na maumbile mengine. Kwa ujumla kuna aina tatu za tembo zilizobakia / zinazofahamika duniani. Aina mbili zipo afrika nazo ni african bush elephant (loxodonta africana) na african forest elrphant (loxodonta cyclotis). Aina moja ya mwisho inapatikana asia na ndio pamoja na wale tembo wa india na inaitwa asian elephant (elephas maximus). Zile aina mbili za africa ni ngumu kidogo kuzitofautisha ila tembo wa asia na wale wa africa tofauti zao ziko waziwazi hadi tabia zao.
220px-Elefants_comparative_anatomy.png

1.asian elephant 2. African elephant

220px-Elephas_maximus_(Bandipur).jpg

Asian elephant (kama wale wa india)

220px-African_Bush_Elephant.jpg

African bush elephant

220px-African_Forest_Elephant.jpg

African forest elephant.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom