Tembo wa Hifadhi ya Taifa Serengeti washitakiwa Serikalini, wananchi waomba chakula cha msaada

comrade igwe

JF-Expert Member
Jan 12, 2015
7,295
3,939
Wana jamvi amani iwe kwenu:

Wananchi wa vijiji vinavyopakana na hifadhi ya taifa ya Serengeti wilayani Bunda mkoani Mara, wamelazimika kuangua kilio wakati wakimwelezea naibu waziri wa kilimo, mifugo na uvuvi jinsi wanavyokabiliwa na njaa kali baada ya makundi makubwa ya tembo kuvamia makazi ya watu na kula chakula kilichohifadhiwa katika maghala huku wakiharibu sehemu kuba ya mazao mashambani.

tembo%285%29.jpg


Baadhi ya wananchi hao kijiji cha kihumbu wilayani bunda,wametoa kilio hicho katika mkutano wa hadhara mbele ya naibu waziri huyo wa kilimo, mifugo na uvuvi Mh William Ole Nasha huku wakiomba serikali kuwapa chakula cha msaada pamoja na kuangalia namna nzuri ya kudhibiti makundi hayo makubwa ya tembo.

Naye mkuu wa wilaya ya Bunda Bi.Yidia Bupilipili, akizungumza wakati akitoa taarifa kwa kuhusu hali chakula kwa kiongozi huyo, amesema wilaya ya Bunda inakabiliwa na njaa kali hasa baada ya makundi hayo ya tembo kuharibu zaidi ya tani mia tano za chakula mashambani.

Hata hivyo naibu huyo kilimo, mifugo na uvuvi Mh. William Ole Nasha, akizungumza na wananchi wa kijiji hicho, pamoja na kutoa pole kwa wananchi wa vijiji vinavyopakana na hifadhi hiyo ya taifa ya Serengeti na mapori ya akiba ya Ikorongo kutokana na athari hizo zinazosababishwa na makundi hayo ya tembo, lakini pia amesikitishwa na idara ya wanyamapori kushindwa kutoa fidia kwa wananchi ambao wamekubwa na tatizo hilo, hatua ambayo amesema imesababisha uhasama mkubwa kati ya wahifadhi na jamii.
 
Juzijuzi tu hawa tembo walikuwa wanajificha, sasa hivi nao wanatanua kitaa! Wenye kazi zao bado wanausoma mchezo!
 
Back
Top Bottom