Tembea Uone

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,201
219
Jana jioni ilikuwa siku yangu ya maajabu kidogo kutokana na vitu ambavyo niliviona sehemu Fulani mjini , nilikuwa nimetoka kazini kwenda sehemu nyingine kwa maongezi nikapigiwa simu kutakiwa kwenda kusoma habari Fulani katika mtandao na nitoe maoni yangu kabla habari hiyo haijaanza kusambaa sana .

Ikabidi niende katika internet café moja mtaa wa jamhuri kwa sababu ndio naona iko haraka haraka katika utendaji wake wa kazi , wakati nafanya kazi zangu nikaona watoto 2 wameingia wamevaa nguo chafu , mmoja anatoa hata harufu , huyu mmoja ninamjua kwa sababu zamani kidogo wakati nasoma chuo nilikuwa nampa hela za kula .

Nilipoongea nae kidogo akaniambia amekuja café kucheza games , kuanzia asubuhi mpaka jioni wanaosha magari au kuomba omba hizo hela wanazopata jioni wanakuja katika internet cafes kucheza games kama watoto wengine wote .

Na huu ndio uzuri wa tekinologia za mawasiliano , mtu akiwa popote anaweza kutumia au kufanyia kazi kama akipewa elimu ndogo tu ya kufanya hichi na kile au akiwa anapenda jambo fulani zaidi .

Mfano hawa watoto sasa wanaenda café kucheza games , wakiwa wakubwa watajinfunza kusoma emails , kufungua na kutumiana email , tatizo ni kwamba wao muda mrefu wanakaa mitaani kwahiyo ni ngumu kujua mambo mengi ya kawaida kama kusoma na kuandika na ndio maana wanaona njia rahisi kwa ni kucheza games .

Haya ni baadhi ya mapinduzi ya kijamii yanayoletwa na tekinologia zetu za mawasiliano na habari , kama mtoto wa mitaani asiyejua kusoma wala kuandika anaingia katika internet café anapewa computer anafungua games na kucheza , kwanini wale watoto wa wenye nazo wanaokaa majumbani wanashindwa kutumia vifaa hivi kwa manufaa zaidi ya hapo walipo ?

Huwa nashangaa kwanini watoto wa mitaani wanawashinda watoto wa majumbani katika mambo kadhaa ambayo ni ya kawaida tu ukiwa na muda , ukikutana na mtoto wa mitaani anacheza games basi yeye hana lingine kwa sababu hajui kusoma wala kuandika .

Mtoto wa nyumbani anatakiwa afanye zaidi ya haya , mfano awe na blog yake ndogo , awe anafanya mambo mengi zaidi ambayo ni changamoto sio kwake tu hata kwa wazazi na ndugu zake wengine wapatwe na moyo ili wapate njia zaidi za kuweza kumsaidia kumpeleka katika hatua zingine za mawasiliano .
 
Back
Top Bottom