Television ya Taifa,TBC, Imetisha!. Yarusha Live Mbili Kwa Wakati Mmoja! Live ya Dodoma on TBC1 At the Same Time Live ya Arusha TBC2- Safari Channel

Inamaana ITV wanaporushaga laiv huwa wanaazima hizo OB Van
No, ob van yenyewe inakuwa imefungiwa link, hivyo vituo ambavyo havina link, wanafunga link kwenye hiyo sehemu au kwenye gari yoyote.

Pia ujio wa technology ya digital kwenye matangazo imerahisisha mambo, wenaweza kutumia high speed internet, karibu mikoa yote ina 4G, hivyo connectivity sio a big issue, the issue ni vifaa vya kurushia, hivyo ITV wanavibeba, na kufanya setting eneo la tukio. Lakini wenye OB equipments ziko ready ndani ya gari tayari kwa kazi.
P
 
Wanabodi
Kwanza wale wenye access, Watch, TBC 1 na TBC 2...shuhudia...!.

Kwa watu wasiojua what it takes kurusha matangazo ya TV live mubashara kutoka sehemu mbili tofauti kwa wakati mmoja, mnaweza msielewe, hapa ninashangaa nini!.

Kiukweli kituo cha Television ya Taifa, TBC, kimetisha!. Kitendo cha kurusha matangazo ya moja kwa moja, Live Mubashara kutoka maeneo mawili tofauti kwa wakati mmoja, sio jambo dogo!. Hongera sana Dr. Ayub Rioba na timu yako.

Live moja ni kutokea jijini ya Dodoma kwenye maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Posta Duniani, live hiyo iko live on TBC1. Wakati huo huo, yaani at the same time, kuna Live ya pili ikitokea Arusha, kwenye uzinduzi wa maonyesho ya Utalii ya Africa Mashariki ambayo iko TBC2- maarufu Safari Channel.

Matangazo ya moja kwa moja ya Redio au TV yanaitwa OB, au Outside Broadcasting.

Ili kituo cha TV kiweze kurusha live, lazima uwe na dude kama hili.
View attachment 1969159
Hilo dubwana, lione tuu kwa nje kama lori tuu, humo ndani shughuli yake sio mchezo!.
View attachment 1969177

Hii inamaanisha sasa TBC inayo hii midude zaidi ya moja.

Leo ndio mara yangu ya kwanza kushuhudia live mbili concurrently zikirushwa na kituo kimoja cha TV. Kwa nchini Tanzania, ukiondoa live za DSTV, na zile za Azam, TBC ndio imefungua pazia la live mbili kwa wakati mmoja. Huu ni uthibitisho TBC ndio TV kiongozi nchini Tanzania.
Hongera sana TBC.

TBC Baba Lao.

Paskali
Wewe ni kada mtafuta teuzi tu ndugu yangu sjui kwa nini uko hvo. Hyo tabia ya uchawa achana nayo ili uwe flexible. Sasa wakirusha hzo live mbili itasaidia nn kama content znalengo la kuisifia ccm tuu. Acha hyo tabia, alafu usiwe kma mshamba technology imesha advance wanachokifanya hao TBC hakina maajabu. Ingekuwa ndo kitu kpya kufanyika hapa ulimwenguni ndo tungeelewa na kuwasifia licha ya maudhui ya hovyohovyo
 
Bado unaangalia TBC!?
Hicho kituo kiboreshwe, hasa kisiwe na mrengo wa wazi wa kisiasa! Kinakwaza sana
 
Kaka Pascali bwana, we mwenyewe umeitaja AZAM kwamba inaweza kurusha mubashara matukio zaidi ya moja kwa wakati mmoja halafu unamalizia kwa kusema eti TBC ndio TV kiongozi, umenichanganya sana hapa. Kwanini hukuwapa pongezi Azam badala yake unatoa pongezi kwa aliye copy? Anyway, sioni ni kwanini TBC washindwe kufanya hivyo ilihali ile ni TV ya taifa na inaweza kupewa pesa zozote kulingana na demand yake, kama sasa ndio wameza kufanya hivyo then tuwalaumu wafanyakazi wa TBC kwa kutokua wabunifu, mtaji kwa TBC sio tatizo kabisa; siamini kama hilo dubwasha unalolisifia linaweza kuzidi bei ya ma V80 (in Polepole's voice ) kadhaa
 
Washauri safari channel watafte ama kutengeneza documentary mpya, kila siku ni kisiwa cha Rubondo tuuu.

Waambie warekodi zile zinaonyeshwa NG Wild halafu watafsiri ama waingize sauti kwa juu kuliko kila siku ni makala zile zile.

Ama hata waweke za sauti ya kizungu hakuna shida.

Mimi ni mpenzi wa makala za wanyama nimeona nitoe maoni yangu.
Kuna copyright issues wakiziweka zile Cha kufanya warekodi zetu wenyewe
 
Bado unaangalia TBC!?
Hicho kituo kiboreshwe, hasa kisiwe na mrengo wa wazi wa kisiasa! Kinakwaza sana
tunatizama sana shanel yetu.hasa has atafakuri baada ya habari.ila siku za hivi karibun aliyekuwa anasoma tafakuri baada ya habari sijui yupo wap.kuna saut ila sio ya yule wa mwanzo.
 
Vituo vingapi ya FTA unavyovifahamu?
DSTV sio TV ya FTA, DSTV ni Cable TV kama ilivyo Azam TV ni Cable TV. Hapa Bongo Tanzania, tuna FTA TV na pia tuna Cable. TBC ni FTA, jee umeisha wahi kuona live mbili za kituo kimoja kingine chochote cha FTA, mimi ndio nimeona leo.
P
 
Wasifie Azam HD wenye picture angavu mpaka anakula tender ya kutembeza ob Van East Africa kurusha mipira live duniani
 
tunatizama sana shanel yetu.hasa has atafakuri baada ya habari.ila siku za hivi karibun aliyekuwa anasoma tafakuri baada ya habari sijui yupo wap.kuna saut ila sio ya yule wa mwanzo.
Aliyekuwa anasoma Tafakuri mwanzo ni Shabani Kissu, sasa amekuwa Mkurugenzi wa Channel Ten, msomaji wa sasa ni Sued Mwinyi.
P
 
Hata tukiachana na azam anayerusha live za mpira 8 kwa pamoja, hata startv wamewahi kurusha live mbili, moja ligi daraja la kwanza huko na nyingine kipindi cha kawaida kutokea daslam.
Labda kama ulijisikia kusifia tu mzee Pasco.
 
17 Reactions
Reply
Back
Top Bottom