Televisheni yafungiwa Zanzibar kwa ukiukwaji maombolezo ya Maalim Seif Sharif Hamad

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
3,938
2,000
1613635185364.png

Tume ya Utangazaji Zanzibar imekifungia kituo cha televisheni cha Tifu kwa muda wa siku saba baada ya kudaiwa kurusha vipindi vinavyokwenda kinyume na uombolezaji wa msiba wa Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad.

Katibu Mtendaji wa tume hiyo, Omar Said akitoa taarifa hiyo alisema kwamba tume hiyo imelazimika kuchukua uamuzi huo baada ya kubaini kwamba kituo hicho katika kurusha wa vipindi vyake katika kipindi hiki, kinakwenda kinyume na muongozo uliotolewa na Serikali kupitia Tume hiyo.

Alisema kufuatia taarifa iliyotolewa na Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Ali Mwinyi hapo jana juu ya msiba wa Makamu wa kwanza wa Rais, Maalim Seif, tume hiyo ilitoa muongozo wa urushaji wa matangazo na vipindi kwa kipindi hiki cha muda wa siku saba za maombolezo kwa vituo vya televisheni, redio na mitandao ya kijamii.

Alisema katika muongozo huo wamevitaka vituo vyote kubadilisha ratiba zao za urushaji wa matangazo na vipindi, na kuandaa vipindi maalum vya maombolezo katika muda huu wa siku saba, huku wakiweka wazi kwamba hawatakuwa tayari kuona kuna kituo kinakwenda kinyume na muongozo huo.

Alisema licha ya hatua hiyo ya kutoa mwongozo kwa vituo hivyo, lakini kituo cha Tifu kimeonekana kwenda kinyume na muongozo huo, hivyo ililazimika kuchukuliwa hatua hiyo, ili kutoa fundisho juu ya kufuata muongozo wa serikali katika urushaji na uandaaji wa vipindi.

“Kwa kweli hatukutaka kuchukua maamuzi haya kwa chombo hiki, lakini kutokana na kukiuka maadili ya muongozo uliotolewa, imelazimika kuchukua uamuzi huo, ifahamike kwamba maamuzi haya yamekuja kufuatia majadiliano na vyombo vingine mbalimbali vya Serikali, juu ya kitendo hicho, na ikaamuliwa kwa pamoja kichukuliwe hatua za kinidhamu,”alisema.

Said aliviomba vyombo vya habari kufuata kikamilifu muongozo uliotolewa na Serikali kupitia Tume ya Utangazaji juu ya urushaji wa vipindi na utangazaji katika kipindi hiki cha msiba wa Maalim Seif aliyefariki jana wakati akipatiwa matibabu jijini Dar es Salaam.
 

Toxic Concotion

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
2,679
2,000
Leo hii baada ya kufa anaonekana wa maana kiasi cha kufungia vituo vya utangazaji. Kipindi cha uhai wake hawakutaka asikike hata chembe.
Kweli unafiki hautoisha duniani. Leo hii Seif Shariff Hamad kawa shujaa wa kuwekewa vipindi maalum, wakati chini ya mwaka mmoja tu alikuwa ni mhaini kwa mujibu wao. Anyways RIP Maalim.
 

Faana

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
17,978
2,000
tume hiyo ilitoa muongozo wa urushaji wa matangazo na vipindi kwa kipindi hiki cha muda wa siku saba za maombolezo kwa vituo vya televisheni, redio na mitandao ya kijamii.
Tume ingeandaa vipindi virushwe sawia kwa TV zote kama kweli inalazimu kufuata nini kirushwe na nini kisirushwe
 

gspain

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
2,773
2,000
Hivi nini maana ya maombolezo? Unawezaje kumlazimisha mtu aomboleze msiba ambao kwake pengine anaona hauna mguso? Ninyi kama serikali mnashiriki maombolezo ya misiba ya wananchi wote?

Tufike mahali hizi sheria na miongozo ya kitumwa tuachane nayo, by the way unatakaje mtu aoneshe sympathy kwako wakati we mwenyewe huna huruma kwake? Kwa nini usioneshe hiyo sympathy wewe angalau kwa kumuonya tu, kulikuwa na ulazima gani kuwafungia?!
 

mwanadome

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
4,511
2,000
Leo hii baada ya kufa anaonekana wa maana kiasi cha kufungia vituo vya utangazaji. Kipindi cha uhai wake hawakutaka asikike hata chembe.
Kweli unafiki hautoisha duniani. Leo hii Seif Shariff Hamad kawa shujaa wa kuwekewa vipindi maalum, wakati chini ya mwaka mmoja tu alikuwa ni mhaini kwa mujibu wao. Anyways RIP Maalim.
Unafiki unaliangamiza hili taifa
 

Giancarlo

JF-Expert Member
May 15, 2018
833
1,000
Kwamba lazima watu wote muomboleze,sasa wafiwa watapata vip faraja maaana kila kituo cha tv kitakuwa kinaomboleza tu mda wote,yaan ukiwasha tv ni maombolezo tu
 

Rutagwerera Sr

JF-Expert Member
Dec 21, 2011
2,487
2,000
Taasisi zingine bwana. Eboo! Kwani lazima mambo mengine yasimame. Na leo ndio anaonekana wa maana sana kiasi hiki loh!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom