Teksi zageuka kuwa shamba la mboga Thailand

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,005
9,872
Katika maegesho ya gari nchini Thailand katika mji mkuu wa Bangkok, utaona mbogamboga zikiwa zimeota katika paa ya magari ya kukodi ambayo yana rangi mbalimbali za kung'aa.

Vizuizi vikali vilivyowekwa nchini Thailand dhidi ya Covid-19 vimesababisha mji huo ambao ulikuwa na hekaheka nyingi kuwa na utulivu, na kufanya madereva wa teksi kukosa kazi.

Baada ya kukosa wateja, madereva wengi waliondoka mjini na kwenda nyumbani kwao vijijini, na kuacha kile kilichoitwa makaburi ya taksi.

Na sasa kampuni moja imeamua kutumia paa za magari hayo ambayo hayafanyi kazi kama shamba la kulimia mbogamboga, ambapo wanatarajia wanaweza kusaidia kuwalisha madereva na wafanyakazi wengine.

Thai staff members of the Ratchaphruek Taxi Cooperative water their community vegetable garden that was built on top of out of use Thai taxis on September 13, 2021 in Bangkok, Thailand.

Wafanyakazi wa taksi za ushirika wa Ratchaphruek wametengeneza bustani ya mbogamboga kwa kuweka udongo juu ya karatasi nyeusi za plastiki.

Wamepanda mbegu mbalimbali za mboga kama pilipili , matango na zukini.

Wana matumaini kuwa baada ya kuwasaidia madereva, chakula chochote kitakachosalia kitauzwa sokoni.


Gari imeandikwa," waziri mkuu tafadhali tusaidie"

Biashara ya taksi mjini Bangkok kwa kawaida inategemea utalii katika sehemu kubwa lakini marufuku yaliyowekwa ya kuzuia wageni kuingia nchini humo ina maana kuwa karibu kila kitu kimesimama.

"Hili ndilo chaguo letu la mwisho," Thapakorn Assawalertkun, mmoja wa wamiliki wa kampuni aliwaambia wakala wa habari AFP, aliongeza kusema kuwa magari mengi yana mkopo mkubwa bado ambao hawajamaliza kulipa.

"Kuotesha mboga za majani katika paa la taksi hakutaharibu magari hayo kwa kuwa kuna mengine ambayo yameshahairibika na hayawezi kutengenezeka . Kuna ambayo yameharibika injini, hayana matairi, hakuna kitu kinaweza kufanyika,"alisema.

1.jpg
 
Hii dunia ukisema ushangae, basi utabaki unashangaa kuanzia asubuhi mpaka usiku kila siku na hautofanya kitu chochote. Inabidi kujifanya kuona kila kitu ni cha kawaida ili mambo yaende!
 
Swali: Magari hayawezi kuharibika ukiotesha mboga kwenye paa la taksi?

Jibu: Kuotesha mboga za majani katika paa la taksi hakutaharibu magari hayo kwa kuwa kuna mengine ambayo yameshahairibika na hayawezi kutengenezeka . Kuna ambayo yameharibika injini, hayana matairi, hakuna kitu kinaweza kufanyika.

Swali: Yanaharibika?

Jibu: Mengine yameshaharibika na hayawezi kutengenezeka.

Swali: Yameharibiwa na upandaji mboga?

Jibu: Kuna ambayo yameharibika injini, hayana matairi, hakuna kitu kinaweza kufanyika.

Muuliza swali: 🙄 🤔

Mtoa jibu: What?🤷‍♂️🤷‍♂️
 
Swali: Magari hayawezi kuharibika ukiotesha mboga kwenye paa la taksi?

Jibu: Kuotesha mboga za majani katika paa la taksi hakutaharibu magari hayo kwa kuwa kuna mengine ambayo yameshahairibika na hayawezi kutengenezeka . Kuna ambayo yameharibika injini, hayana matairi, hakuna kitu kinaweza kufanyika.

Swali: Yanaharibika?

Jibu: Mengine yameshaharibika na hayawezi kutengenezeka.

Swali: Yameharibiwa na upandaji mboga?

Jibu: Kuna ambayo yameharibika injini, hayana matairi, hakuna kitu kinaweza kufanyika.

Muuliza swali:

Mtoa jibu: What?
Hayaharibiki kwasababu wanasema kwamba wanaweka naylon kwenye bodi ma kuweka udogo
 
Hawa jamaa drv tax wanaandamana kwa style yao...hapo wanapeleka ujumbe kwa serekali ilegeze masharti warudi kazini ili.wapate fedha za kujikimu
 
Baada ya msoto mrefu uliosababisha Madereva Taxi wa Thailand kukosa pesa kutokana na sheria kali za Nchi hiyo kudhibiti kusambaa kwa virusi vya corona na kukosekana kwa Wageni kwenye mji mkuu wa Bangkok, Madereva Taxi wameamua kuzigeuza gari zao kuwa 'mashamba madogo' ya kuotesha mboga juu yake.

Vyombo vya habari Thailand vinasema baada ya kukosa Wateja kwenye Mji huo maarufu duniani Madereva wengi waliondoka mjini na kwenda nyumbani kwao vijijini na wengine kugeuza Taxi hizo kwa ajili ya kilimo cha juu ya gari ambacho kinaweza kusaidia kulisha familia za Madereva hao.

MillardAyoUPDATES

Angalia picha chini
FB_IMG_1632253390160.jpg
 
Back
Top Bottom