Teknolojia ya mawasiliano na safari za nje | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Teknolojia ya mawasiliano na safari za nje

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Paul S.S, May 20, 2011.

 1. P

  Paul S.S Verified User

  #1
  May 20, 2011
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Wandugu majuzi Aunt wangu alialikwa na binti yake kwenda USA kwa matembezi, akaja akafikia kwa mwanae wakike mwalimu, wakaanza mchakato wa safari.

  Walihangaika sana kwa takribani mwezi wasijue la kufanya ilibidi waniombe nisaidie maana kikubwa kilichokwamisha ni issue za online.

  Kwanza usumbufu mkubwa ulikuwa kupata pasipoti maombi yalianzia wilayani yakaja mkoani kisha yakatumwa dar, na pasi ilipokuwa tayari ikatakiwa kutumwa tena mkoani kisha wilayani ikachukulie huko,
  Hii ilichukua zaidi ya mwezi tena baada ya kuomba itolewe hapa isirudishwe mkoani. PROCESS NZIMA NI MANUAL.

  Chakufurahisha ni kuwa wao hawakuona tabu ktk hili la pasipoti kuchelewa, majibu kama bado linashughulikiwa wilayani mara mkoani mara bado lipo kwa bosi haikuwa tabu sana kwao.

  Tabu kubwa ilikuwa pale walipotakiwa kufanya kila kitu oline ili kupata visa.

  siku ya jummane tulijaza form online ikatupa access ya kufungua na kuprint pay slip either ukalipie city bank au kwa kutumia ZAP.

  Baada ya malipo unakaa two hrs unaingia tena online unaingiza namba za za pay slip unapata access ya kufanya appointment kwaajili ya interview, bahati nzuri jumatano ilikuwa ipo available tukaichagua.

  Jumatano asbh kaingia ubalozi ndani ya 20 min kamaliza kaambiwa aje kesho yake alhamisi kuchukua visa, JUST SIMPLE LIKE THAT

  Tatizo lingine ikawa ni jinsi gani atapata tiketi yake imeshalipiwa tayar toka USA na imetumwa kwa email.

  Inabidi kuingia tena online ktk web ya KLM unaingiza details za etiket kisha unaiprint, unachagua seat online kisha unaprint board pass kwaajili ya dar airpot,
  Akifika Amstadam anatakiwa kubadili ndege na kuprint tena board pass ktk compyuta zilizopo kila kona pale amstd air port(hapa ilibidi atafutwe mtu mzoefu wasafari amsaidie kufanya hivyo amstdm)

  Ninacho jaribu kuonyesha hapa ni jinsi technolojia inavyoweza kurahisisha mambo kwa kuokoa muda na kukwepa mafoleni na mrundikano wa wateja maofisini.

  Leo kupata visa huitaji kwenda kokote unamaliza kilakitu unasubiri interview tu.

  Wabongo bado tumelala na fursa hizi, leo hii nivigumu kujua kama jina labiashara lipo available ktk site ya BRELA lakini ni rahisi kujua kama id ya paulss inatumika tayari hapa JF, haya mambo ya ajabu kabisa eti unatoka bukoba kuja kusajili biashara Dar ili usije fanya repeatation of names?.

  Hebu angalia mlolongo wa kupata pasipoti ulivyo hivi hao ma IT tech walioajiriwa huko serikalini na mashirika yake wanafanya kazi gani?
  Nisiwalaumu sana pengine wakubwa hawataki maana ulaji utakwisha.

  Pia nimejifunza kuwa sasa dunia inasonga haisubiri mtu, kujua kutumia kompyuta kama end user ni lazima kwa sasa vinginevyo mambo mepesi yatakuwa magumu kwako.
   
 2. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #2
  May 20, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Sasa hapa Tanzania yetu Ukitaka
  • passport inabidi upite kwa wakili au uende kuapa mahakamani hata kama una kitambulisho cha mpiga kura. au una cheti za chakuzaliwa kutoka wakala wa vizazi va vifo
  Sasa watu wa mikooni kupata cheti cha kuzaliwa ni kazi inaweza kuchukua muda wa mwezi na itamgahrimu pesa halali kiasi fulani. So akimalimz akupata cheti cha kuzaliwa kumbe hakimsaidii kitu akitaka passport tena ndo hivyo wakili inbidi lambe kama elfu 20,000 kumgongea muhuri.

  Bado kumbe kitambulihso cha mpiga kura japo kimetolewa na jamuhuri bado hata idara za serikali hawakithamini kama uthibitisho wa Identity.

  Ukisikia ukiritimba at best ndo huo. Wenzetu sio tu tasisi zao za ndani bali hata UK na USA au EU wanashare taarifa za VISA za watu mbali mbali .

  Sasa kwa mambo mengine inabidi tujitamzame na sisi tunaojiita wataaamu wa ICT kama tunaota ushauri mzuri sehemu zetu za kazi.
   
Loading...