Teknolojia ya kuendesha gari kwa kutumia maji imekwama wapi?

raslimali

JF-Expert Member
Nov 4, 2014
1,342
1,010
Kuna teknolojia ipo kitambo ya kuendesha magari na hats mitambo mingine kwa kutumia maji ambapo kifaa hufungwa kuunganisha tenki dogo la maji na injini ya gari.

Kifaa hiki hutenganisha elements mbili zinazotengeneza maji yaani Hydrogen na Oxygen (H2O) na kutumia Hydrogen ambayo ni gesi inayowaka (combustible) na kuipeleka kwenye combustion chambers za injini. Kwanini teknolojia hii haitumiki hapa Tanzania?

Ni teknolojia yenye gharama nafuu na rafiki kwa mazingira na kwa ukanda wa Ozone unaotukinga na mionzi hatari kutoka anga za juu.
 
Ilizuiwa kwasababu maji ni natural resources, na inatakiwa iwe available kwa matumizi mengine (rejea policy za IWRM), sasa assume ikiongezeka issue kama hiyo duh.
 
Hii kitu sidhan Kama kweli..maana maji ni mengi kuliko kitu chochote hapa duniani..karibu asilimia 75-80 ni maji..nadhan labda walikataa kutokana na kwamba hizo ndinga zingeharibu biashara za watu za mafuta
 
Dunia imejaa mabepari, kuruhusu technology hiyo ni kuua biashara ya gesi na mafuta.
 
Wangesema maji ya chumvi basi ndio hayaishi lakini maji freshi basi ingekuwa ndo mseo, tayari kupatikana balaa saa ingine.
 
Dunia imejaa mabepari, kuruhusu technology hiyo ni kuua biashara ya gesi na mafuta.
Kweli, hata ikitokea genius flani avumbue jinsi ya kutengeneza injini za kutumia maji yoyote iwe chumvi au freshi, basi hatoboi, utasikia ameangamizwa na ugonjwa, mara ajali nk
 
Hii kitu sidhan Kama kweli..maana maji ni mengi kuliko kitu chochote hapa duniani..karibu asilimia 75-80 ni maji..nadhan labda walikataa kutokana na kwamba hizo ndinga zingeharibu biashara za watu za mafuta
Maji sio mengi kama unavyowaza.

Unayoyaona ni gharama kuyageuza kuwa salama kwa matumizi ya binadamu.
 
Back
Top Bottom