Teknolojia ya Digitali ya Startimes na Ting: Kero za watumiaji

Hakuna cha startimes wala ting wote wezi tumeibiwa walala hoi! Mm ninazo zote 2 lakini hazina msaada. Star times zilikuwa zikichachachulika wakini naoza kila tkiongeza ujuzi nao wanashtuka. Nimechoka nazo naziuza zote niangalie namna nyigine
 
ikiwa TCRA ilitangaza kuoneshwa local TV stations bure,kwangu mie tofaut kwani tangu jana channels zote eti "not subscribed",wat does this shit mean? STV Guide ndo inaonesha nayo ni matangazo ya TCRA tu.pumbavu xana.
 
Hii nchi iko kama mgonjwa wa kufa. Ikipatikana damu mishipa inakimbia. Mishipa ikirudi, sindano (cannular) zinatoweka!
 
Mie hakuna local hata moja, zimebaki chache.
Nimenunua juzi tu baada ya kusubiri zingine bila mafanikio
 
Ving'amuzi vyao vimeongezewa Giza sipati picha Mpoki huwa inakuwaje ukitizama Ze commedy through Star Times nadhani huwa haonekani zaidi ya macho tu bora warejeshe Analogia ina picha na mwonekano mzuri
 
ki ukweli nilifikilia ni changu tu kumbe hata nyie mmeliona ilo wajilekebishe mbona walianza kwa mbwembwe sana.
 
Wakati nchi yetu, hususani Jiji letu la Dar-es-salaam lilipoondoka kwenye mfumo wa Analogia na kuingia mfumo wa dijitali, Tume ya mawasiliano nchini TCRA, ilituhakikishia wote tulio na TV kuwa ingawa nchi yetu inalazimika kuingia kwenye mfumo wa dijitali, ambapo kila mwenye TV atalazimika kuwa na king'amuzi, tukahakikishiwa kuwa zipo channel za hapa kwetu nchini, zipatazo 5 hivi zitakuwa zinaonekana bure, miongoni mwa channel hizo ni TBC1, StarTV, ITV na Channel ten, zitakuwa zinaonekana bure kabisa, hata kama hujalipia ada ya kila mwezi kwenye king'amuzi chako. Cha ajabu kabisa leo asubuhi wakati nawasha TV yangu, nilipatwa na mshangao mkubwa baada ya kuona hata zile channel ambazo nilikuwa naziona bure, zikawa zinasoma kwenye screen yangu NO ACCESS, NOT SUBSCRIBED!! Kwa maana hiyo hizo channel zote hazionekani tena!! Badala yake kuna channel moja tu ya kampuni ya Startimes, ambayo ndiyo inayoenekana bure, ambayo inaitwa STV Guide, ambayo ni channel maalum kwa ajili ya matangazo yao kampuni ya Startimes! Sijui wadau wenzangu mmeligundua hilo? Sasa ninalowauliza hawa jamaa wa Startimes pamoja na TCRA kwa nini wametufanyia utapeli wa kutuingiza kwenye mfumo wa dijitali na kutuhakikishia kuwa hata sisi walala hoi tusio na pesa za kuweza kulipia channel za pesa, tutaendelea kuziona channel za bure, mbona sasa wamekiuka ahadi yao na kututaka tulipie hata zile channel za bure??!! Au hao Startimes na TCRA wanafuata nyayo za mabosi wao CCM, kwa kupenda tu kudanganya na kutoa ahadi hewa kibao, kwa lengo tu la kuwarubuni wapiga kura wao??!! Sisi wateja tunayo haki ya kuwalazimisha hao Startimes watuonyeshe zile channel za bure kama yalivyo makubaliano yetu, kinyume cha hapo sisi wateja wa ving'amuzi vya Startimes, tutawaburuza mahakamani hao matapeli makubwa wa Startimes!!!
 
Back
Top Bottom