Teknolojia ya 5G na Chanzo cha Covid-19: Nadharia Njama (Conspiracy Theory) yenye maswali mengi

Mchezaji

Member
Oct 5, 2018
42
125
Mchezaji hii theory yako inaitwaje na iko kwenye field gani ya science? Nijulishe maana inavutia kusoma.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndugu Mchezaji haya ni maono, ufunuo au ni science?

Sent using Jamii Forums mobile app
uliza wataalamu wa biology na tiba ama google how normal human cells become cancer cells.

Nakumbuka ilisemekana kwa TV uko tiba ya ukimwi iliwai tengenezwa, ikakabiliwa na mathara yakua ilikua inaamusha cancer cells, sababu dawa hio ilikua inaingizwa mwilini nakushutuliwa kwa stima ili iweze kufika ndani ya mifupa.
Watu walikua wanapona ukimwi na kisha kuanza kugonjeka mbaya na cancer. ikasimamishwa na wakashauri wagonjwa kurudi kwa ARVs.
 
mose

Senior Member
Jun 5, 2009
194
250
Seen mr Mathew T Mndeme...

Your translation and articulation of 5G in Kiswahili was very good and perhaps your choice of '3G - Covid19 debunking stance' brought about an interesting entry for pondering and discussions -- in your perspective.

However, times like this we need to make the society think even beyond the MSM and possible 'Problem/Reactions solutions' that may seem to be rather odd -- as sorted out by the establishment -- in international and local scene.

You, in a person, admit that there is so much going on in the world--this could have served you with better premises to share and explore 5G and Viral subjects separately and avoid that nonsensical damage control narrative covering '2 in 1' prospects in odd combination -- probably trying to vindicate 5G and 'staged' viral epidemic in a clever way...

You are a good language translator and proficient writer of matters of choice; you can still do better without picking up contentious subjects and provocative issues for discussion and enlightening discourses.

Thank you, in way, for you have made ' silent observers' such like me -- to enter in this dialogue and offer my 2 cents...
 
Mathew Togolani Mndeme

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
200
1,000

Thank you brother mose for your contribution.

I wrote this topic knowing its contentious - and possibly contiguous- nature. These are those kinds of issues many of us would avoid discussing in public fora despite knowing many are misled for lack of relevant knowledge, exposure, critical thinking or relevant sources for consultation. Provocative as it is, I thought, it worth a public debate.

It is true that one could have chosen to write on Covid-19 on its own or G5 for the public good. But doing that at a time when the ongoing conversation assumes the two are interrelated with a causality relationship, I'm worried, would have been of no interest to many. Despite the contentions, I want to believe, some (is not many) have found it useful/ helpful seeing it discussed.

Mind you, it was very challenging to me discussing this conspiracy in public, particularly because it touches my own faith and it has carried many among my fellow believers.

MM Togolani
 
Consider all this could be just a set up -- media diversion...

Where are the real 'chips-take?Now, lets see where all this is gonna take us into...

Hmmm
 
Mathew Togolani Mndeme

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
200
1,000
uliza wataalamu wa biology na tiba ama google how normal human cells become cancer cells.

Nakumbuka ilisemekana kwa TV uko tiba ya ukimwi iliwai tengenezwa, ikakabiliwa na mathara yakua ilikua inaamusha cancer cells, sababu dawa hio ilikua inaingizwa mwilini nakushutuliwa kwa stima ili iweze kufika ndani ya mifupa.
Watu walikua wanapona ukimwi na kisha kuanza kugonjeka mbaya na cancer. ikasimamishwa na wakashauri wagonjwa kurudi kwa ARVs.

Ndugu Mchezaji mimi sikutaka kusikiliza wataalamu wengine au kugoogle au Tv "Sliema nini". Nilitaka wewe uelezee kwa ufasaha na mpangilio hicho unachokijua na kuona ni sahihi. Just make an assumption that I (and others) do not know the truth/reality/facts, but you know it all/well. Now, do us a favour by putting the facts down and support them with whatever you think is revelant from Google and/or "wataalamu".

Please educate us.

MM Togolani
 
Mathew Togolani Mndeme

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
200
1,000
Asante kwa ufafanuzi wa kisayansi kuhusu 5G ikihusianishwa na Covd-19. Lakini nikupe angalizo kuwa yapo mambo ya kisayansi yenye azma nzuri sana kwa maendeleo ya Dunia lakin pia nyuma yake yakibeba sura nyingine za hatari ambayo mwenye kuyajua ni Mungu. Kwa Dunia ya sasa n maendeleo lakini kwa ajenda ya sirini ni kwa maangamizi ya rohoni . Vita vyetu wakristo kiimani sio vya damu na nyama Bali ktk ulimwengu wa roho. Mungu anayejua yote huyafunua haya kupitia watumishi wa kweli wa Mungu. Angalizo sio kila asemaye yeye n nabii basi n mtumishi wa Mungu hapana. Biblia inatuonya na kutuhabarisha kuwa sisi tunaoiamin kuwa hatuko gizani kiasi mambo haya yatupate kama mwizi hivyo Mungu huyafunua mapema yaliyoko nyuma ya pazia. Asomaye na afaham habar za nabii Elisha na mfalme aliyekua akipanga njama kulivamia taifa la Israel vile Mungu alivyoyaweka wazi hata wakabak wanashangaa. Ufu.13 16-17 INA mwangaza wa Dunia inakoelekea. Hii no hiari ya kila mtu kuamini kile Mungu anamjalia kukifaham tunapoelekea kutimizwa kwa unabii mwingi ktk Biblia. Maranatha

Ndugu Quick win nakubaliana kabisa na angalizo lako. Ila nina maswali machache.

Moja, hivi hao wataalamu wa nadharia njama na "watumishi" waliofunuliwa kuhusu 5G kuwa chanzo cha Covid-19 wanawasaidia nini watu kwa hofu wanazowajengea? Wakishayasema hayo wanayosema, suluhisho ni kitu gani?

Pili, hivi ni sahihi kwa mtu kutumia uongo, uzushi na mambo ya kupika katika kujenga hoja za kuelezea anachokiita ni ukweli? Uongo na uzushi unawezaje kutumika kuelezea kinachoitwa ukweli uliojificha?

Tatu, hivi wakati hawa wengine wanatumia sayansi yenye adhma nzuri ya maendeleo kutulaghai au kueneza njama zao, "sisi wengine" tunafanyaje au tunatoa mbadala gani? Tunasubiri gunduzi zao halafu tuanze kulalamikia njama au nasi tunatoa mbadala?

Nne, ni wangapi kati ya "sisi tunaofanyiwa njama" hatutatumia teknolojia ya 5G itakapoenea (iwapo bado hatujaanza kutumia)?

Tano, aliyeaminisha watu kwamba hizo njama zinazosemwaa dhidi ya 5G haziwezi kutekeleza kwa 4G ni nani na kwa nini?

MM Togolani
 
Quick win

Member
Jun 3, 2017
73

Moja, kuwajengea watu hofu hakusaidii Bali kinachofanyika no kuwajulisha watu hivyo suluhisho no kuwa yajayo yamekaribia hivyo wanatakiwa kujiandaa au kukesha rohoni maana Yesu yu karibu kurudi kunyakua kabisa ikiwa unaamini hill, hz n moja ya dalili za kuja kwake. Lengo kuu la Dunia inapolekea sasa n New World. Order, utawala mmoja, Dini moja nk
Mbili, sio sahihi kutumia uongo au uzushi kuusaidia ukweli, lkn kumbuka biblia yasema iko njia ionekanayo machoni pa mtu kuwa ni njema lkin kumbe ni njia ya mauti. Ni kweli sayansi inasema ukweli ktk ugunduzi wake lakin Biblia ilikua na majibu hayo yaliyotabiriwa na manabii wa zaman sana kabla ya ugunduzi kuwa maarifa yataongezeka na nk, ktk maarifa hayo wasemapo in amani na salama ndipo uharibifu uwajiapo.
Tatu, sayansi INA adhma nzuri ya maendeleo na sio kila ugunduzi n mbaya hapana Bali kama ilivyo pesa in nzuri sana kwa matumizi mazuri lkn ina maangamizi makubwa kwa matumizi mabaya maana shina la mabaya yote no kupenda pesa kuliko Mumgu ndio chanzo cha maovu mengi. Kwa kuwa nyuma ya siri ya yajayo ni hakuna kuuza wala kununua bila ruksa ya Huyo mtawala ajaye then technolojia ya kasi yenye weledi mkubwa lazima iwezeshwe kufanikisha azma hiyo, hivyo sio ajabu jambo hili likihusihwa na 5G ikiwa mfumo utaliwezesha jambo hill maana lazima litafanyika.
Nne, Kwa kuwa tupo Duniani kwa wakati huu hakuna njia ambapo twaweza kukwepa kuutumia kabla madhara lengwa kufika, lkn Biblia inalo jibu ndio maana ya Unyakuo Rapture itokee maana siku hizo zisingalifupizwa hakuna ambaye angeweza kutoroka kutokuingizwa ktk mfumo,
Tano, je 4G kwa nn haikiweza kutumika, wewe mwenyewe unalo jibu kuwa ndio maana umekuja teknolojia ya hii mpya maana kwa yaliyokusudiwa huo uliopo hauwezi na ikiwa huu utaonekana unafel sio ajabu kuletwa mwingine zaidi lkn azma lazma itimizwe ufu 13 inavyoelekeza. We niambie kwa mawazo yako ili haya yafanye kazi ktka ufunuo 13 n mfumo gani utakaowalazimisha matajiri kwa maskini wrote kuingizwa na kumsujidia mnyama!? Unless wewe kama huamin hayo ktk ufu basi itakua una uelewa tofauti na kinacholekezwa hapo.
Kifupi, Biblia INA majibu yote kabla ya hata wanasayansi kugundua hayo. Ayubu aliweza kuelezea kuwa dunia no mduara na imetundikwa penye utupu lkn wanasayansi imewachukua muda gani kuufam ukweli huo! Asomaye na afahamu tumeonywa. Asante
 
Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
14,476
2,000
Hiyo Dini moja katika NWO itaongozwa kutokea Vatican, Mecca, Moscow, New Delhi au Beijing?

Unamaanisha nini unaposema 4G haikweza kutumika?

Amri kuu ni Upendo

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
738
500
a
MUHTASARI
Mlipuko wa Covid-19 unasambaa ukiambatana na taarifa nyingi zisizo sahihi au za kupotosha. Taarifa hizi zinatengenezwa, ama kwa watu kukosa uelewa sahihi wa jambo wanalolizungumzia au kwa makusudi, kama “Nadharia Njama” (Conspiracy Theory). Mojawapo ni Nadharia Njama inayohusianisha mlipuko wa Covid-19 na tekenolojia mpya ya mawasiliano ya 5G. Nadharia hii inaenezwa na kuaminiwa kwa kasi sana hasa na baadhi ya makundi ya kiimani. Hii imetokana na baadhi ya watumishi kadhaa duniani “wenye majina” kuibeba na kuifanya sehemu ya mahubiri yao kipindi hiki cha taharuki. Kwenye makala hii, ninafafanua teknolojia ya 5G kwa kifupi, madhara yake, na kujaribu kuonesha mapungufu ya nadharia njama kuhusu uhusiano wa 5G na Covid-19. Lengo kuu ni kutoa mwanga kwenye jamii yetu kuhusu kinachosambazwa kupitia nadharia njama ya 5G na kuibua mjadala utakaotusaidia kuujua ukweli wa jambo hili tunapopambana na Covid-19. Kwa undani zaidi, soma makala nzima.

View attachment 1412217
Utangulizi.
Katika mapambano dhidi ya mlipuko wa Covid-19 kwenye nchi yetu na nyingi za Afrika, kuna eneo moja halijatazamwa kwa mapana yake. Eneho hilo ni ugonjwa huu kuhusianishwa na nadharia njama kadhaa na kupewa tafsiri za kiimani kuliko za kisayansi. Kwa kufanya hivyo, kuna hatari kwa baadhi ya watu kupuuzia mlipuko huu na hivyo kuhatarisha maambukizi kua makubwa. Pili, nadharia njama zinaongeza taharuki ya mlipuko na kuwapa watu madhara ya kisaikolojia kujiona wamezungukwa na hatari muda wote kutoka kwa watu wasiowajua. Ukifuatilia kwenye internet na vyombo vya habari vya kimataifa, utaona kuna kundi kubwa la watu hawaamini kama Covid-19 ni ugonjwa unaosababishwa na virusi ambao ni viumbe wa kawaida tulionao kwenye dunia hii. Kinyume chake wanaamini kuna njama, ama za kibaguzi, kibishara, au za kiimani zilizopelekea watu fulani wasiotajwa kutengeneza au kusababisha kutokea kwa ugonjwa wa Covid-19. Moja ya nadharia hizo ni ile inayoaminisha kwamba Covid-19 inasababishwa na teknolojia mpya ya mawasiliano ya 5G.

Je,5G ni kitu gani?
Teknolojia ya mawasiliano ya simu imekuwa ikipanuka na kuendelea siku hadi siku. Teknolojia ya mawasiliano ndio iliyokua kwa kasi zaidi katika historia ya kizazi chetu. Pamoja na mambo mengine, ukuaji wa teknolojia ya mawasiliano unapimwa kwa spidi/kasi ya kusafirisha data kati ya pande mbili zinazowasiliana. Kwa miaka mingi, spidi ya data imekuwa ikiboreshwa na kuongezeka kwa kuboresha miundombinu ya mawasiliano (hardware na software). Hivyo, tangu mwaka 1940, tumetoka kwenye teknolojia inayoitwa 0G (herufi “G” ikimaanisha Generation au kizazi) kwenda kwenye teknolojia inayoitwa 4G (4 generation au kizazi cha 4) tunayotumia sasa.

Kwa sasa, wavumbuzi wameibuka na teknolojia ya 5G ambayo ina spidi kubwa zaidi inayoweza kusafirisha zaidi ya 1 Gbit za data kwa sekunde. Kwa spidi hii kali, tunaweza kufanya kazi nzito zaidi ambazo teknolojia zilizopita haziwezi. Kwa mfano, teknolojia hii inaweza kutumika kwenye magari yanayojiendesha yenyewe (self-driving/autonomous cars); uwezo wa kuunganisha vitu mbalimbali katika mtandao kwa urahisi (Internet of Things); kuwa na miji yenye huduma za kijamii zilizojengwa na kuboreshwa kwa teknolojia ya mawasiliano (smart cities); kuongoza vyombo vya usafiri; vifaa vya burudani; nk. Teknolojia ya 5G inamwingiza binadamu kwenye aina mpya kabisa ya kuishi, na maisha yanatazamiwa kuboreshwa kwa sehemu kubwa. Lakini swali kubwa la kujiuliza hapa ni nini hasa kinatusukuma tunahamia 5G na tutapata faida au athari gani?

Ili kujua kwa nini dunia inaongelea 5G ni lazima uitazame kama kijiji kinachoendelea kwa kasi kubwa na hivyo kupelekea mabadiliko ya mahitaji mengi. Mathalani, kiwango cha data/taarifa kinachozalishwa katika dunia ni kikubwa mno. Ukichukulia mtandao wa Google pekee tuliouzoea, kila siku unazalisha takribani 20 petabytes (10PT) za data (Petabyte 1 ni sawa na Gigabyte (GB) milioni 1). Pia, sekta ya tamthilia (movie) inahama kwa kazi kutoka kutegemea video zinazouzwa kwa njia ya DVD au kaseti kuelekea kutazama tamthilia online kupitia mitandano kama Youtube na Netflix. Pia, utazamaji wa television unahamia kwenye Smart TV ambazo zinakupa uwezo wa kutazama television huku ukiwa unapata huduma nyingi kwa mtandao mithili ya matumizi ya kompyuta. Mahitaji haya ndiyo yalifanya wavumbuzi waanze kufikiria namna ya kuongeza uwezo wa kusafirisha data na kuibuka na 5G. Makampuni ya mawasiliano yanakimbilia kuwekeza katika teknolojia ya 5G kwa sababu ya faida nyingi ambazo wataje wao watapata. hata hivyo kuna changamoto kubwa mbili za 5G kimuondombinu.

 1. Teknolojia ya 5G inahitaji uwekezaji mkubwa wa miundombinu mipya ya mawasiliano kwa sababu inalazimisha kubadilisha ile iliyoko kwa sehemu kubwa. Hadi sasa kuna takribani nchi 35 (nyingi zikiwa tajiri) ambazo tayari zina miundombinu ya 5G na bado inajengwa. Ufungaji wa miundombinu hii kwa nchi nyingi umeanza mwaka 2019.

  Nchi zinazoongoza kuwa na miundombinu ya 5G kwenye miji mingi ni South Korea, China, na Marekani. Kwa miaka kama 2 iliyopita, utakua umesikia siasa za 5G kati ya mataifa makubwa hasa Marekani, Uingereza na China. Hii imetokana na ukweli kwamba kampuni ya Huawei ya wachina imekua mbele hatua kadhaa kiteknolojia na kuzifanya nchi nyingi zikiwemo za Magharibi kutumia teknolojia zake ikiwemo kuweka miundombinu ya 5G. Hii imewapa taharuki maadui zao kiuchumi hasa Marekani kwa hoja kwamba mitambo yao sio salama kwa kuwa inaratibiwa au kudukuliwa na serikali ya China (hili tuliachie hapa maana ni mjadala mwingine).

 2. Nyingine ni ukweli kwamba wateja watalazimika kuwa na vifaa vilivyotengenezwa kutumia teknoljia ya 5G, na hivyo kuingia gharama ya ziada/kubwa.
Pamoja na changamoto hizi na nyingine, bado 5G inatoa matumaini mapya ya maendeleo yatakayomwezesha binadamu kufanya shughuli nyingi ngumu kwa muda mfupi. 5G inafanikishwa mambo mawili makubwa. Moja ni kiwango cha data kinachoweza kusafirishwa, na mbili ni spidi/kasi ya data kusafiri kati ya kifaa kimoja na kingine.

Je, 5G ina madhara gani kiafya?
Nadharia njama ya 5G imejikita katika kile kinachoitwa madhara makubwa ya 5G kwa afya zetu. Kumesambaa habari nyingi duniani zilizoanzishwa na watu wachache na zimeshika kazi kama moto wa mabua kiasi kwamba zimeanza kuaminika kama ukweli. Hii imepelekea siku ya jana mtandao wa Youtube kuamu kuanza kufuta video zote kwenye mfumo wao zinazoongela nadharia njama ya G5 na uhusiano wake na Covid-19 (tazama hapa). Katika nchi za kiafrika ambapo kwa sehemu kubwa tumeturuhu watu wengine wafikirie na hata kuamua kwa niaba yetu, nadharia hii imeingizwa kwenye viunga vya kiimani na imeshakua ukweli kwa watu wengi maana huwa tunaogopa kuhoji mambo ya kiimani au wanachokisema watumishi.

Nimesikiliza na kusoma maelezo ya waanzilishi na wainjilisti wa nadharia njama ya 5G ili kuelewa msingi wa taharuki wanayoijenga. Mengi wanayoongea ni uongo, uzushi, ya kuungaunga, na hayana usahihi wowote kisayansi wala kiimani. Nadharia hii imeanzishwa na wataalamu wa nadharia njama (conspirancy theorists - wawili wakiwa ni waingereza) na kudakwa na baadhi ya watumishi “wenye majina” kama hoja ya mahubiri yao. Baadhi ya watumishi (hasa wa kikristo) hupenda kujionesha kua wao wana majibu au maelezo ya kila jambo duniani. Hivyo wamechukua hoja ya 5G na kuitumia kama ilivyo au kwa kuitohoa kujengea hoja za chanzo na malengo ya Covid-19. Nitaje kwa kifupi baadhi ya hoja zilizoko kwenye nadharia njama ya 5G.

 1. Taswira inajengwa kwamba kuna mkakati wa watu ambao wanaleta teknolojia ya 5G kwa lengo la kuitawala dunia na hasa kutufanya sisi wanadamu wote kuunganishwa kwenye mtandao mmoja ili kuweza kutaribiwa. Mkakati huu unapewa majina mengi lakini mojawapo ni mbinu ya kufanikisha kinachoitwa “New World Order (NWO)”. NWO ni nadharia njama inayodai kuna kundi la siri lenye nguvu kuliko mataifa yote litakaloitawala dunia nzima kibabe.
  UDHAIFU: wanaoaminisha nadharia hii hawataji watu hao ni kina nani, wako nchi gani, na iwapo ni wa dunia hii au sayari nyingine. Ukiachilia kutajwa kwa baadhi ya viongozi wakuu wa baadhi ya nchi na dini kubwa, nadharia hii inabaki kuwa yakufirika na imekuwepo kwa muda mrefu.

 2. Hoja inajengwa kwamba vifaa vya teknolojia ya 5G vina mionzi mikali yenye madhara kwenye miili yetu. Katika kupambana nayo, miili yetu inatengeneza virusi wa Corona.
  UDHAIFU: Moja, hakuna ushahidi wa kisayansi wowote juu ya hili. Pili, kama miili yetu inatengeneza virusi wa Corona tunapopigwa na mionzi ya 5G, kwa nini basi tusingekua tunaugua wote kwenye eneo lenye 5G? Tatu, kwa nini watu wanaoathirika wanapona?

 3. Wakati huohuo wanadai Covid-19 inasambazwa kwa watu kupitia vipimo tunavyofanyiwa kujua iwapo tuna maambukizi. Lengo kubwa la kuingiziwa virusi hivi ni ili dunia nzima iwe na maambukizi kisha kupitishwe taratibu/sheria inayomtaka kila mtu lazima apewe chanjo ya kumkinga na Covid-19. Kupitia chanjo hiyo tutaingiziwa “chip” ndogo ya mawasiliano kwenye miili yetu (mithili ya line ya simu yako) itakayowezesha watu hao wasiojulikana kutufuatilia kama vile mitambo ya kompyuta. Pia, mtu hataweza kupata visa kuingia nchi nyingine iwapo hajathibitisha kua na una kinga ya Covid-19.
  UDHAIFU: Moja, tuna ushahidi kutoka nchi nyingi watu kuambukizwa na kueonesha dalili (wengine hadi kufariki) kabla ya kupimwa. Pili, ili uweze kupachika chip ya kielekroniki ifanye kazi na kuweza kusafirisha data na mfumo wa mwili, ni lazima ipachikwe mahili maalumu na kuunganishwa na mfumo wa mawasiliano wa mwili. Wanaohubiri nadharia hii hawatuelezi ni kwa jinsi gani chanjo tutakayopewa (ama vidonge au kimiminika) itaingiza chip mwilini na ikafanye kazi.

 4. Wakristo wanatahadharishwa kwamba 5G ni mpango wa shetani na Covid-19 ni vita dhidi yao. Wengine wanakwenda mbali zaidi kudai Covid-19 imetengenezwa kwa lengo la kuangamiza waafrika ila waliotengeneza wamekosea ikawaathiri wao wenyewe.
  UDHAIFU: Hoja hii ni dhaifu kama zingine maana ni ya kufikirika.

 5. Katika kujenga hoja zao, baadhi ya manabii wa njama hii wanasema virusi sio viumbe halisia bali wanatengenezwa kwa malengo mabaya.
  UDHAIFU: Huu ni uongo ulioopitiliza kwani wanasayansi wa viorolojia wanatuambia kuna aina takribani 5,000 ya virusi wa asili duniani. Sifa kubwa ya virusi ni kutokua na uwezo wa kuishi wenyewe bila kuwa ndani au juu ya kiumbe kingine. Hivyo wanaweza kuishi kwa wanadamu, wanyama, ndege, samaki, mimea na hata viumbe vidogo kama bakteria. Hata hivyo wataalamu wa bayoteknolojia wanaweza kutengeneza virusi kwa njia za kimaabara kwa malengo mbalimbali.

 6. Wanajenga hoja kwamba kirusi cha Corona ni kipya na hajawahi kuwepo. Moja ya filamu ya kijapani iliyotengenezwa 2018 ina kipengele wanachotaja visuri wa Corona hivyo kipengele hiki kinatumika kuthibitisha kwamba Corona ni mkakati wa silaha za kibalojia.
  UDHAIFU: Hoja hii inadhirisha jinsi upotoshaji huu usivyo na mashiko. Virusi wanaosababisha Covid-19 (yaani SARS-CoV-2), ni kafamilia kamoja tu kati ya familia karibu 60 za ukoo wa Coronavirus. Wana dada yao anaitwa SARS-CoV-1 aliyesababisha mlipuko wa SARS kule China mwaka 2002/2004 lakini ukadhibitiwa. Pia wana binamu naitwa MERS-Cov aliyelipuka kule uarabuni 2012 na kudhibitiwa pia.
Uhalisia uko wapi?
Kuna uwezekano mkubwa wa teknolojia ya mawasiliano kuwa na madhara kiafya kama zilivyo teknolojia nyingi tunazotumia kila siku (magari, simu za mikononi, kompyuta, nk). Kwenye teknolojia ya mawasiliano, madhara yanahusishwa moja kwa moja na mionzi inayotumika kusafirisha data (kwa mfano simu zetu kuwasiliana na minara ya mawasiliano au na kifaa cha kupata mtandao wa intenet kwa njia ya upepo (WiFi)).

Kwa mfano, tafiti kadhaa zilizofanyika nchi kama India, Australia, Marekani, Ufaransa, nk, zimeonesha uwezekano wa madhara yatokanayo na matumizi ya simu za mikononi (sio za 5G). Ziko tafiti zimeonesha mionzi ya simu inaweza kusabanisha kansa, kuharibu mbegu za kiume, nk. Watafiti wanatoa tahadhari na kuwashauri watu kupuunguza mawasiliano ya simu za mikononi na kuzitaka kampuni zinazotengeneza simu kuwa wawazi kwa kuweka tahadhari wazi juu ya madhara mtu anayoweza kuyapata kwa kutumia simu. Wanashauri tuwazuie watoto kutumia simu na vifaa vingine vyenye WiFi ili kuzuia madhara ya mionzi ambayo imeonekana inaweza kusababisha kansa ya ubongo.

Kuna mjadala na mvutano mkubwa kati ya watafiti na watu walio kwenye sekta ya mawasiliano kuhusu ukweli wa madhara vifaa vya mawasiliano. Wanaopinga uwepo wa madhara wanasema hakuna ushahidi wa kutosha kuthibitisha yale yanayodaiwa [Hii ni mada ndefu hivyo kwa sasa niiachie hapa nirudi kwenye 5G].

Hivyo basi, kama simu ambazo tayari tunatumia zenye teknolojia ya 2G, 3G au 4G zimethibitika kwamba zinaweza kua na madhara yatokanayo na mionzi, ni wazi 5G inaweza kuwa na ina hiyohiyo ya madhara. Yanaweza yakawa ama nafuu zaidi kutokana na maendeleo ya teknolojia au makali zaidi kwa sababu hiyohiyo. Manabii wa nadharia njama ya 5G wanajenga hoja kwamba mionzi itokayo kwenye vifaa vya 5G ina nguvu isiyoweza kustahimilika na miili yetu.

Hata hivyo, lazima tutambue kwamba, wagunduzi wa mawasiliano nao ni binadamu na wanapotengeneza teknolojia mpya, wanazifanyia tafiti za kina kupima madhara yake kabla ya kuzipitisha kutumika. Pia, kila nchi (hasa zilizoendelea) zina taasisi za viwango, uratibu na udhibiti kwa lengo la kuthibitisha ubora na usalama wa mitambo ya mawasiliano kabla ya kutumika katika jamii (sisi tuna TCRA). Hakuna taifa/serikali hata moja duniani, iko tayari kufunga mitambo ya mawasiliano ambayo ina madhara kwa watu wake huku wakijua haitachagua nani wa kumdhuru.

Fursa inayotumiwa na wanaohubiri nadharia njama ya 5G
Baadhi ya manabii wa nadharia njama ya 5G ni watu wenye elimu kubwa na ufahamu mpana wa mambo. Wataalamu wengi wa nadharia njama wana akili nyingi na ni wasomi wazuri. Hivyo wanatumia nafasi hiyo kama njia ya kuonesha wanachokiongea kina ukweli. Kunahitajika uwezo mkubwa na uelewa wa mambo kung'amua yaliyo nyuma ya nadharia zao. Hata hivyo, miongoni mwao kuna wengi hawana kabisa uelewa wa teknolojia za mawasiliano na hawana uwezo wa kukuambia 5G ni kitu gani au hizo hatari zinatokeaje katika uhalisia. Ukiwasikiliza vema, wanatumia baadhi ya nadharia za mifumo ya teknolojia ya mawasiliano kwa kuungaunga kama namna ya kuonesha uhatari wa 5G. Wanataja maneno kama artificial intelligence (AI), Internet of Things (IoT) au Machine Leaning (ML) kujazia hoja zao bila kuelewa zinalenga nini hasa. Kwa mtu asiye na eleimu ya mambo haya (na hawa ni wengi kwenye jamii) akitajiwa mambo haya anapata picha inayotisha sana. Kama vile haitoshi, watu hawa hawana uelewa wa kutosha kuhusu epidemilojia ya magonjwa ya mlipuko. Ila, wanafanikiwa kwa kiasi kikubwa kupotosha kwa kua wanajua au kuamini kwamba wanaowasikiliza hawana uelewa wa mambo au elemu yao ni ndogo kuweza kung’amua ukweli au kutafuta usahihi wa wanachokisema.

Hitimisho na Ushauri
Nadharia njama ya 5G na nyingine zina hatarisha watu wengi kuambukizwa na Covid-19 kwani wanaozisambaza wanatoa maelezo yanayokanganya na kuwafanya wengi wasifuate maelekezo ya kisayansi ya ugonjwa huu na namna ya kukabiliana nao. Ndio mana utaelewa ni kwa nini juzi kule Abijan Ivory Coast wananchi wameandama na kwenda kuvunja jengo maalum linaloandaliwa kwa ajili ya kupimia wagonjwa wa Covid-19. Pia utaelewa ni kwa nini, baadhi ya “watumishi” wanahamasisha waumini wao waendelee kufanya ibada za pamoja kwa wingi zaidi wakiamini Covid-19 ni mbinu za mpinga Kristo na wanatakiwa kuamini haitawapata wao. Waliosambaza Covid-19 kwa wingi kule Korea ya Kusini walikua wakristo (walokole) waliopuuzia athari za ugonjwa huu. Waliambukizana kwa wingi na wakafanya karibu mji mzima kulemewa na maambukizi.

Kama nilivyosema kwenye moja ya makala zangu kuhusu janga la Covid-19 na kuziweka
hapa Jamii Forum, mlipuko huu umedhihirisha ni kwa kiasi gani sisi waafrika tulio wengi sio jamii inayoongozwa na elimu, maarifa, sayansi, na teknolojia. Imetuonesha namna tunavyofanya maamuzi yetu bila kutumia taarifa sahihi na tulivyo warahisi kuamini taarifa za uongo, za uzushi, na kutotaka kujishughulisha kutafuta ukweli na maarifa. Pia, imetuonesha namna mfumo wetu wa elimu usivyotuandaa na kutuwezeha kutumia uwezo wetu wa kufikiri, kufanya tafakuri tunduizi, na kuchambua mambo kwa lengo la kutafuta maarifa, ukweli au usahihi wa kile tunachosikia.

Kama vile haitoshi, mlipuko huu umetuonesha namna baadhi ya "watumishi wa dini zetu" wanavyotumia kila fursa wanayoipata kutuweka mbali na ukweli kwa makusudi na kwa manufaa yao binafsi. Hawataki tutumie akili zetu na elimu kutafuta majawabu ya maswali magumu yanatotukabili au suluhisho la changamoto tunazokutana nazo. Kila mara wanataka tutumie fikra za kiimani kama "shortcut" ambayo haitufikishi wanapotuahidi. Ifike mahali, wapendwa hawa wakubali kwamba wao sio miungu na hawana ufunuo wa kila jambo. Wao ni watumishi tu hivyo hawawezi kuwa na maelezo au majawabu ya kila swali au utata unaojitokeza kwenye jamii. Ni sahihi kabisa wakisema hawana maelezo au hawajui au bado wanamwomba wanayemtumikia kupata majawabu. Kukiri hivi hakuwapunguzii kitu katika nafasi yao ya utumishi. Pia kwa mambo ya kitaalamu/kisayansi, ni vema wakatafuta wabobezi wa eneo husika wakawapa mwanga wa kutosha wa kisayansi kabla ya kuyaongelea kwa umma katika muktadha wa kiimani. Hii ina msaada mkuwa sana na inawapa heshima hata nje ya waumini wao. Wana fursa kubwa ya kupata maelezo ya kitaalamu tena bure kutoka kwa makundi yao na hata wasio wa makundi yao.

Moja ya mambo yanayotuchelewesha waafrika kuendelea kwa kasi kama mataifa mengine tuyatazamayo kama vielelezo, ni kuhoji kila kitu kigeni kwa mtizamo wa kukiogopa au kukishuku huku tukiwa hatuna maelezo sahihi wala uthibitisho wa tunachoamini/kuaminishwa/kuwaaminisha wengine. Mbaya zaidi tunakua hatuna mbadala wa kuwapa tunaowajengea hofu. Unawaaminisha watu kuwa 5G ni hatari au ni shetani huku mfukoni una simu ya 4/5G na hotuba au mahubiri unayotoa unayarusha live kwa Youtube inayotumia teknolojia ya 5G kuweza kustahimili wingi wa watu wanayoitumia. Pia una accounts za mitandao ya kijamii ambayo kwa sehemu kubwa zinategemea teknolojia unayopambana nayo. Sasa tukuamini kwa lipi?

Zingatia
 1. Uchambuzi na maoni niliyoyatoa hapa, hayamaanishi kwamba ninaamini hakuna madhara yanayoweza kusababishwa na teknolojia ya 5G. Pia, hayamaanishi ninapinga watu kuhojia, kutafiti, au kuweka mashaka kuhusu usalama wa teknolojia hii. Hapana. Hoja yangu nya msingi ni kutofautina na upotofu unaonezwa na nadharia njama ya kuhusianisha Covid-19 na 5G. Tuhoji na kutafiti madhara ya 5G na mambo mengine (kama ni lazima) kwa kutumia ukweli na ushahidi wa kisayansi badala ya dhana za kufikirika na ndoto za abunuwasi.

  Sehemu kubwa ya Afrika tuko kwenye mkwamo kama jamii na mapokeo tuliyoletewa na waliotutawala (hasa imani) yanatuathiri kifikra na kimitazamo kuliko waliozinzisha. Hivyo tukimaliza hili la Covid-19, tuanze kuweka mikakati ya muda mrefu ya kujikwamua tulipokwama ili kurahisha maendeleo ya watu na vitu. Pamoja na bidii na imani zetu, tunahitaji elimu na maarifa sahihi ili tuweze kupiga hatua na kuleta maendeleo endelevu.

 2. Uchambuzi huu haujalenga kuwashambulia wakristo au "watumishi" kwani nami ni mmoja wao. Nimetaja ukristo (tena kwa tahadhari kubwa) maana ndio kundi nililoko na ninashuhudia jinsi baadhi yetu wanavyokazana kupotosha kuhusu Covid-19 na kinaathiri jamii kubwa.

 3. Neno "Nadharia Njama" sio rasmi katika viunga vya lugha ya Kiswahili bali nimelitohoa mimi mwenyewe baada ya kuketi na kamusi za Kiswahili nikiwa natafuta tafsiri/maana ya "Consipiracy Theory". Sifahamu tafsiri rasmi ya dhana hii kwa Kiswahili.

Mathew Togolani Mndeme (mmtogolani@gmail.com)
Mtafiti wa mifumo ya digitali kwenye ufuatiliaji na udhibiti wa magonjwa

 • Shukrani kwa classmate wangu Dr. Baraka Maiseli (Lecturer in Electronic and Telecommunications Engineering, UDSM) kwa ushauri kwenye ufafanuzi wa teknolojia ya 5G
asante mkuu kwa elimu nzuri kabisa kuhusu five G. lakini nina maswali kwako unielimishe pia!
1. Kama nadharia hiyo imetolewa na wakristo kwa wakristo shida iko wapi? maana wakristo wana kitabu chao chenye kuonesha unabii wa kila jambo litakalotokea hapa duniani kabla ya kiama, mfano kuja kwa Anti christ, New world order, chapa ya mnyama 666 na kwa hakika unabii HUO unatimilika mmoja baada ya mmoja kwa wakati wake!!
2. Na je ni kweli wewe hujawahi kuisikia New World Order ikizungumzwa nje ya ukristo? Je unakubali itakuja? kama huikubali sawa, lakini kama unakubaliana na unabii huu wa kibiblia je unadhani utekelezaji wake utaanza lini na utakuaje?
ASANTE!
 
Amri kuu ni Upendo

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
738
500
Makanisa ya manabii na mitume,viongozi wao wasome haya maelezo.
MAELEZO HAYA WATAYASOMA SAWA, LAKINI JE WAKIYALINGANISHA NA MAELEZO YA KIBIBLIA YATA MATCH?
NA JE YAKIKATAANA UNADHANI UTAWASHAURI WAZINGATIE MAELEZO HAYA WATELEKEZE YA BIBLIA!!
MAANA SIKU ZOTE MUNGU MKWELI BINADAMU MWONGO.
 
Mathew Togolani Mndeme

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
200
1,000
Moja, kuwajengea watu hofu hakusaidii Bali kinachofanyika no kuwajulisha watu hivyo suluhisho no kuwa yajayo yamekaribia hivyo wanatakiwa kujiandaa au kukesha rohoni maana Yesu yu karibu kurudi kunyakua kabisa ikiwa unaamini hill, hz n moja ya dalili za kuja kwake. Lengo kuu la Dunia inapolekea sasa n New World. Order, utawala mmoja, Dini moja nk
Mbili, sio sahihi kutumia uongo au uzushi kuusaidia ukweli, lkn kumbuka biblia yasema iko njia ionekanayo machoni pa mtu kuwa ni njema lkin kumbe ni njia ya mauti. Ni kweli sayansi inasema ukweli ktk ugunduzi wake lakin Biblia ilikua na majibu hayo yaliyotabiriwa na manabii wa zaman sana kabla ya ugunduzi kuwa maarifa yataongezeka na nk, ktk maarifa hayo wasemapo in amani na salama ndipo uharibifu uwajiapo.
Tatu, sayansi INA adhma nzuri ya maendeleo na sio kila ugunduzi n mbaya hapana Bali kama ilivyo pesa in nzuri sana kwa matumizi mazuri lkn ina maangamizi makubwa kwa matumizi mabaya maana shina la mabaya yote no kupenda pesa kuliko Mumgu ndio chanzo cha maovu mengi. Kwa kuwa nyuma ya siri ya yajayo ni hakuna kuuza wala kununua bila ruksa ya Huyo mtawala ajaye then technolojia ya kasi yenye weledi mkubwa lazima iwezeshwe kufanikisha azma hiyo, hivyo sio ajabu jambo hili likihusihwa na 5G ikiwa mfumo utaliwezesha jambo hill maana lazima litafanyika.
Nne, Kwa kuwa tupo Duniani kwa wakati huu hakuna njia ambapo twaweza kukwepa kuutumia kabla madhara lengwa kufika, lkn Biblia inalo jibu ndio maana ya Unyakuo Rapture itokee maana siku hizo zisingalifupizwa hakuna ambaye angeweza kutoroka kutokuingizwa ktk mfumo,
Tano, je 4G kwa nn haikiweza kutumika, wewe mwenyewe unalo jibu kuwa ndio maana umekuja teknolojia ya hii mpya maana kwa yaliyokusudiwa huo uliopo hauwezi na ikiwa huu utaonekana unafel sio ajabu kuletwa mwingine zaidi lkn azma lazma itimizwe ufu 13 inavyoelekeza. We niambie kwa mawazo yako ili haya yafanye kazi ktka ufunuo 13 n mfumo gani utakaowalazimisha matajiri kwa maskini wrote kuingizwa na kumsujidia mnyama!? Unless wewe kama huamin hayo ktk ufu basi itakua una uelewa tofauti na kinacholekezwa hapo.
Kifupi, Biblia INA majibu yote kabla ya hata wanasayansi kugundua hayo. Ayubu aliweza kuelezea kuwa dunia no mduara na imetundikwa penye utupu lkn wanasayansi imewachukua muda gani kuufam ukweli huo! Asomaye na afahamu tumeonywa. Asante
Ndugu Quick win namba nikujibu kwa pamoja na Amri kuu ni Upendo,

Naona tatizo moja kubwa kwenye maelezo yenu. Kama vile ambavyo kwenye tafiti tunaongozwa na philosophical assumptions/stance/position, naona maelezo yenu na fikra zenu munaongozwa na nadharia zenye lengo la kujenga hofu na kuunganisha kila consipiracies/uzushi na unabii wa Biblia. Sielewi ni kwa namna gani unakubali kwamba sio sahihi kutumia uongo, uzushi, na maelezo ya kuungaunga kuusaidia ukweli (neno la Mungu) lakini wakati huohuo unataka mambo hayohayo yaunganishwe na kinachosemwa na Biblia. Naelewa Biblia inasema nini kuhusu unabii wa siku za mwisho ila kitu ambacho sitaelewa hadi kesho, ni baadhi ya wakristo wenzangu kutaka kutumia kauli za kutunga na nadharia wanazozichomoa kutoka kwa wazushi wengine huku duniani, ili kujengea watu hofu kuhusu siku za mwisho au mbinu za shetani.

Huu mtizamo wa kwamba neno la Mungu linahitaji kutumia nadharia njama za kizushi zilioanzishwa na hata wasio na imani kwa Mungu mumeutoa kwenye mstari gani?

Labda nimiulizeni maswali machache ya ufahamu:
 1. Hivi mumewahi kupanda ndege mukasafiri angalau masaa 5 au kumi hewani bila kutua? Kama mumewahi, mukiwa kule juu huwa munajipa nafasi ya kufikiria ni kwa jinsi gani mwanadamu aliweza kuibuka na ugunduzi wa ajabu karibu zaidi ya miaka 100 sasa? Mumewahi kufikiria ni kwa jinsi gani tumeweza kurusha midege hewani na kuiratibu tutakavyo?

 2. Hivi kama 1969 (zaidi ya miaka 50 sasa) binadamu waliweza kusafiri zaidi ya kilometa 384,400 kwenda mwezini na wakiwa kule wanawasiliana na duniani (kukiwa bado hakuna hata 1G wala internet)? Kama hili liliwezekana ni nini kinachowaaminisha kwamba 5G ni tishio kiimani na ni mkakati wa siku za mwisho?

 3. Hivi munafahamu kwamba tumetuma chombo (New Horizons interplanetary space probe) angani ambacho kilikua kinasafiri kwa 58,500 km/h kwa miaka 9 mfulilozo (kutoka 2006 hadi 2015) kuifikia sayari ya mwisho kabisa katika mfumo wetu wa jua (our solar system) iliyoko umbali wa takribani 5.1 billion kms? Munafahamu kwamba kwa miaka yote hii chombo hiki kilikua kinaongozwa kutoka duniani kikipitia sayari za mbali moja baada ya nyingine huku kikituma picha duniani? Munafahamu kwamba chombo hiki kiliendelea kuwasialina na dunia hata baada ya kutona nje ya mfumo wetu wa jua?

 4. Hivi munafahamu kwamba kule kwenye sayari na Mars iliyoko takribani kilometa milioni 202.4 tumetuma vyombo vitatu sasa vinavyofanya kazi ya kuitafiti ile sayari huku vikiongozwa kutoka duniani na vikitutumia picha?

  Sasa nimiulizeni tena:
  Hivi cha kushangaa hapa ni kipi kati ya wanadamu kutengeneza na kurusha ndege hewani; kwenda mwezini na kurudi miaka 50 iliyopita; kuongoza chombo hewani kwa miaka 9 kikisaifiri umbaliwa zaidi ya 5B km; kufanya tarifi kwenye Mars kwa kutumia robots zinazoongozwa toka duniani; au ni teknolojia ya 5G ambayo haina cha ajabu zaidi ya kuongeza speed na volume ya mawasiliano ambayo tayari tunayo? Kipi kati ya hivi ni dalili ya siku za mwisho? Kipi kati ya hivi ni kazi ya mpinga kristo katika harakati za kuitawala dunia kwa NWO?

  Tatizo la jumla:
  Tatizo kubwa linalotukumba wakristo wengi ni kukubali ujinga kutumika kama silaha ya kiimani. Tunatumia ujinga wetu wa kutokujua mambo au kukosa uelewa mpana au kukosa exposure, kama silaya ya kila kitu chini ya mwemvuli wa imani. Tumeruhusu baadhi ya "watumishi" watudanganye na kutuchanganya wapendavyo. Chochote wakisemacho nyuma ya "neno la Mungu" au "mistari fulani ya Biblia" tunakimeza kama ndio kweli na kweli pekee bila kujipa muda wa kufikiria na kuchambua wenyewe.

  Baadhi ya watumishi hawa wanaendekeza ujinga kwenye jamii zetu. Badala ya kutusaidia na sisi tujikwamue kwenye ujinga tujikite kwenye speed ya maendeleo ya kisayansi na teknolojia, wanakazana kutuvika ujinga ili wazidi kuongoza fikra zetu watakavyo kwa kigezo cha imani. Wakati huohuo, wao wako kwenye mandege kila mara wanakwenda kwenye nchi zilizoendelea kiteknolojia kufaidi kazi za kisayansi zilizoboresha maisha ya wenzetu. Na wakirudi nyumbani hawaachi kutusimulia (kutoa ushuhuda) habari za ulaya, marekani, China,Japan, Australia na kwingineko wanakokwenda kutanua na kushuhudia maisha yalivyoboreshwa na teknolojia. Wengi wengine waoto wao hawawasomeshi kwenye mazingira yanayoamini 5G ni siku za mwisho bali wamewapeleka kwenye nchi zinazotumia teknolijia hizo ili nao waendane na waketi.

  Naomba nisiongelee hili zaidi ila nimishaurini kujiepusha na watu wanaotumia ujinga kama mtaji wa kuwa juu ya wengine na kufanikisha mipango yao. Hili ndilo lengo kuu la Conspiracy theorists na "baadhi ya watumishi" wanaoungana nao..

  MM Togolani
 
Quick win

Member
Jun 3, 2017
73
125
Tatizo la jumla:
Tatizo kubwa linalotukumba wakristo wengi ni kukubali ujinga kutumika kama silaha ya kiimani. Tunatumia ujinga wetu wa kutokujua mambo au kukosa uelewa mpana au kukosa exposure, kama silaya ya kila kitu chini ya mwemvuli wa imani. Tumeruhusu baadhi ya "watumishi" watudanganye na kutuchanganya wapendavyo. Chochote wakisemacho nyuma ya "neno la Mungu" au "mistari fulani ya Biblia" tunakimeza kama ndio kweli na kweli pekee bila kujipa muda wa kufikiria na kuchambua wenyewe
Nakubaliana nawe kwa jambo la wako watumish naweza sema ni wa shetan kabisa Ila wamejivika ngozi ya kondoo ambao Yesu alikwisha onya watatokea manabii wengi wa uongo , sio wachache Bali wengi. Mtawafahamu kwa matunda yao.
Ninachokikataa ni ule usemi wako wa kushabikia masuala ya kisayansi kama ndoo yana majibu yote hapo sio kweli, kabla ya ugunduzi wa hii sayansi ya ndege he umewahi kujiuliza ni sayansi gani ilitumika Nabii Eliya alipopanda gari la moto? He Henoko naye alivyotwaliwa je? He Joshua aliposimamisha jua kwa Siku moja nzima ili ashinde vita alitumia remote IPI? Je Paulo alipoenda mbingu ya tatu alitumia ndege IPI?,Yesu akapaa na mawingu je wanasayansi wanasemaje hapo? Je Filipo alipobebwa kwenda azoto ? Jaman Biblia INA siri nyingi zinazohitaj Roho wa Mungu kuzijua.. Akili au hekima ya kibinadamu haina majibu kwa mambo ya rohoni (1kor 2;6-hadi mwisho).
Manabii wa uongo wapi kuchuma kwa ajili ya tumbo lao ni dhahiri kwa kujikusanyia Mali, manabii wa kweli wapi kuufunua ukweli wa rohoni ila kuliandaa kabisa kwa unyakuo. Ndg yangu yaonekanaumebobea ktk teknolojia n vema sana, lkn ktk hiyo teknolojia ndio itakayotumika sana kuukamilisha unabii wa cku za mwisho na unahitaji kuujua ufunuo wa Mungu ili kujua mahusiano yaliyomo ktk ulimwengu wa rohoni na kinachoendelea. Otherwise uelewa ulionao utakufaidia kuupata ulimwengu lkn vya rohoni vitabaki kutambulikana rohoni. 'Asomaye na afahamu' tumeonywa. Wakati Dunia imepigishwa magoti inyenyekee kuna jambo linaendelea nyuma ya pazia usilolijua. Ni kweli Dunia imekua kiganjani ili Antichrist afanye atakavyo ingawa hata hiyo Antichrist hatajikubali kama Antichrist Bali kisayansi ataitwa mkombozi wa Dunia iliyoshindwa kupata majibu, lkn wasemapo kuna amani na salama hapo ndipo uharibifu utakapotokea.. Ni kweli Mungu atawalipa mabaya manabii wanaolipotosha kabisa ila kwa kuwa watu hawaitaki kweli basi wataangukia uongo waukubali.
 
Bombabomba

JF-Expert Member
Dec 23, 2017
1,408
2,000
Hongereni wote mliochangia hoja kwa maana ya kujenga. Binafsi mmenisaidia sana. Hu Uzi nimeukopi na kuweka kwenye PC yangu niendelee kurejea. Ubarikiwe M. Togolani M.M Hakika umetusaidia sana tulio wengi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Quick win

Member
Jun 3, 2017
73
125
Someone just shared this somewhere, you can choose to believe or not, but for me this is an issue we have been discussing ! Nyuma ya pazia kinachoendelea, kwa waamin wanaelewa sana!

FOR THOSE ASKING ABOUT 5G.

5G is an improvement over 4G it is 10x faster than 4G. 5G is not the 666 but 5G is part of the medium for introducing the 666. How ? Now look at this.

With a 5G phone!you don't need to move around with your Phone, You just keep it at home. But a MicroChip will be implanted under your skin! With that Micro Chip. you can answer your phone with your body and you can call someone with your body without using phone. The device can read your mind,They know your next action before you do it.

With a 5G and the Implant MicroChip you don't need an International Passport at the air port and you can do any bank transaction any where in the world. And that means you can use it to buy and sale.

(Can you see that BUYING AND SELLING, Rev 13 ) Tomorrow a leader would rise up and say nobody should buy and sale until you have that MicroChip (666) clearly that's what the Bible warned us, 2000 years ago.

They know Christians will not buy the Idea of MicroChip Implant that's why people like Bill Gates a confirmed FREEMASON is saying everybody should take vaccination. They want to secretly introduce the Implant through the vaccination and we Christians say no to their vaccination, because whether the MicroChip is the 666 or not God has warn us in Rev:13 thousands of years before this evil people were born not to put any microchip Implant in our body.

They produce a disease and they are bringing a solution to the disease (Think about that) . We can't stop their plans, because God didn't say we (Christians) can stop them, but we have to warn people, not to fall to their traps.

They suppose to introduce CORONA VIRUS a man made disease since 2012 . 50% of this evil people and people that brought this CORONA VIRUS live in America , the coming of Donald Trump dealt with their plans greatly that's why they had to move to China an ungodly nation to launch it. But God is above them, they are trying to go faster than God. The foolish people thing they are intelligent but unknown to them they can not destroy Earth that they did not create.

The CORONA VIRUS, 5G and the MicroChip is just a rehearsal by this evil people , they can not force it on everybody until Christians are Raptured away for the wedding feast between JESUS CHRIST GLORIFIED and His bride (Church) .

CHRISTIANS do not get panicked and start losing hope on life that JESUS CHRIST is coming now and you say what is the hope in life.

Yes JESUS CHRIST is coming very soon but nobody knows when. Please go ahead with your normal activities.

Go to school, get married , aspire in life but be more wiser. Watch and pray with the consciousness that JESUS can come the next minute. Stop living carelessly anymore.

As we wait for his coming at anytime. Let's Preach the Gospel everywhere in the world and get as many people as possible to Jesus.

JUST DECIDED TO SHARE.
REMAIN RAPTURE CONSCIOUS.
 
mwengeso

JF-Expert Member
Nov 27, 2014
8,498
2,000
MUHTASARI
Mlipuko wa Covid-19 unasambaa ukiambatana na taarifa nyingi zisizo sahihi au za kupotosha. Taarifa hizi zinatengenezwa, ama kwa watu kukosa uelewa sahihi wa jambo wanalolizungumzia au kwa makusudi, kama “Nadharia Njama” (Conspiracy Theory). Mojawapo ni Nadharia Njama inayohusianisha mlipuko wa Covid-19 na tekenolojia mpya ya mawasiliano ya 5G. Nadharia hii inaenezwa na kuaminiwa kwa kasi sana hasa na baadhi ya makundi ya kiimani. Hii imetokana na baadhi ya watumishi kadhaa duniani “wenye majina” kuibeba na kuifanya sehemu ya mahubiri yao kipindi hiki cha taharuki. Kwenye makala hii, ninafafanua teknolojia ya 5G kwa kifupi, madhara yake, na kujaribu kuonesha mapungufu ya nadharia njama kuhusu uhusiano wa 5G na Covid-19. Lengo kuu ni kutoa mwanga kwenye jamii yetu kuhusu kinachosambazwa kupitia nadharia njama ya 5G na kuibua mjadala utakaotusaidia kuujua ukweli wa jambo hili tunapopambana na Covid-19. Kwa undani zaidi, soma makala nzima.

View attachment 1412217
Utangulizi.
Katika mapambano dhidi ya mlipuko wa Covid-19 kwenye nchi yetu na nyingi za Afrika, kuna eneo moja halijatazamwa kwa mapana yake. Eneho hilo ni ugonjwa huu kuhusianishwa na nadharia njama kadhaa na kupewa tafsiri za kiimani kuliko za kisayansi. Kwa kufanya hivyo, kuna hatari kwa baadhi ya watu kupuuzia mlipuko huu na hivyo kuhatarisha maambukizi kua makubwa. Pili, nadharia njama zinaongeza taharuki ya mlipuko na kuwapa watu madhara ya kisaikolojia kujiona wamezungukwa na hatari muda wote kutoka kwa watu wasiowajua. Ukifuatilia kwenye internet na vyombo vya habari vya kimataifa, utaona kuna kundi kubwa la watu hawaamini kama Covid-19 ni ugonjwa unaosababishwa na virusi ambao ni viumbe wa kawaida tulionao kwenye dunia hii. Kinyume chake wanaamini kuna njama, ama za kibaguzi, kibishara, au za kiimani zilizopelekea watu fulani wasiotajwa kutengeneza au kusababisha kutokea kwa ugonjwa wa Covid-19. Moja ya nadharia hizo ni ile inayoaminisha kwamba Covid-19 inasababishwa na teknolojia mpya ya mawasiliano ya 5G.

Je,5G ni kitu gani?
Teknolojia ya mawasiliano ya simu imekuwa ikipanuka na kuendelea siku hadi siku. Teknolojia ya mawasiliano ndio iliyokua kwa kasi zaidi katika historia ya kizazi chetu. Pamoja na mambo mengine, ukuaji wa teknolojia ya mawasiliano unapimwa kwa spidi/kasi ya kusafirisha data kati ya pande mbili zinazowasiliana. Kwa miaka mingi, spidi ya data imekuwa ikiboreshwa na kuongezeka kwa kuboresha miundombinu ya mawasiliano (hardware na software). Hivyo, tangu mwaka 1940, tumetoka kwenye teknolojia inayoitwa 0G (herufi “G” ikimaanisha Generation au kizazi) kwenda kwenye teknolojia inayoitwa 4G (4 generation au kizazi cha 4) tunayotumia sasa.

Kwa sasa, wavumbuzi wameibuka na teknolojia ya 5G ambayo ina spidi kubwa zaidi inayoweza kusafirisha zaidi ya 1 Gbit za data kwa sekunde. Kwa spidi hii kali, tunaweza kufanya kazi nzito zaidi ambazo teknolojia zilizopita haziwezi. Kwa mfano, teknolojia hii inaweza kutumika kwenye magari yanayojiendesha yenyewe (self-driving/autonomous cars); uwezo wa kuunganisha vitu mbalimbali katika mtandao kwa urahisi (Internet of Things); kuwa na miji yenye huduma za kijamii zilizojengwa na kuboreshwa kwa teknolojia ya mawasiliano (smart cities); kuongoza vyombo vya usafiri; vifaa vya burudani; nk. Teknolojia ya 5G inamwingiza binadamu kwenye aina mpya kabisa ya kuishi, na maisha yanatazamiwa kuboreshwa kwa sehemu kubwa. Lakini swali kubwa la kujiuliza hapa ni nini hasa kinatusukuma tunahamia 5G na tutapata faida au athari gani?

Ili kujua kwa nini dunia inaongelea 5G ni lazima uitazame kama kijiji kinachoendelea kwa kasi kubwa na hivyo kupelekea mabadiliko ya mahitaji mengi. Mathalani, kiwango cha data/taarifa kinachozalishwa katika dunia ni kikubwa mno. Ukichukulia mtandao wa Google pekee tuliouzoea, kila siku unazalisha takribani 20 petabytes (10PT) za data (Petabyte 1 ni sawa na Gigabyte (GB) milioni 1). Pia, sekta ya tamthilia (movie) inahama kwa kazi kutoka kutegemea video zinazouzwa kwa njia ya DVD au kaseti kuelekea kutazama tamthilia online kupitia mitandano kama Youtube na Netflix. Pia, utazamaji wa television unahamia kwenye Smart TV ambazo zinakupa uwezo wa kutazama television huku ukiwa unapata huduma nyingi kwa mtandao mithili ya matumizi ya kompyuta. Mahitaji haya ndiyo yalifanya wavumbuzi waanze kufikiria namna ya kuongeza uwezo wa kusafirisha data na kuibuka na 5G. Makampuni ya mawasiliano yanakimbilia kuwekeza katika teknolojia ya 5G kwa sababu ya faida nyingi ambazo wataje wao watapata. hata hivyo kuna changamoto kubwa mbili za 5G kimuondombinu.

 1. Teknolojia ya 5G inahitaji uwekezaji mkubwa wa miundombinu mipya ya mawasiliano kwa sababu inalazimisha kubadilisha ile iliyoko kwa sehemu kubwa. Hadi sasa kuna takribani nchi 35 (nyingi zikiwa tajiri) ambazo tayari zina miundombinu ya 5G na bado inajengwa. Ufungaji wa miundombinu hii kwa nchi nyingi umeanza mwaka 2019.

  Nchi zinazoongoza kuwa na miundombinu ya 5G kwenye miji mingi ni South Korea, China, na Marekani. Kwa miaka kama 2 iliyopita, utakua umesikia siasa za 5G kati ya mataifa makubwa hasa Marekani, Uingereza na China. Hii imetokana na ukweli kwamba kampuni ya Huawei ya wachina imekua mbele hatua kadhaa kiteknolojia na kuzifanya nchi nyingi zikiwemo za Magharibi kutumia teknolojia zake ikiwemo kuweka miundombinu ya 5G. Hii imewapa taharuki maadui zao kiuchumi hasa Marekani kwa hoja kwamba mitambo yao sio salama kwa kuwa inaratibiwa au kudukuliwa na serikali ya China (hili tuliachie hapa maana ni mjadala mwingine).

 2. Nyingine ni ukweli kwamba wateja watalazimika kuwa na vifaa vilivyotengenezwa kutumia teknoljia ya 5G, na hivyo kuingia gharama ya ziada/kubwa.
Pamoja na changamoto hizi na nyingine, bado 5G inatoa matumaini mapya ya maendeleo yatakayomwezesha binadamu kufanya shughuli nyingi ngumu kwa muda mfupi. 5G inafanikishwa mambo mawili makubwa. Moja ni kiwango cha data kinachoweza kusafirishwa, na mbili ni spidi/kasi ya data kusafiri kati ya kifaa kimoja na kingine.

Je, 5G ina madhara gani kiafya?
Nadharia njama ya 5G imejikita katika kile kinachoitwa madhara makubwa ya 5G kwa afya zetu. Kumesambaa habari nyingi duniani zilizoanzishwa na watu wachache na zimeshika kazi kama moto wa mabua kiasi kwamba zimeanza kuaminika kama ukweli. Hii imepelekea siku ya jana mtandao wa Youtube kuamu kuanza kufuta video zote kwenye mfumo wao zinazoongela nadharia njama ya G5 na uhusiano wake na Covid-19 (tazama hapa). Katika nchi za kiafrika ambapo kwa sehemu kubwa tumeturuhu watu wengine wafikirie na hata kuamua kwa niaba yetu, nadharia hii imeingizwa kwenye viunga vya kiimani na imeshakua ukweli kwa watu wengi maana huwa tunaogopa kuhoji mambo ya kiimani au wanachokisema watumishi.

Nimesikiliza na kusoma maelezo ya waanzilishi na wainjilisti wa nadharia njama ya 5G ili kuelewa msingi wa taharuki wanayoijenga. Mengi wanayoongea ni uongo, uzushi, ya kuungaunga, na hayana usahihi wowote kisayansi wala kiimani. Nadharia hii imeanzishwa na wataalamu wa nadharia njama (conspirancy theorists - wawili wakiwa ni waingereza) na kudakwa na baadhi ya watumishi “wenye majina” kama hoja ya mahubiri yao. Baadhi ya watumishi (hasa wa kikristo) hupenda kujionesha kua wao wana majibu au maelezo ya kila jambo duniani. Hivyo wamechukua hoja ya 5G na kuitumia kama ilivyo au kwa kuitohoa kujengea hoja za chanzo na malengo ya Covid-19. Nitaje kwa kifupi baadhi ya hoja zilizoko kwenye nadharia njama ya 5G.

 1. Taswira inajengwa kwamba kuna mkakati wa watu ambao wanaleta teknolojia ya 5G kwa lengo la kuitawala dunia na hasa kutufanya sisi wanadamu wote kuunganishwa kwenye mtandao mmoja ili kuweza kutaribiwa. Mkakati huu unapewa majina mengi lakini mojawapo ni mbinu ya kufanikisha kinachoitwa “New World Order (NWO)”. NWO ni nadharia njama inayodai kuna kundi la siri lenye nguvu kuliko mataifa yote litakaloitawala dunia nzima kibabe.
  UDHAIFU: wanaoaminisha nadharia hii hawataji watu hao ni kina nani, wako nchi gani, na iwapo ni wa dunia hii au sayari nyingine. Ukiachilia kutajwa kwa baadhi ya viongozi wakuu wa baadhi ya nchi na dini kubwa, nadharia hii inabaki kuwa yakufirika na imekuwepo kwa muda mrefu.

 2. Hoja inajengwa kwamba vifaa vya teknolojia ya 5G vina mionzi mikali yenye madhara kwenye miili yetu. Katika kupambana nayo, miili yetu inatengeneza virusi wa Corona.
  UDHAIFU: Moja, hakuna ushahidi wa kisayansi wowote juu ya hili. Pili, kama miili yetu inatengeneza virusi wa Corona tunapopigwa na mionzi ya 5G, kwa nini basi tusingekua tunaugua wote kwenye eneo lenye 5G? Tatu, kwa nini watu wanaoathirika wanapona?

 3. Wakati huohuo wanadai Covid-19 inasambazwa kwa watu kupitia vipimo tunavyofanyiwa kujua iwapo tuna maambukizi. Lengo kubwa la kuingiziwa virusi hivi ni ili dunia nzima iwe na maambukizi kisha kupitishwe taratibu/sheria inayomtaka kila mtu lazima apewe chanjo ya kumkinga na Covid-19. Kupitia chanjo hiyo tutaingiziwa “chip” ndogo ya mawasiliano kwenye miili yetu (mithili ya line ya simu yako) itakayowezesha watu hao wasiojulikana kutufuatilia kama vile mitambo ya kompyuta. Pia, mtu hataweza kupata visa kuingia nchi nyingine iwapo hajathibitisha kua na una kinga ya Covid-19.
  UDHAIFU: Moja, tuna ushahidi kutoka nchi nyingi watu kuambukizwa na kueonesha dalili (wengine hadi kufariki) kabla ya kupimwa. Pili, ili uweze kupachika chip ya kielekroniki ifanye kazi na kuweza kusafirisha data na mfumo wa mwili, ni lazima ipachikwe mahili maalumu na kuunganishwa na mfumo wa mawasiliano wa mwili. Wanaohubiri nadharia hii hawatuelezi ni kwa jinsi gani chanjo tutakayopewa (ama vidonge au kimiminika) itaingiza chip mwilini na ikafanye kazi.

 4. Wakristo wanatahadharishwa kwamba 5G ni mpango wa shetani na Covid-19 ni vita dhidi yao. Wengine wanakwenda mbali zaidi kudai Covid-19 imetengenezwa kwa lengo la kuangamiza waafrika ila waliotengeneza wamekosea ikawaathiri wao wenyewe.
  UDHAIFU: Hoja hii ni dhaifu kama zingine maana ni ya kufikirika.

 5. Katika kujenga hoja zao, baadhi ya manabii wa njama hii wanasema virusi sio viumbe halisia bali wanatengenezwa kwa malengo mabaya.
  UDHAIFU: Huu ni uongo ulioopitiliza kwani wanasayansi wa viorolojia wanatuambia kuna aina takribani 5,000 ya virusi wa asili duniani. Sifa kubwa ya virusi ni kutokua na uwezo wa kuishi wenyewe bila kuwa ndani au juu ya kiumbe kingine. Hivyo wanaweza kuishi kwa wanadamu, wanyama, ndege, samaki, mimea na hata viumbe vidogo kama bakteria. Hata hivyo wataalamu wa bayoteknolojia wanaweza kutengeneza virusi kwa njia za kimaabara kwa malengo mbalimbali.

 6. Wanajenga hoja kwamba kirusi cha Corona ni kipya na hajawahi kuwepo. Moja ya filamu ya kijapani iliyotengenezwa 2018 ina kipengele wanachotaja visuri wa Corona hivyo kipengele hiki kinatumika kuthibitisha kwamba Corona ni mkakati wa silaha za kibalojia.
  UDHAIFU: Hoja hii inadhirisha jinsi upotoshaji huu usivyo na mashiko. Virusi wanaosababisha Covid-19 (yaani SARS-CoV-2), ni kafamilia kamoja tu kati ya familia karibu 60 za ukoo wa Coronavirus. Wana dada yao anaitwa SARS-CoV-1 aliyesababisha mlipuko wa SARS kule China mwaka 2002/2004 lakini ukadhibitiwa. Pia wana binamu naitwa MERS-Cov aliyelipuka kule uarabuni 2012 na kudhibitiwa pia.
Uhalisia uko wapi?
Kuna uwezekano mkubwa wa teknolojia ya mawasiliano kuwa na madhara kiafya kama zilivyo teknolojia nyingi tunazotumia kila siku (magari, simu za mikononi, kompyuta, nk). Kwenye teknolojia ya mawasiliano, madhara yanahusishwa moja kwa moja na mionzi inayotumika kusafirisha data (kwa mfano simu zetu kuwasiliana na minara ya mawasiliano au na kifaa cha kupata mtandao wa intenet kwa njia ya upepo (WiFi)).

Kwa mfano, tafiti kadhaa zilizofanyika nchi kama India, Australia, Marekani, Ufaransa, nk, zimeonesha uwezekano wa madhara yatokanayo na matumizi ya simu za mikononi (sio za 5G). Ziko tafiti zimeonesha mionzi ya simu inaweza kusabanisha kansa, kuharibu mbegu za kiume, nk. Watafiti wanatoa tahadhari na kuwashauri watu kupuunguza mawasiliano ya simu za mikononi na kuzitaka kampuni zinazotengeneza simu kuwa wawazi kwa kuweka tahadhari wazi juu ya madhara mtu anayoweza kuyapata kwa kutumia simu. Wanashauri tuwazuie watoto kutumia simu na vifaa vingine vyenye WiFi ili kuzuia madhara ya mionzi ambayo imeonekana inaweza kusababisha kansa ya ubongo.

Kuna mjadala na mvutano mkubwa kati ya watafiti na watu walio kwenye sekta ya mawasiliano kuhusu ukweli wa madhara vifaa vya mawasiliano. Wanaopinga uwepo wa madhara wanasema hakuna ushahidi wa kutosha kuthibitisha yale yanayodaiwa [Hii ni mada ndefu hivyo kwa sasa niiachie hapa nirudi kwenye 5G].

Hivyo basi, kama simu ambazo tayari tunatumia zenye teknolojia ya 2G, 3G au 4G zimethibitika kwamba zinaweza kua na madhara yatokanayo na mionzi, ni wazi 5G inaweza kuwa na ina hiyohiyo ya madhara. Yanaweza yakawa ama nafuu zaidi kutokana na maendeleo ya teknolojia au makali zaidi kwa sababu hiyohiyo. Manabii wa nadharia njama ya 5G wanajenga hoja kwamba mionzi itokayo kwenye vifaa vya 5G ina nguvu isiyoweza kustahimilika na miili yetu.

Hata hivyo, lazima tutambue kwamba, wagunduzi wa mawasiliano nao ni binadamu na wanapotengeneza teknolojia mpya, wanazifanyia tafiti za kina kupima madhara yake kabla ya kuzipitisha kutumika. Pia, kila nchi (hasa zilizoendelea) zina taasisi za viwango, uratibu na udhibiti kwa lengo la kuthibitisha ubora na usalama wa mitambo ya mawasiliano kabla ya kutumika katika jamii (sisi tuna TCRA). Hakuna taifa/serikali hata moja duniani, iko tayari kufunga mitambo ya mawasiliano ambayo ina madhara kwa watu wake huku wakijua haitachagua nani wa kumdhuru.

Fursa inayotumiwa na wanaohubiri nadharia njama ya 5G
Baadhi ya manabii wa nadharia njama ya 5G ni watu wenye elimu kubwa na ufahamu mpana wa mambo. Wataalamu wengi wa nadharia njama wana akili nyingi na ni wasomi wazuri. Hivyo wanatumia nafasi hiyo kama njia ya kuonesha wanachokiongea kina ukweli. Kunahitajika uwezo mkubwa na uelewa wa mambo kung'amua yaliyo nyuma ya nadharia zao. Hata hivyo, miongoni mwao kuna wengi hawana kabisa uelewa wa teknolojia za mawasiliano na hawana uwezo wa kukuambia 5G ni kitu gani au hizo hatari zinatokeaje katika uhalisia. Ukiwasikiliza vema, wanatumia baadhi ya nadharia za mifumo ya teknolojia ya mawasiliano kwa kuungaunga kama namna ya kuonesha uhatari wa 5G. Wanataja maneno kama artificial intelligence (AI), Internet of Things (IoT) au Machine Leaning (ML) kujazia hoja zao bila kuelewa zinalenga nini hasa. Kwa mtu asiye na eleimu ya mambo haya (na hawa ni wengi kwenye jamii) akitajiwa mambo haya anapata picha inayotisha sana. Kama vile haitoshi, watu hawa hawana uelewa wa kutosha kuhusu epidemilojia ya magonjwa ya mlipuko. Ila, wanafanikiwa kwa kiasi kikubwa kupotosha kwa kua wanajua au kuamini kwamba wanaowasikiliza hawana uelewa wa mambo au elemu yao ni ndogo kuweza kung’amua ukweli au kutafuta usahihi wa wanachokisema.

Hitimisho na Ushauri
Nadharia njama ya 5G na nyingine zina hatarisha watu wengi kuambukizwa na Covid-19 kwani wanaozisambaza wanatoa maelezo yanayokanganya na kuwafanya wengi wasifuate maelekezo ya kisayansi ya ugonjwa huu na namna ya kukabiliana nao. Ndio mana utaelewa ni kwa nini juzi kule Abijan Ivory Coast wananchi wameandama na kwenda kuvunja jengo maalum linaloandaliwa kwa ajili ya kupimia wagonjwa wa Covid-19. Pia utaelewa ni kwa nini, baadhi ya “watumishi” wanahamasisha waumini wao waendelee kufanya ibada za pamoja kwa wingi zaidi wakiamini Covid-19 ni mbinu za mpinga Kristo na wanatakiwa kuamini haitawapata wao. Waliosambaza Covid-19 kwa wingi kule Korea ya Kusini walikua wakristo (walokole) waliopuuzia athari za ugonjwa huu. Waliambukizana kwa wingi na wakafanya karibu mji mzima kulemewa na maambukizi.

Kama nilivyosema kwenye moja ya makala zangu kuhusu janga la Covid-19 na kuziweka
hapa Jamii Forum, mlipuko huu umedhihirisha ni kwa kiasi gani sisi waafrika tulio wengi sio jamii inayoongozwa na elimu, maarifa, sayansi, na teknolojia. Imetuonesha namna tunavyofanya maamuzi yetu bila kutumia taarifa sahihi na tulivyo warahisi kuamini taarifa za uongo, za uzushi, na kutotaka kujishughulisha kutafuta ukweli na maarifa. Pia, imetuonesha namna mfumo wetu wa elimu usivyotuandaa na kutuwezeha kutumia uwezo wetu wa kufikiri, kufanya tafakuri tunduizi, na kuchambua mambo kwa lengo la kutafuta maarifa, ukweli au usahihi wa kile tunachosikia.

Kama vile haitoshi, mlipuko huu umetuonesha namna baadhi ya "watumishi wa dini zetu" wanavyotumia kila fursa wanayoipata kutuweka mbali na ukweli kwa makusudi na kwa manufaa yao binafsi. Hawataki tutumie akili zetu na elimu kutafuta majawabu ya maswali magumu yanatotukabili au suluhisho la changamoto tunazokutana nazo. Kila mara wanataka tutumie fikra za kiimani kama "shortcut" ambayo haitufikishi wanapotuahidi. Ifike mahali, wapendwa hawa wakubali kwamba wao sio miungu na hawana ufunuo wa kila jambo. Wao ni watumishi tu hivyo hawawezi kuwa na maelezo au majawabu ya kila swali au utata unaojitokeza kwenye jamii. Ni sahihi kabisa wakisema hawana maelezo au hawajui au bado wanamwomba wanayemtumikia kupata majawabu. Kukiri hivi hakuwapunguzii kitu katika nafasi yao ya utumishi. Pia kwa mambo ya kitaalamu/kisayansi, ni vema wakatafuta wabobezi wa eneo husika wakawapa mwanga wa kutosha wa kisayansi kabla ya kuyaongelea kwa umma katika muktadha wa kiimani. Hii ina msaada mkuwa sana na inawapa heshima hata nje ya waumini wao. Wana fursa kubwa ya kupata maelezo ya kitaalamu tena bure kutoka kwa makundi yao na hata wasio wa makundi yao.

Moja ya mambo yanayotuchelewesha waafrika kuendelea kwa kasi kama mataifa mengine tuyatazamayo kama vielelezo, ni kuhoji kila kitu kigeni kwa mtizamo wa kukiogopa au kukishuku huku tukiwa hatuna maelezo sahihi wala uthibitisho wa tunachoamini/kuaminishwa/kuwaaminisha wengine. Mbaya zaidi tunakua hatuna mbadala wa kuwapa tunaowajengea hofu. Unawaaminisha watu kuwa 5G ni hatari au ni shetani huku mfukoni una simu ya 4/5G na hotuba au mahubiri unayotoa unayarusha live kwa Youtube inayotumia teknolojia ya 5G kuweza kustahimili wingi wa watu wanayoitumia. Pia una accounts za mitandao ya kijamii ambayo kwa sehemu kubwa zinategemea teknolojia unayopambana nayo. Sasa tukuamini kwa lipi?

Zingatia
 1. Uchambuzi na maoni niliyoyatoa hapa, hayamaanishi kwamba ninaamini hakuna madhara yanayoweza kusababishwa na teknolojia ya 5G. Pia, hayamaanishi ninapinga watu kuhojia, kutafiti, au kuweka mashaka kuhusu usalama wa teknolojia hii. Hapana. Hoja yangu nya msingi ni kutofautina na upotofu unaonezwa na nadharia njama ya kuhusianisha Covid-19 na 5G. Tuhoji na kutafiti madhara ya 5G na mambo mengine (kama ni lazima) kwa kutumia ukweli na ushahidi wa kisayansi badala ya dhana za kufikirika na ndoto za abunuwasi.

  Sehemu kubwa ya Afrika tuko kwenye mkwamo kama jamii na mapokeo tuliyoletewa na waliotutawala (hasa imani) yanatuathiri kifikra na kimitazamo kuliko waliozinzisha. Hivyo tukimaliza hili la Covid-19, tuanze kuweka mikakati ya muda mrefu ya kujikwamua tulipokwama ili kurahisha maendeleo ya watu na vitu. Pamoja na bidii na imani zetu, tunahitaji elimu na maarifa sahihi ili tuweze kupiga hatua na kuleta maendeleo endelevu.

 2. Uchambuzi huu haujalenga kuwashambulia wakristo au "watumishi" kwani nami ni mmoja wao. Nimetaja ukristo (tena kwa tahadhari kubwa) maana ndio kundi nililoko na ninashuhudia jinsi baadhi yetu wanavyokazana kupotosha kuhusu Covid-19 na kinaathiri jamii kubwa.

 3. Neno "Nadharia Njama" sio rasmi katika viunga vya lugha ya Kiswahili bali nimelitohoa mimi mwenyewe baada ya kuketi na kamusi za Kiswahili nikiwa natafuta tafsiri/maana ya "Consipiracy Theory". Sifahamu tafsiri rasmi ya dhana hii kwa Kiswahili.

Mathew Togolani Mndeme (mmtogolani@gmail.com)
Mtafiti wa mifumo ya digitali kwenye ufuatiliaji na udhibiti wa magonjwa

 • Shukrani kwa classmate wangu Dr. Baraka Maiseli (Lecturer in Electronic and Telecommunications Engineering, UDSM) kwa ushauri kwenye ufafanuzi wa teknolojia ya 5G
Bandiko lako linatoa changamoto la "kifikra" na "imani" kwa Watumishi wa Mungu wanaodai kuponya magonjwa nje ya utaratibu wa kisayansi, na waumini wanao waamini.

Mlipuko wa COVID-19 unaweza kuwa mwisho wa "wahubiri makajanja" ambao wanatumia udhaifu wa waumini kuishi kwa imani zaidi kuliko uhalisia wa kisayansi.
 
MakinikiA

JF-Expert Member
Jun 7, 2017
3,055
2,000
wachina wame launch 5G so wanatoa sadaka,popote penye product ya mchina corona lazima iguse..... :cool: :cool: :cool: :cool: :cool: :cool: 😷😷😷
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom