Teknolojia: Viongozi wa serikali ya JK watapeliwa mihela | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Teknolojia: Viongozi wa serikali ya JK watapeliwa mihela

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KANDA MBILI, Jul 17, 2012.

 1. KANDA MBILI

  KANDA MBILI Member

  #1
  Jul 17, 2012
  Joined: Jul 9, 2012
  Messages: 56
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 25
  Viongozi waandamizi wa Serikali wakimemo Wakuu wa Wilaya na Maofisa Elimu wa Wilaya katika mikoa kadhaa nchini, wametapeliwa mamilioni ya fedha na kikundi cha watu wanaotumia jina la Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo, Katibu wa Siasa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye huku wengine wakijitambulisha kuwa ni maafisa Usalama wa Taifa.

  Habari za uhakika zilizothibitishwa na viongozi wenyewe ni kwamba viongozi hao wametapeliwa kwa kutumia mtandao wa simu na wanatoka katika wilaya za mikoa ya Tabora, Kigoma na Pwani.

  Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mulugo, alipoulizwa suala hilo alithibitisha kupokea taarifa hizo kutoka maeneo mbalimbali kwamba Maafisa Elimu wakiwemo Wakuu wa Wilaya wametapeliwa kwa kutumia jina lake.
  “Nipo njiani naelekea Mbeya kwenye matatizo, lakini utapeli huo nimeusikia ambapo Maafisa Elimu wa Tabora, Kigoma na Rufiji wakiwemo baadhi ya Wakuu wa Wilaya wametapeliwa kwa kutumia jina langu na leo (juzi) hii nimeelezwa kuwa Ofisa Elimu Wilaya ya Rufiji ametapeliwa Sh. 800,000,” alisema Mulugo.

  Mkuu wa Wilaya ya Uvinza, Kigoma, Hadija Nyembo, ni miongoni mwa viongozi waliotapeliwa Sh. 700,000 siku ya Jumatano, wiki iliyopita.

  Katika sakata hili namba zinazotumika kutapeli ni 0718 015 554 na 0754 967 357 na 0759342027 na 0757273380 na 0659105925 ambazo wapigaji hujitambulisha kama maofisa mbalilimbali wakiwemo USALAMA WA TAIFA(TISS), WAKUU WA CCM KUTOKA MAKAO MAKUU LUMUMBA DAR, NAPE NAUYE, NAIBU WAZIRI WA ELIMU(mulugo philipo)

  Source:NIPASHE

  MY TAKE:
  Siku hizi inavyoelekea jina la usalama wa taifa ni BIG DEAL mjini...I think ukitaka kumliza muheshimiwa yeyote we jitambulishe unatoka TISS fasta unapewa chako.labda kwa sababu ya uoga wa kuokotwa mabwepende.

   
 2. Kennedy

  Kennedy JF-Expert Member

  #2
  Jul 17, 2012
  Joined: Dec 28, 2011
  Messages: 11,251
  Likes Received: 2,931
  Trophy Points: 280
  Waliotapeliwa wanafanana na ccm yao,TISS wenyewe wana njaa kama wengine.
   
 3. N

  Ni Mimi Msiogope JF-Expert Member

  #3
  Jul 17, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 352
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hehehehe...

  Liwalo na Liwe
   
 4. KANDA MBILI

  KANDA MBILI Member

  #4
  Jul 17, 2012
  Joined: Jul 9, 2012
  Messages: 56
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 25
  lishakuwa mkuu.......
   
 5. Makala Jr

  Makala Jr JF-Expert Member

  #5
  Jul 17, 2012
  Joined: Aug 25, 2011
  Messages: 3,397
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Hao ndo viongozi wasomi wa ccm,very poor in reasoning before acting.How comes for Intellectual Leaders to be robbed so easily without asking for ID verifications? Hawa ndo watahusika kwenye mikataba ya uwekezaji kwenye halmashauri,watawezaje? CHADEMA tukichukua nchi upuuzi huu hautavumiliwa!
   
 6. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #6
  Jul 17, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Wanatapeliana wenyewe kwa wenyewe, wote wapo kwenye kundi la Mafisadi. Sisi walalahoi tunawasubiria 2015 watakiona cha moto
   
 7. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #7
  Jul 17, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,778
  Likes Received: 36,776
  Trophy Points: 280
  Kwa iyo hata kama wangekuwa ni usalama taifa au nape wangestahili kupatiwa fedha hizo kutoka kwa hao maafisa elimu??

  Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
   
 8. KANDA MBILI

  KANDA MBILI Member

  #8
  Jul 17, 2012
  Joined: Jul 9, 2012
  Messages: 56
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 25
  yawezekana washazoea kumtumia kwenye ishu fulani fulani si unajua tena magamba "UKITAKA KULA SHARTI ULIWE KIDOGO"
   
Loading...