Teknolojia na ubunifu wa kampuni za simu unakuza biashara nchini

wanzagitalewa

Senior Member
Jan 25, 2018
128
84
Ni jambo lililo wazi kuwa, teknolojia ni msingi wa maendeleo ya biashara nyingi. Kuanzia kwenye mifumo ya kupokea malipo, kulipa wafanyakazi, kuhifadhi taarifa muhimu hadi kutafanya utafiti wa masoko; kote huko teknolojia inahakikisha mambo yanakwenda sawia. Kwa maana hiyo, ili kuhakikisha biashara zinakwenda vyema katika zama hizi, teknolojia ni lazima iwe jambo la msingi.

Kampuni nyingi hapa nchini hasa zile ndogo na za kati zinategemea huduma ya teknolojia toka kampuni za mawasiliano ya simu. Kampuni ya Tigo Tanzania ni moja ya kampuni za simu ambazo zinazipa kipaumbele biashara ndogo na za kati kuziwezesha kukua kupitia huduma za kiteknolojia. Tigo inatoa huduma kama Bulk SMS kwa kampuni mbalimbali kuziwezesha kuwasiliana na wateja wao kwa bei rahisi, huku pia ikitoa huduma bora ya mtandao wa intaneti kusaidia ukuaji wa biashara hizo.

Hivi sasa Tigo imeanzisha huduma Customer Service Portal ambayo inasaidia kampuni na mashirika mbalimbali kukua katika ulimwengu huu wa teknolojia. Huduma hii inawezesha watumiaji kuona mwenendo wa biashara yao kila wakati kama malipo, matumizi na mapato na kuwawezesha kujua walipo na wanapoelekea muda wowote wanapotaka kufanya hivyo.

Mbali na huduma hii, Tigo pia ndiyo kampuni pekee inayomiliki na kuendesha kituo cha kuhifadhi takwimu (data centre) chenye hadhi ya juu ya Tier II nchini. Katika zama hizi ambazo takwimu na taarifa ni jambo la muhimu sana,Tigo inahakikisha kuwa inawapa watumiaji wake uwezo wa kuhifadhi taarifa zao kwa ubora wa hali ya juu kabisa.

Tunaweza kusema bila kupepesa macho kuwa kwa huduma kama hizi na nyingine lukuki, Tigo inaongoza njia katika teknolojia na ubunifu kusaidia kukua kwa biashara ndogo na za kati.

Hii ni habari njema kwa wateja wa Tigo ambao kila mara wamekuwa wakinufaika na huduma bora za kampuni hii.

Tigo inakusudia kuhakikisha kuwa huduma hizi zinapatikana kwa kila Mtanzania, kila kona ya nchi.

Kama ilivyoripotiwa, Tigo sasa imejiunga na Zantel. Hatua hii inazifanya kampuni hizo mbili kuunganisha huduma zake Tanzania bara na visiwani. Habari njema sana hii kwa wateja kwani punde si punde wateja wa kampuni zote mbili wataanza kufurahia huduma na faida zote zipatikanazo katika kampuni hizo mbili.
 
Basi ntaleta taarifa zangu muhimu mnihifadhie,mnacharge bei gani kuhifadhi taarifa?
 
Back
Top Bottom