Teknolojia imebadili mfumo wa maisha, vijana wa sasa wanashindwa kuandika kwa mkono

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,595
215,272
Usishangae kukutana na mwanafunzi wa elimu ya juu anaeandika na ukashindwa kusoma muandiko wake. Vijana wanafanya kazi za shule kwa kutumia computer, wanatumiana ujumbe kwa simu. Hii imefanya sanaa ya uandishi wa mkono kupotea.

Vitabu siku hizi wanasoma kwenye kindle. Niliongea na binti mmoja na kumfahamisha kuwa mpaka sasa huwa nina print journal articles, alinicheka na kuniambia si rafiki wa mazingira. Zaidi ya social media kusoma vitabu na journals za umeme nimeshindwa.

Walimu wafikirie njia ya kutoa tunzo la miandiko bora ili kutunza sanaa hii muhimu iliyohitajika kwa vizazi vijavyo.

1634704867534.png

Kiti chenye kabati la vitabu, matumizi ya viti vya aina hii si muhimu kwa vijana wa leo
 
Usishangae kukutana na mwanafunzi wa elimu ya juu anaeandika na ukashindwa kusoma muandiko wake. Vijana wanafanya kazi za shule kwa kutumia computer, wanatumiana ujumbe kwa simu...
Nilionaga miaka zaidi ya 20 iliyopita wazungu wengi wana miandiko mibaya, finally nimekuja kuelewa sababu, na mimi leo nikitaka kuandika kwa mwandiko mzuri lazima nitumie ALL CAPS, otherwise hati itakuwa mbaya.

Wakati nipo shule nilikuwa mmoja kati ya wanafunzi wenye hati safi, baba na mama ndio usiseme miandiko yao utadhani ni ni new roman au Tahoma.
 
Back
Top Bottom