Elections 2010 Teja wa MwanaHalisi

Ng'wanangwa

JF-Expert Member
Aug 28, 2010
10,827
4,172
Leo katika pilikapilika zangu za kutaka kuwahi kazini nilikuwa na akili moja tu kichwani, "kununua na kusoma MwanaHalisi".

Nikashuka kituo cha daladala. Kituo cha kwanza kwa muuza magazeti.

"Naomba MwanaHalisi". Akanijibu, "sina". Nikakasirika. Nikaenda kijiwe kingine cha kuuza magazeti: "Naomba MwanaHalisi". Jibu: "Sina".

Akili ikanijia: "Hivi leo siku gani?".

Nikacheki Casio yangu orijino: Tuesday.

Aaaaaaaaaaaaaaah!!!!

Kimyakimya nikachukua Mwananchi nikatambaa.

Ila nikagundua kitu kimoja: Wauza magazeti wa bongo ni vilaza kiaina. Kati ya wawili niliowauliza hakuna hata mmoja aliyenijibu kuwa leo siyo Jumatano.

Come Wednesday.
 
Labda walidhania unaulizia toleo la wiki iliyopita ambalo kinadharia linatakiwa liwe bado linauzwa hadi leo Jumanne kama bado wanalo.
 
Labda walidhania unaulizia toleo la wiki iliyopita ambalo kinadharia linatakiwa liwe bado linauzwa hadi leo Jumanne kama bado wanalo.

heshima kwako MMK.

Ahsante kuwatetea, lakini laiti kama wangejua....nilikuwa namaanisha leo Jumatano
 
Labda walidhania unaulizia toleo la wiki iliyopita ambalo kinadharia linatakiwa liwe bado linauzwa hadi leo Jumanne kama bado wanalo.
Mwanakijiji amini usiamini Si rahisi kupata mwanahalisi Alhamisi wako juu na siku hizi wanauza si mchezo!
 
Back
Top Bottom