Teja wa MwanaHalisi

Ng'wanangwa

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2010
Messages
10,429
Likes
1,279
Points
280

Ng'wanangwa

JF-Expert Member
Joined Aug 28, 2010
10,429 1,279 280
Leo katika pilikapilika zangu za kutaka kuwahi kazini nilikuwa na akili moja tu kichwani, "kununua na kusoma MwanaHalisi".

Nikashuka kituo cha daladala. Kituo cha kwanza kwa muuza magazeti.

"Naomba MwanaHalisi". Akanijibu, "sina". Nikakasirika. Nikaenda kijiwe kingine cha kuuza magazeti: "Naomba MwanaHalisi". Jibu: "Sina".

Akili ikanijia: "Hivi leo siku gani?".

Nikacheki Casio yangu orijino: Tuesday.

Aaaaaaaaaaaaaaah!!!!

Kimyakimya nikachukua Mwananchi nikatambaa.

Ila nikagundua kitu kimoja: Wauza magazeti wa bongo ni vilaza kiaina. Kati ya wawili niliowauliza hakuna hata mmoja aliyenijibu kuwa leo siyo Jumatano.

Come Wednesday.
 

Forum statistics

Threads 1,203,564
Members 456,824
Posts 28,119,016