SoC01 TEHAMA kwenye kulinda mazingira

Stories of Change - 2021 Competition

muhin

Member
Jul 16, 2021
7
6
Maana ya baadhi ya maneno

Application
Mfumo ambao hutumika kwa shughuli husika

Android application
Mfumo unaofanyakazi kwenye simu zinazotumia OS ya android

Apple application
Mfumo unaofanyakazi kwenye simu zinazotumia OS ya apple

Apple store
Sehemu ambayo imehifadhiwa mifumo mbalimbali ya ya apple
Play store
Sehemu ambayo imehifadhiwa mifumo mbalimbali ya android
Web based application
Mfumo unaofanyakazi kwenye tovuti.
TEHAMA
Teknologia ya habari na mawasiliano

Utangulizi
Kwa sasa dunia kila siku inapiga hatua moja mbele kwenye upande wa teknologia na sayansi hivyo basi kwa baadhi ya maendeleo ya sayansi na teknologia huleta uchafuzi wa mazingira, uchafuzi huo hutokana na maendeleo ya viwanda ambayo huchangia kwa asilimia zaidi ya 70 kwenye kuleta uchafuzi wa mazingira na kwa upande mwengine uchafuzi huo hukosa huduma ya kuondolewa kwa haraka kwa nchi kama zetu kutokana na teknologia tunayoitumia kwenye kuondoa taka hizo kwa watumiaji wa mwisho wa bidhaa kutoka viwandani na sehemu zingine.

Kulingana na hali ilivyo kwa sasa serikali na wadau tofauti tofauti wanajikita kwenye kupunguza athari za uchafuzi wa mazingira kwa juhudi mbalimbali wanazozifanya ili kujaribu kuondoa tatizo la uchafuzi wa mazigira lakini uhalisia bado tatizo hili la kuwa na mazingira machafu bado lipo kwenye jamii zetu na baadhi ya sehemu za kazi.

Kwa ajili iyo nimeonelea kubuni juhudi hii kwenye upande huo ili kuhakikisha tunapunguza uchafuzi wa mazingira haswa katika upande wa jamii zetu na baadhi ya sehemu za kazi zetu.

Tatizo

Uhalisia ulivyo kwa sasa tunajitahid kutumia njia mbadala ya kupunguza tatizo la uchafuzi wa mazingira kama vile vifungashio vinavyoweza kuoza kwa haraka lakini kwa upande mwengine bado hatujautumia ufanisi zaidi katika kutatua jambo hilo kwa upande wa teknologia ya TEHAMA sababu ina mchango mkubwa kwenye kutatua changamoto hii tuliyonayo
Kulingana na matatizo ya uchafuzi wa mazingira nimeonelea kuondoa tatizo la uchafuzi katika ngazi ya jamii na sehemu za kazi zetu kwenye upande huu wa TEHAMA kwa kuenda sambamba na teknologia inavyokua kila siku ili kupunguza athari za mazalia ya viwanda na mabaki ya kila siku ya matumiz ya wanadamu .
Naamini teknologia ya TEHAMA ina ufanisi wa haraka kwenye kutatua changamoto hii.

Utekelezaji

Kutokana na teknologia ilivyo kwa sasa wengi wa watu katika jamii wanatumia simu janja (smartphone) na kompyuta kwenye matumizi tofautofauti ambazo zenyewe tukizitumia kwenye upande mwengine tunaweza kupunguza athari zinazotokana na mabaki ya matumizi ya wanadamu(takataka) ya kila siku ambayo hukaa kwa muda mrefu bila ya kuondolewa kutokana na ukosefu wa uratibu mzuri wa kidigitali katika sekta hii
Teknologia hii itafanya kazi kwa kutumia mifumo ya android application , apple application pamoja na web based application ambayo kwanza itababadili mfumo wa uzoaji taka uliopo kutoka analogia kwenda kidigitali pili utaongeza ufanisi zaidi sababu utawezesha uondoshwaji wa taka kwa haraka zaidi.


Ufanyaji kazi

Mfumo huu utajulikana kama safisha hub ambao watumiaji wataipakua kutoka kutoka kwenye play store na apple store , ufanyaji kazi wake itahusisha watumiaji ambao ni jamii na wazabuni mbalimbali ambao watajisajili kwenye mfumo huo kwa lengo la kutoa huduma.
Kwa upande wa watumiamiaj baada ya kuipakua watajisajili ili kufahamu sehemu walipo ili iwe rahisi kufikiwa na huduma ya safisha hub kwa haraka na pia kwa wazabuni ambao wao watajisajil kama watoa huduma wa safisha hub ambao wao watafanya mawasiliana na mteja aliye karibu na wao kwa kuangalia sehemu alipo ili wafike eneo kwa haraka ili wakamuondelee takataka ili kuhifadhi uharibifu mwengine utakaotakana na takataka kwa kukaa muda mrefu bila ya kutolewa
Aina ya takataka ambazo zitasafishwa au kuondolewa ni kama :-
1. Maji machafu
2. Mabaki ya viwandani
3. Takataka za majumbani
4. Takataka za masokoni
5. Takataka za mahospitalini


Maelezo ya ziada
Baada ya kupakupakua huduma hii kutoka play store au apple store
WATUMIAJI WATOAHUDUMA
• Watajisajili kwenye mfumo
Kamavile jina ,sehemu ya kazi au sehemu ya kuishi na nambari ya simu

• Ataomba huduma anayoitaka ya undoshaji wa aina za taka alizokua nazo kwa kuangalia mtoa huduma aliyekaribu na yeye.

• Atakua yu teyari kupokea huduma kwa haraka zaidi kwa kuchagua mtoa huduma aliye karibu na yeye. • Watajisajili kwenye mfumo kamavile jina la kampuni ,jina la mtoa huduma nambari ya gari


• Watapokea maombi kutoka kutoka kwa mteja ambaye ameomba kupatiwa huduma Fulani ya uondoshwaji taka

• Watamfikia anayetaka huduma kwaharaka zaidi kwa kuangalia sehemu alipo.


Lengo kuu

Lengo kuu la mfumo huu kusaidia uondoshwaji wa takataka kwa haraka zaidi ambazo zikikaa kwa muda mrefu huleta au huwa sababu ya matatizo mengine mfano uharibifu wa mazingira na milipuko ya magonjwa mbalimbali kama vile kipindupindu na mengineyo.

Malengo mengine
• Kuisaidia serikali kwenye harakati za kutunza mazingira na athari zinatokana na ukaaji wa muda mrefu wa taka bila kutoka eneo ambalo hazitakiwi kukaa kwa muda mrefu kiasi icho.
• Kuleta ushindani kwenye huduma hii ya uondoshaji takataka kwa kusajili wazabuni tofautitofauti kwa lengo uondoshaji taka kwa haraka zaidi.
• kutoa ajira kwa vijana kwa sababu mfumo huu utatoa mwanya kwa makapuni tofautitofauti ambayo yatajisajili kwa lengo la kutoa huduma hii katika jamii zetu husika.
• Kuongeza pato kwa serikali kwa sababu watumiaji wa mfumo huu watachangia kiasi kidogo kwaajili ya huduma wanayopatiwa ya utolewaji takataka kwa wakati na kwa upande malipo haya serikali watapata pato kwa njia ya moja kwa moja na isiyo ya moja kwa moja.
(a)Kwa njia ya moja kwa moja lazima wazabuni wapate ridhaa ya kufanya shughuli hii katika manispaa za majiji ambazo itawabidi walipe leseni za ufanyaji wa kazi hii
(b)Kwa njia isiyo ya moja kwa moja kama huduma zingine kama vile ununuzi wa umeme (luku) ,ulipaji wa huduma za maji , utumaji wa pesa kwenye mitandao ya simu na mabenki kuna VAT ambayo serikali wanaipata hivyo basi huduma hii itaongeza pato kwa serikali.
• Kutoa fursa kwa vijana kuweza kubuni njia mbadala za kupunguza matatizo yanayozikabili jamii zetu kutakana na elimu wanazozipata kutoka mashuleni , vyuo vya kati pamoja na vyuo vya juu.
• Utoaji wa elimu juu ya umuhimu wa uhifadhi wa mazingira kwa faida ya kizazi cha cha sasa na kijacho.


Hitimisho

TEHAMA huwa na faida kama tukiitumia katika mambo yenye faida kama haya hivyo ni vema wadau mbalimbali waunge mkono wenye wenye mawazo chanya ambayo yanamsaada kwenye jamii zetu kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.
 
Nimelipenda wasilisho lako ndugu. Unadhani unaweza kuwashirikisha watu wengine katika kutekeleza wazo hili.. mfano wataalam wa tehama, hasa wahandisi wa program za simu?
Pm plse
 
Back
Top Bottom