Tegeta wafa na kiu huku wamezungukwa na tanki la dawasco!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tegeta wafa na kiu huku wamezungukwa na tanki la dawasco!!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Am I Crazy?, Jul 27, 2009.

 1. A

  Am I Crazy? Member

  #1
  Jul 27, 2009
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakazi wa Tegeta eneo la wazo hill wamelalamika kwa ukosefu wa maji safi huku wakiishi mita chache tu kutoka lilipo tanki kubwa la dawasco. Jana nilikuwa maeneo ya huko, eneo maarufu kama ''mkorosho bangi'' na kushuhudia jinsi wananchi wanavyopata shida ya maji huku tanki kubwa la kusambaza maji likiwa jirani kabisa na makazi yao!!

  Baadhi ya wakazi niliozungumza nao walidai kuwa tanki hilo linasambaza maji maeneo ya mbezi, mikocheni na masaki huku wao wakiambulia patupu mbali na kuwa jirani na lilipojengwa tanki hilo.

  Waliongezea kusema kuwa walishatuma maombi DAWASCO kuomba kusambaziwa maji, lakini hawakupata jibu lolote la kuridhisha zaidi ya kuona mabomba makubwa yakitandazwa kuelekea mbezi na masaki.

  Wananchi wa huku hutegemea maji ya kununua kwa watu binafsi waliochimba visima ambapo hununua ndoo moja kwa shilingi 200!!! ''Tumechoshwa na kununua maji ya chumvi kwa gharama kubwa huku tukiwa karibu kabisa na tenki la maji, tunaomba serikali kupitia dawasco watuunganishie maji ili tuweze kupata maji safi, uwezo wa kulipa bili tunao'' alisema mwananchi mmoja.


  Swali kwa Dawasco: Je hii ni sawa?????????
   
 2. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #2
  Jul 27, 2009
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Wangapi wamekufa mkuu?
  Wana umri gani?
  Wamefia wapi?
  Wameshazikwa?
   
 3. A

  Am I Crazy? Member

  #3
  Jul 27, 2009
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapo nimetumia msemo, sorry kama hukusoma kiswahili but nadhani waswahili watanielewa. Lengo ni kuwasaidia wananchi hawa wenye matatizo.
   
 4. A

  Am I Crazy? Member

  #4
  Jul 27, 2009
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Nimeona niweke na picha ya hilo tank ili ambao hawajawahi kuliona wajionee wenyewe!

  [​IMG]
   
Loading...