Tegeta, Dar: Mapenzi yamekatisha maisha ya kijana mwenzetu

nipekidogo

JF-Expert Member
Apr 17, 2019
1,587
3,026
Salaam wakuu!

Kuna kila dalili vifo vinavyotokana na mapenzi kuzidi kuongezeka.

Kwa masikitiko makubwa jana tumemuaga jamaa yetu aliyeshambuliwa na mke wake na kupelekea kufariki.

Kwa mashuhuda waliowahi kufika eneo la tukio ni kwamba huyu kijana aliyezaliwa 1991 alikuwa akiishi maeneo ya Tegeta kwa Ndevu na mwanamke waliyebahatika kupata watoto wawili lakini inasemekana mtoto wa pili hakuwa wa huyo mwanaume kwamba mwanamke alimsaliti akiwa Chuo cha ualimu.

Jamaa akihangaika kusaidia kulipa ada na mwanamke kuamua kumbambikia mumewe mimba na baada ya mtoto kuanza kukua ndipo tetesi za kutokuwa mwanaye zilipoanza na kupelekea mzozo kati yao na baadae familia za pande mbili kuingilia kati na kuwaweka sawa na maisha yakaendelea.

Kwa maelezo ya wapangaji wenzao ni kwamba Jumamosi jioni kulitokea kupishana kauli kati ya mme na mke.

Usiku mke alimvizia mme akiwa amelala na kumpiga na kitu kizito kichwani na kupoteza maisha baada ya hapo mwanamke alipiga kelele kuomba msaada kwamba amempiga mme wake lakini hakujua kama atakufa.

Baada ya taratibu za kipolisi tulimuaga marehemu Jana kwao maeneo ya Tegeta kwa Ndevu ambapo mimi pia nilihidhurua kwakuwa baadhi ya ndugu wa mwanaume tunafahamiana.

Inasikitisha kuona mapenzi sasa yanaendelea kuondoa uhai wa watu, mpaka sasa mwanamke anashikiliwa na vyombo vya dola wakati mazishi yanatarajiwa kufanyika huko Kasulu.
 
Back
Top Bottom