TECNO yadhamiria kusogeza huduma zake karibu na wananchi

TECNO Tanzania

Senior Member
Jul 6, 2016
192
216
Kampuni ya simu za mkononi TECNO imezindua duka kubwa la simu, maarufu ‘Smarthub’ Mtaa wa Mwenge jijini Arush, duka ambalo linatoa huduma mbalimbali ikiwa ni hatua muhimu katika kusogeza huduma kwawananchi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa duka hilo mwishoni mwa wiki, Afisa Utamaduni Jiji la Arusha Bw. Benjamin Maneno ambaye pia alimwakilisha Mkurugenzi wa Jiji kama mgeni rasmi, alisema;

“Kwa karne tuliyofikia hivi sasa, matumizi ya smartphone hayaepukiki, kwahiyo tunachoomba sasa wananchi waje kwenye maduka ya TECNO kwaajili ya kupata fursa ya kupata vipato kupitia simu za TECNO, sio kutumia kuchati tu lakini unapotumia intaneti kwenye simu za TECNO unaweza kufanya biashara na hata kupata masomo”

Unnamed QQ Screenshot20200224150052.png

Afisa Michezo na Utamaduni Jiji la Arusha Benjamin Maneno ambaye alimwakilisha Mkurugenzi Jiji la Arusha kama mgeni rasmi akiweka sahihi yake katika bango maalum lililokuwa limeandaliwa na TECNO.

Unnamed QQ Screenshot20200224150803.png

Pichani ni Bw. Benjamin Maneno Afisa Michezo na Utamaduni Jiji la Arusha ambaye alimwakilisha Mkurugenzi Jiji la Arusha kama mgeni rasmi akipiga makofi mara baada ya kukata utepe kuashiria uzinduzi wa duka la kisasa la TECNO.Wengine ni Diwani Jiji la Arusha Mh. Walence Kinabo (Kushoto), Mhasibu Mapato Jiji la Arusha.

Kwa upande wake Msimamizi wa Mauzo kanda ya Kaskazini Bw. Kassim Haji alisema,

“Tunawakaribisha wateja wa mikoa ya karibu katika Duka hili jipya la TECNO “Smart Hub”, Kuna faida nyingi ambazo wateja watanufaika nazo ikiwemo huduma ya kupata fursa ya kununua bidhaa zetu za simu kwa bei nafuu, vifaa vya simu, kupewa elimu ya bure kuhusiana na matumizi, sifa na mifumo ya simu, vilevile kwa mteja atakayenunua simu katika msimu huu wa Valentine, ataingia kwenye droo ya kujishindia friji kubwa”

Unnamed QQ.png

Msimamizi wa Mauzo kanda ya Kaskazini Bw. Kassim Haji akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya tukio la uzinduzi wa duka la TECNO.

Uzinduzi huo uliohudhuriwa na viongozi wa serikali pamoja na wadau mbalimbali wa TECNO uliambatana na burudani huku diwani wa Jiji la Arusha Mh. Walence Kinabo akipendekeza mambo mbalimbali yanayohusu kupotea kwa simu.

“Leo tunawashukuru sana uongozi mzima wa TECNO kwa kujali mahitaji ya wananchi wa jiji la Arusha kuamua kufungua duka jipya la kisasa. Uongozi mzima wa TECNO wajaribu kuwafundisha wananchi wanapokuja kununua simu mambo ya msingi wanayoweza kuhifadhi ili baadaye simu ikipotea waweze kui-track” Alisema Mh. Kinabo.

TECNO imedhamiria kupanua wigo wa huduma zake na kuzisogeza karibu na wateja wake kwa kufungua maduka makubwa ya kisasa yenye huduma zote ambapo wateja hawatatumia muda mrefu kupata huduma hizo.

Hata hivyo TECNO tayari imeshaweka maduka makubwa katika majiji yote makubwa Tanzania ikiwemo, Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza na Mbeya.

Unnamed QQ Screenshot20200224150430.png

Mhudumu wa Duka Jipya la TECNO Lililopo mtaa wa Mwenge jijini Arusha akiwaelekeza wateja mifumo ya simu za TECNO hivi karibuni.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom