Tecno ni halisi, ni orijino na kamwe haziwezi kuwa bandia

Hivi kweli unategemea asilimia 80 ya watanzania wanaoishi vijijini watumie Samsung Galaxy or the like? Waweza pia kutusaidia watanzania wenzako hizo athari za kiafya ni zipi?
Hivi kwa nini watu wakisikia jina la galaxy wanaingiwa na woga wa bei? Galaxy ziko nyingi, ila pia si lazima ununue galaxy. Zipo simu nyingine.
Kabla hamjanunua TECNO zenu fanyeni kwanza window shopping, kuna simu nzuri zaidi ya hizo TECNO mnazonunua na zinauzwa bei nafuu zaidi ya hizo TECNO mnazonunua.
 
Labda utusaidie wewe kwa nini mnasema tecno ni hatari kwa Afya zetu?
 
Labda utusaidie wewe kwa nini mnasema tecno ni hatari kwa Afya zetu?
Sijazungumzia suala la afya, hilo sina utaalam nalo. Ila ubora wa TECNO ndio hafifu. Na ndio maana soko lao ni Afrika tu. Kampuni ya CHINA lakini hata huko CHINA kwenyewe hawauzi simu zao.
 
Sijazungumzia suala la afya, hilo sina utaalam nalo. Ila ubora wa TECNO ndio hafifu. Na ndio maana soko lao ni Afrika tu. Kampuni ya CHINA lakini hata huko CHINA kwenyewe hawauzi simu zao.
Okay, nilitaka kujua kama inaweza kunieleza madhara ya kiafya tunayopata kwa kutumia Simu za tecno. Hilo ndio suala la msingi zaidi. Kuhusu ubora sipingani na hilo kwa kuwa sina ushahidi. Siwezi kusema zina ubora mdogo kwa sababu zinauzwa Africa pekee.
 
Hivi kweli unategemea asilimia 80 ya watanzania wanaoishi vijijini watumie Samsung Galaxy or the like? Waweza pia kutusaidia watanzania wenzako hizo athari za kiafya ni zipi?
Hivi mkuu ulishafanya uchunguzi wa bei za simu? Mbona simu zipo nzur nying tu tena ni affordable, tecno phanton 5 inauzwa laki 8 wakati ni simu ya kiboya kwa lg g2 ambayo unapata around 300 hadi 350 tu
 
Kuna jamaa ana samsung j7 duh hii simu imenifanya niziogope samsung ukiangalia spec...na jinsi inavyofanya kazi utachoka ipo too slow, ina pata moto, inatumia chaj balaa halafu storage ni 16Gb na memory 16gb lkn baada ya muda inagoma kudawnload inaleta pop up kuwa low storage.
Yani jamaa akija nayo nimuelekeze baadhi ya mambo hadi na choka mwenyewe nimesha zoea tecno c8 yangu mambo ni fasta fasta, chaji ya uhakika, haijawahi pata moto hata ikiwa na matumuzi makubwa.
Yani hadi naiogopa hiyo simu isijenifia mikononi na bado ni mpya.
inawezekana ikawa ni fault device airudishe samsung, j7 ni kati ya simu zinazokaa sana na charge (angalia table ya gsmarena) pia hizi j series zinatumia touchwiz mpya ambayo ipo very fast na ni nyepesi ni touchwiz hio hio iliotumika kwenye note 5 na high end device za samsung, na hio storage umeikagua kuwa ni ndogo?
 
Mmh tcra wameitambua tecno yangu
ca32fe9d352014e77104452b92f316d4.jpg
 
Tecno simu nzuri tu hata kama hazina ubora wa Samsung na nyinginezo, pia zinawasaidia sana watanzania japo wale wanaotumia high end devices wanaponda kila siku na kuzusha maneno without any evidence.
Na pia inasikitisha watu kureview simu za tecno kimtazamo tu bila kufanya research ya kutosha
dah nyie jamaa nawapigia salute kwa kutoelewa, narudia tena tecno hawana advantage ya bei ni fikra tu za watu kuwa simu zao ni za bei rahisi ila katika kila price point zipo simu za bei nzuri zaidi na zinazotoa kilicho bora zaidi na mifano hii nimetoa
-lg g2 inadestroy tecno yoyote ile kuwahi kupata kutokea na bei ni around laki 3 ina maana ukinunua tecno yoyote kwa zaidi ya laki 3 umenunua bidhaa dhaifu
-simu za snapdragon 410 zina power kushinda low end yoyote ile ya tecno, angalia hapa zimejaa kibao
Phone Finder results - GSMArena.com
sehemu pekee ambayo kidogo Tecno ina make sense ni simu za sub 100,000 lakini na huko pia ni bora ununue simu za voda/airtel/tigo ambazo zinauzwa rahisi.
 
mkuu hio + mbele ya lg g3 unamaanisha simu nyengine? hapo mimi naona s5 ndio nzuri imebalance,
Thanks kaka. Kuna simu niliona kapost mad Ice akasema hio shot kachukua na lg g3 plus. So nikaitafta ila nikawa napata lg g3 alone.
Nashukuru. Kuna jamaa anauza s5 kwa 400k ngoja nimtafte mwisho wa mwezi huu
 
Ameweka Link inayoelezea madhara ya mionzi ya Simu. Katika taarifa hio imeonesha kwamba Simu zote zina mionzi. Wameelezea pia namna head set zisivyosaidia kupunguza mionzi. Labda wataalamu watueleze tofauti ya mionzi ya Simu za tecno na mionzi ya Simu nyingine kama Samsung nk. Tusaidieni tafadhari kama kuna researchers ambao tayari wametoa report kwamba tecno ni hatari kwa Afya zetu.
issue si kwamba tecno ina madhara issue ni kwamba hazijapimwa. yani ni kama unafanya mapenzi na mtu ambae humjui afya yake anaweza kua ameathirika au hajaathirika hivyo ni risk. na lawama si za tecno ni za serikali yetu wao ndio walitakiwa wazipime na kutoa majibu ili tujue. hivyo ni juu yako wewe mtumiaji kama unaamua kutake risk au kutafuta simu salama.
 
Kati ya lg g3+ na s5 na note3 samsung unashauri mtu achukue ipi Kati ya hizo?
Tatizo betri za simu za hayo makampuni hazitunzi charge inavyotakikana.
Sioni umuhimu wa kuwa na simu ambayo haiwezi kutunza charge nkafanya non-stop usage throughout the day.
Kwa wale wa kupiga na kukata labda zitwafaa hizo brand...Haya ni maoni yangu kama mtumiaji wa kikwelii wa smartphone.
 
So wewe hutumia brand ipi?
 
Sawa mkuu, ila nina jambo moja tu la kukukumbusha, kuishi katika nyumba ya udongo ama ghorofani ni jambo la hiari na haimaanishi wote wanaoishi kwenye nyumba za udongo hawana uwezo wa kujenga ghorofa.
Hivyo kitu ambacho nakiona sana ni ile hali ya nyie kudharau na kuongea shit juu ya tecno kana kwamba haziserve purpose kama hizo high-end brands. Mimi sio shabiki ila naongea kama smartphone enthusiast hivyo sina bias. Wanaotumia tecno waposatisfied in the same way kama watumiaji wa samsung,sony or lg.
Nashangaaga sana mnapoobgelea hayo maswala ya socket sijui chipset. Hivi yanaathiri vipi basic functions za simu???, at least ram na battery na camera labda ila msiongelee maswala ya socket, sijui chipset.
Sijaona mantiki yako.

By the way, huhitaji kua na akili sana kujua kua nyumba ya udongo na gorofa zote ni nyumba na zinasaidia kutimiza hitaji moja la kulala au kuishi ila inapokuja suala ya ubora gorofa haiwezi kulingana na nyumba ya udongo.

Tatizo tecno fans mnaziwa nyumba ya udongo kwa bei karibu au zaidi ya gorofa alafu mnalazimisha kulinganisha nyumba zenu za udongo na magorofa kisa mlinunua kwa bei ya gorofa.

Ndio maana nikasema tecno fans wana dogmatic personality, unawambia 1 jumlisha 1 ni 2 na unampa ushahidi ila yeye hataki ushahidi na anaukataa kwa makusidi.

Labda nikupe mfano mwingine kwa fauda yako, passo au vits ni chombo cha usafiri kama vogue au range rover, zote dhumuni lake ni usafiri, lakini hazifanani bei na hata ubora, makighafi na utaalam uliotumika kutengeneza vogue ni wa juu zaidi kuliko vits, lakini ukishikwa masikio na wajanja mjini ukauziwa vits kwa bei ya range rover basi usikomae kulazimisha kua vits yako ni sawa na range rover.
 
dah nyie jamaa nawapigia salute kwa kutoelewa, narudia tena tecno hawana advantage ya bei ni fikra tu za watu kuwa simu zao ni za bei rahisi ila katika kila price point zipo simu za bei nzuri zaidi na zinazotoa kilicho bora zaidi na mifano hii nimetoa
-lg g2 inadestroy tecno yoyote ile kuwahi kupata kutokea na bei ni around laki 3 ina maana ukinunua tecno yoyote kwa zaidi ya laki 3 umenunua bidhaa dhaifu
-simu za snapdragon 410 zina power kushinda low end yoyote ile ya tecno, angalia hapa zimejaa kibao
Phone Finder results - GSMArena.com
sehemu pekee ambayo kidogo Tecno ina make sense ni simu za sub 100,000 lakini na huko pia ni bora ununue simu za voda/airtel/tigo ambazo zinauzwa rahisi.
Mbona mi sijazungumzia bei hapo, vp chief? By the way maoni yangu ni mtazamo wangu tu... Unaeza kuwa na moani tofauti
 
Mbona mi sijazungumzia bei hapo, vp chief? By the way maoni yangu ni mtazamo wangu tu... Unaeza kuwa na moani tofauti
umesema highend wanawaponda tecno post yangu ni kukwambia sio highend tu hao wasio afford hizo highend kwenye budget zao ndogo wanapata simu nzuri kwa hela zao
 
Kaika cm zinazoongoza kwa mafundi tecno ni namba moja..
Kaka tecno ziko nyingi kwa mafundi au wanaoomba msaada humu wengi hutumia hizi brand za tecno. Kitu ambacho mimi nakijua sio kwa sababu tecno ni mbovu kwa kiwango hicho ila ni majority ya watanzania ndio wanaotumia tecno. Kipindi ambacho tecno hawaja anza kutuuzia simu zao nokia ndio zilikuwa nyingi kwa mafundi simu kuliko Samsung, lg sony nk. Kwa uchache wao tunawaona watumiaji wa brand nyingine nao wakienda kwa mafundi simu. Ni hesabu tu za asilimia.
 
umesema highend wanawaponda tecno post yangu ni kukwambia sio highend tu hao wasio afford hizo highend kwenye budget zao ndogo wanapata simu nzuri kwa hela zao
Kaka kuna mtu anataka kuniuzia Samsung Grand prime , SM~G531F ambao ni Duos kutoka India, Pls unaweza kuniambia ni bora kiasi gani? Samahan kwa usumbufu.

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom