Huwezi kuwako kwenye serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar mkaongoza wote kutekeleza ILANI ya CCM ya Uchaguzi halafu ukaja kwenye Bunge la muungano ukapinga. Kwa hiyo "technically" CUF sio upinzani. CCM na CUF "dugu" moja.
What is your say ?
CUF walitaka CHADEMA wamwachie Hamad Rashid kipindi kingine cha miaka mitano, kwani ndio utamaduni wa uongozi Tanzania walivyochomoa na wao wakaamua kususa.
CUF walitaka CHADEMA wamwachie Hamad Rashid kipindi kingine cha miaka mitano, kwani ndio utamaduni wa uongozi Tanzania walivyochomoa na wao wakaamua kususa.
Soma Kanuni za Bunge hapa chini
14.-(1) Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni atachaguliwa
chini ya utaratibu ulioainishwa kwenye fasili za Kanuni hii
zinazofuata.
(2) Wabunge wote wa Upinzani wanaweza kuunda Kambi Rasmi
ya Upinzani iwapo idadi yao itakuwa si chini ya asilimia kumi na
mbili na nusu ya Wabunge wote.
(3) Chama cha Upinzani hakitakuwa na haki ya kuchagua
Kiongozi wa Upinzani Bungeni, isipokuwa tu kama kina idadi ya
Wabunge wasiopungua asilimia kumi na mbili na nusu ya Wabunge
wote.
(4) Endapo kutakuwa na Vyama vya Upinzani zaidi ya kimoja
ambavyo kila kimoja kina Wabunge asilimia kumi na mbili na nusu
au zaidi, basi Chama chenye idadi kubwa zaidi ya Wabunge kuliko
vingine ndicho kitakuwa na haki ya kuchagua Kiongozi wa Kambi
Rasmi ya Upinzani Bungeni, lakini, ikiwa kutakuwa na vyama viwili
au zaidi vyenye idadi sawa ya Wabunge ambao ni zaidi ya asilimia
kumi na mbili na nusu, Wabunge wa vyama vinavyohusika
watachagua Kiongozi wa Upinzani Bungeni chini ya utaratibu
watakaokubaliana wenyewe.
15.-(1) Chama chenye haki ya kumchagua Kiongozi wa Kambi Rasmi
ya Upinzani Bungeni kinaweza pia kuchagua Naibu Kiongozi wa
Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni.
(2) Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni atateua
Wabunge wa Chama chake au Wabunge wa Kambi Rasmi ya
Upinzani Bungeni ambao watakuwa wasemaji wakuu wa Kambi ya
Upinzani kwa Wizara zilizopo za Serikali.
16.-(1) Chama kinachounda Serikali na Chama chenye haki yaUteuzi
kuchagua Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, vitateua
Wanadhimu wa vyama hivyo Bungeni ambao watajulikana kwa
jina la Mnadhimu wa Serikali na Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya
Upinzani Bungeni.
(2) Vyama hivyo vitateua pia Wanadhimu Wasaidizi ambao idadi
yao itaamuliwa na vyama vyenyewe.
unahakika unachosema???
popote pale duniani mwenykt wa upinzani ni lazma atoke chama kikuu cha upinzani>>
CUF siku zoote ni waroo wa madaraka wanataka madraka uwezo hawana...
tokea tumeanza mfumo wa vyama vini wao wagobea wale wale wakati wengine huwa wanabadilisha ... wasipoangalia 2010 watapata nusu ya kura walizopat
Ulitaka cuf wafanyeje?wasusie mseto?kwa mtu yeyote anayefahamu hata punje tu ya historia ya zenj tangu 1963 hawezi kubeza hatua iliyofikiwa.hoja ya msingi ni namna gani mseto utahifadhi siasa za ushindani kama ilivyo kwenye baadhi ya nchi zilizopiga hatua kama ujeruman.hii haina uhusiano na vita ya kuongoza kambi ya upinzan ktk bunge la jamhuri ya muungano.logicaly,chadema wanayo haki ya kuunda kambi hiyo peke yao au kushirikisha wenzao.history is a good teacher.mwaka 2005,cuf waliunda kambi ya upinzan peke yao kabla ya kuona mantiki ya kuwashirikisha wenzao baadaye.kama sikosei,dk slaa akawa msaidizi wa hamad rashid
Naona una hasira (hiyo red sio 2015 kweli?)