Kanisa Katoliki lapoteza Mapadri 25 na Watawa 60 kwa tatizo la upumuaji ndani ya miezi miwili

Aanze kiongozi wa kiroho aliyemkana Mungu hadharani kwakuiita imani ushirikina na science mkombozi
Amesema Mungu si hirizi! Yes! Only hirizi ndio kitu ambacho unakitumainia bila kuhitaji akili! Mungu katuumba na akili,nafsi huru si kwaajili ya mapambo alafu yeye atawale! Pale pa kutumia akili huhitaji Mungu! Ukisikia mkojo unahitaji Mungu? Sasa tunajua kinachoendelea na kusumbua dunia nzima! Kwanini tusiseme ukweli ili jamii ijichunge?

Science ni kiwakilishi cha akili na hizi akili hukupewa kwendea chooni tu. Sala lazima iende na matendo! Ukikutana na Simba utasali ukikimbia, ukijifanya unakemea utatafunwa ndugu!
 
Amesema Mungu si hirizi! Yes! Only hirizi ndio kitu ambacho unakitumainia bila kuhitaji akili! Mungu katuumba na akili,nafsi huru si kwaajili ya mapambo alafu yeye atawale! ..
Walianza lini kuamini science? Walivyo nyonga wana science wakati huo huyo Mungu alikuwa hirizi?

Science inaamini kuhusu Mungu? Can light and darkness co-exist?

Wameiacha theolojia madhabahuni wapo busy kupiga siasa, pathetic!
 
Hao mapadri huwa wanafanya mazoezi au ni kukaa tu ndani wakidhani ndio njia sahihi ya afya zao?

Zaidi ya hapo kanisa limepungukiwa upako, nadhani mapadri na watawa wa siku hizi wengine wana madhambi mengi saana hivyo wanapaswa kutubu na kumrudia mungu.

Wakati mungu anawambia wana wa islaeri watazame fimbo ya musa na waliokaidi kwa kuona wanaweza kujiokoa wenyeqwe walikufa na upuuzi wao.

Tulifundishwa dini kuwa ni heli kufa ukimtumaini mungu sasa kitima anatwambia nini kuhusu hili

Na kama ndivyo basi father kitima asitwambie kwenda kanisani ili tuanze kuiabudu sayansi kwa maana hata matokeo yake unaweza kuyaona kuliko historia ya mungu ambaye hatujawahi kumuona lakini father anatuaminisha kisha yeye mwenyewe haamini katika hilo.
Swali langu kwa father popote alipo, je kama maji ya baraka yanauwezo wa kumfukuza shetani kama tuanvyofundihswa.
Je tunaweza kuyatumia kufukuza corona?

Na kama hayawezi basi anatushauli tumtumie mungu kumfukuza shetani tu kwa kuwa ndo anauwezo nae?

Na mambo mengine ambayo hayamuhusu shetani basi tusiyaombe kanisani tena kwa mungu bali tutumie akiri zetu kuyatatua?
 
Imani hanb
Amesema Mungu si hirizi! Yes! Only hirizi ndio kitu ambacho unakitumainia bila kuhitaji akili! Mungu katuumba na akili,nafsi huru si kwaajili ya mapambo alafu yeye atawale! P
Imani haba, watu wanasali tu lakini hawana imani ya kiroho,

Kama ndivyo basi yule aliyetupwa kwenye shimo la simba basi angeliwa mara moja.

Mapadri na watawa baadhi wanalinajisi kanisa.

Huko wengine wnafanya ngono na wengine wanaharibu vijana wetu. Sasa hapo mungu atakaa nao?
 
Huenda kuna vitu nyuma hatuvijui pia.hii corona ya pili inaonekana kabisa ineletwa na mawakala kuondoa watu flani public figure Ili vaccine zao zipitishwe
 
Kwa hiyo wewe unavyoona rate ya vifo kule marekani ni sawa na ya hapa kwetu?

Kifo hakifichiki, siyo kwamba hakuna waliokufa, wapo ila si kwa wingi mnaotka kutuaminisha
Ngoja nkuambie ki2 marekani kwenyewe usidhani kila sehemu wanasikia vifo kama unavojua wewe. Zile takwimu hutolewa na wataalam wa afya na wengne wanasikia kweny vyombo vya habari kama wewe. Come to your senses man.

Ngoj nkupe ratio kwa idadi ya wamarekani waliokufa ratio yake ni sawa wafe wabongo 83,000 tangu janga lianze. Sasa nkuulize swali katika nchi ya watu million 60 wakifa hyo idadi we na takwimu zikafichwa unaeza gundua namba?

Sent from my SM-J111F using JamiiForums mobile app
 
Biblia inatamka wazi kuwa hukumu itaanzia nyumba ya Mungu sababu haimpi utukufu Mungu sasa hivi kwenye Corona wanasayansi ndio wanapewa utukufu na maaskofu masista wachungaji na mapadre tujiandae kuzika wengi zaidi ya hao kuanzia maaskofu mapadre wachungaji masista nk hawa waliokufa cha mtoto .Narudia hukumu ya Mungu imeanza kanisani.Yeyote asiyekiri Mungu Kuwa Bwana na Mwokozi kwenye Corona ajiandae kuondoka na Corona.Watengeneze mambo yao saa yeyote wanaondoka
Jamani hivi tanzania Mungu mnaemwimba ni yupi? Mbona kwenye maandiko hatumuoni? Hivi wewe unajiona mtakatifu sana ndo maan Mungu kakuacha hai kawaua masista kwasababu wana dhambi?

Duu inatilia mashaka usomaji wenu wa maandiko. Hujui hata purpose ya Yesu duniani ilikuwa nn aisee afu unatoa hukumu kwa wenzio ambao ni binadamu kama wewe?

Sent from my SM-J111F using JamiiForums mobile app
 
Masista na mapadre hawachanganyiki sana na watu watakuwa Corona wanapeana wenyewe sababu wai huenda sana Roma italia kwa papa...
Si kweli. Masista wengine ni wakunga au madaktari hivyo wanakutana na waathirika moja kwa moja. Mapadre kwa masistavhukutana na waumini katika ibada na shughuli nyingine.
 
Huyo petro wenu yupi wa Waafrika au wa wazungu?
Nyote mnaojifanya sijui petro,yesu'n.k mtakiona cha moto kwani Mwenyezi Mungu hajaribiwi....
Nyinyi wa mila mmetufelisha mambo mengi sana zamu ya Yesu sahivi. Hamjui chochote maisha ya mwanadamu bali tunguli tu. Ny nd mmesababisha africa ibaki nyuma kimaendeleo em tuacheni kidogo tupate pumziko la milele. Huku tunaambiwa njooni enyi nyote mnaolemewa na mizigo na nitawapumzisha.

Nyny mnatuambi shangazi yako anakuroga. Saa hivi tunajua tukifa tunaenda wapi nyny mlishindwa kutupa hicho kitu. Mlishindwa kutufundisha kujali wenzetu kama maandiko yasemavyo usiibe usiue usizini usimsemee jirani yako uongo usitamani mali ya mwenzio. Mlitufundisha uchafu wa mwili na akili mlitufanya tukae mbali na Mungu.

Sasa tumepata upendeleo kwahiyo mtuache tu.
 
Shetani akapewa nafasi ya kuwarubuni watu wa Mungu leo ni kilio na kusaga meno! Uongo ukatamalaki, taifa likahadaiwa - HAKUNA CORONA! Yamfaa mpotoshaji yule afungiwe jiwe la kusaga na kutupwa baharini sio kwa upotoshaji ule tena madhabahuni!..
Watu wanahisi kwasababu bible haijajikita sna kweny historia ya mwili bali imani basi wanahisi zamani walikuwa maroboti ya Mungu hawaugui wala hawana dawa.

Mungu kaweka dawa kwenye miti why is that? Kwann watu wake wanaenda hospital na wanapona? Mungu aliposema kuwa ukiwa na imani ndogo kama chembe ya haladari (kama sikosei neno) utaamisha mlima doesn't mean umuombe ahamishe mlima kweli bila sababu kwasababu atakuona mpumbavu uliopofuka.

Sijui kama tunamkosea kwahili tunaomba tusamehewe atujaze imani na amani kati yetu.
 
Akafunge makanisa yao akuna anaye mzuia,mtumishi gani aamini nguvu za Mungu,eti Mungu si hirizi.Magonjwa hayo yalikukuwapo hata enzi Musa lakini Mungu alimwambia Musa achonge nyoka wa shaba atakaye mwangalia ndie atayepona (soma Hesabu 21:4-9) mtumishi gani anaogopa kifo...
Mifano miwili tofauti. Unajua kwann waliletewa yule nyoka? Afu usichanganye mambo bible inajenga imani hasa hasa kwasababu tumeumbwa na akili mambo mengine Mungu atatuongoza tukiwa na imani. Swali kwako.

Je, ni kwanini mtume Paulo alimtumia waraka Tito kuwa atumie mvinyo kumponya maradhi yanasumbua. Kwann Mungu kaumba chakula kiupe mwili upambane na Magonjwa?
 
Hapo ndio umuhimu wa uislam unapokuwepo Mara tano kila siku kunawa mikono mbona mashehe cjasikia
Duuuu! Kwani serikalini umesikia? Maalim Seif Hamad Vipi au alihasi uislamu? Yani waislamu wengne na nyny ni tatizo kujumlisha jumlisha watu. Wale masheikh walioambukizwa saudia mmewazidi imani? Je, vipi saidia kutumia chanjo ya uviko-19 ? Ny waislamu wengne nahisi dini yenu yenyewe pia hamjailewa mnaenda hata kinyume nayo.
 
Hao mapadri na masista waliofariki ni kwa sababu mbali mbali ikiwemo changamoto ya upumuaji (Na si kila changamoto ya upumuaji ni corona). Halafu ni Takwimu ya Tanzania nzima kwa miezi miwili!! Si kwa siku moja au wiki moja kwa jimbo moja!..
Kwa hyo unachukua nafasi ya malaika kuthibitisha kuwa tanzania wanasali sana kuliko mataifa yote duniani? Ok! Twende. Bible inasema yeyote ajikwezae atashushwa na ajishushae atainuliwa. Je kwann nyny mnajikweza namna hyo?

Ujue Tanzania nchi inachekesha sana kama nyny kweli mna imani kiasi hicho msingekuwa blinded na media za marekani ambazo mara nyngi zinaonesha content za kidunia. Mungu angewaonesha wenzenu wa mataifa mengne yenye imani. Halafu Mungu hahusiki na geo location zenu mlizogawiana berlin out of sin za ukandamizaji wa baadhi y mataifa makubwa.

Taifa la kweli la Mungu liko ndani ya nyoyo za watu nd maan sio kila myahudi alimpokea Yesu jpo lilikuwa taifa teule sembuse nyny wabongo.
 
Wala hazitishi japo baadhi ya watu wangependa kulazimisha zionekane kuwa zinatisha!!
Kwanza kifo si kigeni kwenye kila jamii ya watanzania ikiwemo jamii ya mapadri na masista! Tena kwa sababu mbalimbali ikiwemo tatizo la upumuaji hata kabla ya corona!!
Padre kasema walikuwa wanakufa wa5 wa4 wa2 m1 au non katika range ya huo muda. Kwahyo ukikuta imefika 87 lazima ushtuke. Halafu kwann mwenzio afe kwamba ye nd ana dhambi sana? Kila mtu ana haki ya kuishi.
 
Je unataka kusema kuwa sisi hapa Tanzania hatujapambana? Au unataka mpaka tufanye copy and paste kama wanavyofanya mataifa mengine bila kuangalia hali halisi ya mazingira yetu?...
Biblia inasemaje kuhusu imani na matendo? Je kweli kama taifa mnatenda bora kuliko mataifa mengine nd mkaponywa? Je hamzini, hamuibi? hamuui? hamsemi uongo ? Je mnaheshimu baba na mama?

Je, hamtamani maliza wenzenu? Je mnaabudu Mungu wa kweli pasi miungu mingine? Na mengineyo collectivelly as nation kama mnavosema.

Hawa vijana waosifia misambwanda kila siku wako kategory gan? Wanaoabudu pesa je? Wezi? Imani ni swala la moyoni zaidi kuliko la ujumla. Yesu akiwa kwenye mkutano wa hadhara akafwatwa mwalimu mam n ndugu zako wanatak kukuona. Jibu lilikuwa mama yangu na ndugu zangu ni wale tu wanaoshika neno langu (kumbuk hawa ni ndugu wa damu kabisa.
 
Marekani wamekufa, Italia wamekufa, wazungu wengi wamekufa na wanaendelea kufa. Hawa ndiyo wataalamu na wanasayansi wa dunia, wanajua kujihami kuliko sisi, na watu makini na wenye maendeleo kuliko sisi...
Takwimu zinaonesha kama wasingechukua hatua walizochukua vifo vingekuwa mara 10 zaidi ya hivyo, hatua walizochukua wamepunguza idadi ya vifo wala sio kumaliza ugonjwa, na sisi kama tungechukua hatua kama hizo idadi ya vifo ingekuwa ndogo sana
 
Hatukuwahi kushinda wimbi lolote ilikuwa ni ghiriba ya shetani tu, tokea Corona iingie haikuwahi kutoka hadi leo hii ililazimishwa na mtu pale alipowaita watendaji wa serikali na kuwapiga stop wasitoe takwimu na kuwatangazia wananchi wafanye maombi baada ya hapo tukatangaziwa Corona imekwisha yaani tulifanywa wajinga au kama watoto wadogo lakini cha ajabu kuna wapumbavu wachache waliamini ule ujinga.
Kama sisi ni mabingwa wa dua na maombi ebu tufanye hivyo ili siku tukiamka tukute mabarabara yote yameshapigwa lami.
Unamkufuru Mungu, wala huna shukrani. Unaukataa hadharani uponyaji wa Mungu dhidi ya korona kwa Taifa letu. Kwa kufanya hivyo unaiita laana ya corona katika maisha yako nanyumba yako mwenyewe!! Usije kutafuta mchawi utakapoona corona inakutafuna.
 
Mapadre25 watawa 60 so tuliambiwa corona Inauwa Wanaume zaidi au hii ya South Africa imegeuza kibao
Poleni sana wale wote mliopoteza Ndugu na jamaa na marafiki
 
Hatukuwahi kushinda wimbi lolote ilikuwa ni ghiriba ya shetani tu, tokea Corona iingie haikuwahi kutoka hadi leo hii ililazimishwa na mtu pale alipowaita watendaji wa serikali na kuwapiga stop wasitoe takwimu na kuwatangazia wananchi wafanye maombi baada ya hapo tukatangaziwa Corona imekwisha yaani tulifanywa wajinga au kama watoto wadogo lakini cha ajabu kuna wapumbavu wachache waliamini ule ujinga.
Kama sisi ni mabingwa wa dua na maombi ebu tufanye hivyo ili siku tukiamka tukute mabarabara yote yameshapigwa lami.
Ukweli kuwa bado upo hai ni ushahidi tosha kuwa Mungu alisikia maombi yetu na kutuponya na corona! Hivi wewe ulijikinga na corona kumzidi waziri mkuu wa Uingereza au aliyekuwa Rais wa Marekani?

Wote hao waliugua na baadhi yao walikaribia kufa! Wewe u mzima wa afya. Afya yako aliyokupa Mungu usiitumie kumkufuru Mungu kwa kukataa hadharani yale ambayo Mungu ametufanyia watanzania ukiwemo wewe!

Nakusihi kwa rehema za Mungu utubie uovu huu ambao mwisho wake umelenga kukuangamiza!! Unathubutuje kumkejeli akupaye pumzi ya uhai kola sekunde.

Mambo ya ujeuri kama haya ukiyaendekeza unaweza kujikuta unaokota makopo barabarani, uwe mwangalifu!
 
Ametueleza kuwa corona ipo na inaua. Sijajua sijui mtanzania gani hajui Kama corona ipo. Hata huku shamba tunajua.

Ametueleza Mapadri 25 na Watawa 60 wamekufa kwa corona ndani ya siku 60. Ninadhani ameisaidia Serikali kupata data ijapo sijajua Kama Mapadri wako juu ya sheria ya Takwimu. Ninadhani si sahihi kwake kama muumini anayesimamia haki. Ninadhani aisaidie serikali kupata majina na mahali walipofia hao ndugu ili serikali iweke kwenye kumbukumbu.

Kituko cha huyu Katibu kilichonifanya nihisi Kama anatumika kuleta taharuki ni pale kuonyesha kuwa wao wanajikinga. Lakini yupo kwenye camera hana Barakoa wala sanitizer. Lakini anatumia mike ambazo hata hajui zimetoka wapi. Nimejiuliza hivi yupo serious kwenye vita hii au naye anaigiza ili mradi tu wanaotoa misaada huko waseme kasema? Ninadhani ili kuonyesha u serious tungemuona yeye mwenyewe kavaa barakoa, Ana special mike n.k Lakini kwa mtiririko ninaona ni maigizo kutumia vifo kujinufaisha.

Na kuhusu kinga wanashindwa kututhibitishia kisayansi kuwa huko wanakopewa hizo chanjo vifo vimeisha au vimepungua? Kama bado wanakufa sisi chanjo inatusaidia nini? Uganda wapo lockdown toka mwaka jana wameokoa nini zaidi ya kujitengenezea umasikini?

Tuendelee kuchukua tahadhari za kujilinda na korona, tuache kutishishiana na kuleteana woga. Mungu atatuvusha hata Kama wachungaji wata surrender. Madam Rais alishasema hakuna lockdown Mapadri hawana uwezo wa kutu lockdown. Wakati wa kufa ukifika tutakufa, Lakini ha tutakufa kinyonge, tutakufa tungali tunapambana na kazi za kusaka mkate wa kila siku.

Huwezi kutufundisha kujikinga na corona wakati wewe mwenyewe umeshindwa kuonyesha demonstration kwenye press. Huna Barakoa, huna sanitizer na unatumia mike ambazo hujui zimetoka wapi, ni UHUNI.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Back
Top Bottom