Papaa Mobimba
JF-Expert Member
- Jan 27, 2018
- 752
- 3,092
Katibu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, Padri Charles Kitima amesema kuwa ndani ya miezi miwili iliyopita zaidi ya mapadri 25, masista na manesi 60 na wenyeviti wawili wa Baraza la Walei wamefariki dunia kwa sababu mbalimbali ikiwemo changamoto ya upumuaji.
Ameongeza kuwa vifo vinaendelea na kuwataka Watanzania kuendelea kuchukua tahadhari na kuacha mzaha katika katika suala zima la Corona.
Huyu Mungu si hirizi, anataka kila binadamu awajibike na atumie uwezo wake kufikiri. Corona ipo, unaambiwa chukua tahadhari unasema mimi nasali. Mungu wetu anataka watu wawajibike, si kusema tu, tunasali - Ameongeza Padri Charles Kitima