TEC: Ndani ya miezi 2, zaidi ya mapadri 25, Watawa 60 wamefariki kwa tatizo la kupumua. Huyu Mungu si hirizi, anataka kila binadamu kuwajibika

Papaa Mobimba

JF-Expert Member
Jan 27, 2018
639
1,000
Katibu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, Padri Charles Kitima amesema kuwa ndani ya miezi miwili iliyopita zaidi ya mapadri 25, masista na manesi 60 na wenyeviti wawili wa Baraza la Walei wamefariki dunia kwa sababu mbalimbali ikiwemo changamoto ya upumuaji.

Ameongeza kuwa vifo vinaendelea na kuwataka Watanzania kuendelea kuchukua tahadhari na kuacha mzaha katika katika suala zima la Corona.

Huyu Mungu si hirizi, anataka kila binadamu awajibike na atumie uwezo wake kufikiri. Corona ipo, unaambiwa chukua tahadhari unasema mimi nasali. Mungu wetu anataka watu wawajibike, si kusema tu, tunasali - Ameongeza Padri Charles Kitima
 

dudus

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
13,896
2,000
... what a saddest moment! Wapumzike kwa amani. Corona ipo; wananchi tuchukue tahadhari tujiepushe na kauli za wanasiasa matapeli! Ukifa umekufa wewe ni simamnzi kwa familia yako huyo anayekudanganya hakuna Corona wala hatakuwa na msaada wowote kwa familia yako in your absence!

Jikinge na uwakinge wengine; jali uhai wako na wa wengine utakuwa umetimiza kwa matendo amri isemayo USIUE.
 

Cicadulina

JF-Expert Member
Sep 8, 2015
818
1,000
Hatari na nusu
IMG_20210303_114349.jpg
 

Clemence Mwandambo

JF-Expert Member
Dec 2, 2018
921
1,000
Marekani wamekufa, Italia wamekufa, wazungu wengi wamekufa na wanaendelea kufa. Hawa ndiyo wataalamu na wanasayansi wa dunia, wanajua kujihami kuliko sisi, na watu makini na wenye maendeleo kuliko sisi.

Hawa watu wameweka lockdown lakini korona imewafuata mpaka majumbani, hata viongozi wa nchi zao wamepatwa na huu ugonjwa. Swali ni Je? Nini unaweza kuwa utatuzi? Tusaidiane kutafakari tusiache misimamo ya kisiasa itutawale.
 

Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
15,203
2,000
... what a saddest moment! Wapumzike kwa amani. Corona ipo; wananchi tuchukue tahadhari tujiepushe na kauli za wanasiasa matapeli! Ukifa umekufa wewe ni simamnzi kwa familia yako huyo anayekudanganya hakuna Corona wala hatakuwa na msaada wowote kwa familia yako in your absence!

Jikinge na uwakinge wengine; jali uhai wako na wa wengine utakuwa umetimiza kwa matendo amri isemayo USIUE.
Hizo ndio gharama za kumfurahisha shetani. Anafurahia sana kafara kama hizo.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom