BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,009
TEC na KKKT: Mkisema ni nongwa; Msiposema ni nongwa.
Makanisa mawili makongwe hapa nchini yamesema kwa uchungu kuhusu vifo vinavyotokana na Corona. Nawapongeza.
Mijadala inayoendelea kuhusu matamko hayo inaonyesha makanisa haya yana dhamana ya kuchukua hatua katika jamii. Yalipokaa kimya watu walihoji. Sasa yamesema, baadhi ya watu (Mzalendo na Mwana harakati huru Musiba) wanahoji kwa nini yaseme.
Bahati mbaya makanisa yamesema baada ya Viongozi wake wengi kufa. Maaskofu, mapadre, wachungaji, watawa, madaktari, wauguzi na watawala wamekufa wengi. Hata angekuwa mmoja, ni wengi.
Mimi natamani yangesema zaidi ya yalivyosema. Ningetamani waseme hata haya ili kuimarisha vita dhidi ya Corona:
1. KKKT imekemea wanaoshangilia pale Viongozi wa serikali wanapougua Corona. Ni sahihi wakemewe. Ningetamani tukemee pia watanzania wanaowashangilia Wana siasa wanaotumia majukwaa kufanya mizaha juu ya Corona na kuonyesha kuwa Corona si lolote. Wananchi WAACHE kabisa kushangilia kifo. Kumshangilia kwa makofi mwanasiasa anayechezea Corona ni sawa na kushangilia pale mtu anapokufa kwa Corona. Tangu Sasa makofi yawe kipimo cha kukosa uzalendo.
2. Baadhi ya hospitali za umma zinakataa kupokea wagonjwa wenye dalili za Corona. Matokeo yake hospitali chache za mashirika na makanisa ndizo zinapokea wagonjwa hao. Hii inasababisha mrundikano wa wagonjwa sehemu moja. Serikali ikemee tabia ya hospitali zinazokataa wagonjwa lakini pia serikali izipe msaada na vifaa zile hospitali zinazopokea wagonjwa. Kubaguana si tabia ya Corona.
3. Pamoja na hotuba za kutahadhalisha, nashauri mabango ya kuelimisha mitaani yawekwe; Viongozi wa mitaa wakague kila nyumba kuona uwepo wa vifaa vya usafi. Mbona kodi tunaenda majumbani kufuatilia?
4. Wataalam wa magonjwa mlipuko wanakiri hatua mojawapo ya kudhibiti maambukizi ni kujitenga au kuzuia muingiliano kwa muda ili upepo mbaya upite. Tukichukua tahadhari zote tukaacha hili, hii vita tutaishinda? Wataalam waongee. Sisi wengine tukae na kusikiliza kama tunavyosikilizwa pale tunapoongelea utaalam wa uwanja wetu.
Tusizuiane kulia.
HATA MMOJA NI WENGI.