TEC: Mipasuko kwenye jamii Husababishwa na Watu fulani kujiona bora zaidi na wako juu ya Katiba na sheria

Sijui mungu wako alivyokuelekeza ufunge, and hoja ni kuwa mna mbwembwe nyingi siku ya kutangaza kwaresma but Sijawah kuona anayefunga chochote kile.
Mkuu nachokiona kwako ni kuwa mfungo wako wewe Ni tofauti na mfungo wa hao jamaa. Wewe kufunga kwako Ni kwa damu na nyama ndo maana inaonekana Sana kwa nje. Hao jamaa wao wanazingatia zaidi ya rohoni. Ndo maana unawaona hawana tabu kuingia na mabuti kanisani kwani kwao sakafu kuchafuka tope si ya muhimu Sana Bali la muhimu kwao Ni roho isichafuke tope. Sasa roho haoinekani Mkuu lakin sakafu unaiona kirahisi tu.
 
Hahahhahha
 
Hakuna nabii alienda kumkosoa mfalme kipindi cha mfungo .Kipindi cha mfungo walikitumia kwa kuwa mbele za MUngu tu Kuomba yao na kuombea taifa hawakwenda kukosoa.Huo mfungo batili baraza lifute huo waraka umekaa kifarisayo sio wa mfungo wa Kikristo!!
Sauti ya viongozi wa dini ni sauti ya Mungu mwenyewe Nabii Nathaniel aitumwa kwenda kwa Mfalme Daudi kumweleza kuwa alivyomchukua Besheba mke wa Huria ni dhambi, Mfalme Daudi aifunga siku saba kwa ajili ya toba. Viongozi wetu Maaskfu wameona viongozi wa kisiasa wanajina wao ni daraja la juu haswa baada ya kuchaguliwa basi wafanye toba.

Ndugu yangu kwenye biblia hakuna kipindi cha mfungo, wana wa Israel walikuwa wanafunga baada ya kuambiwa makosa na dhambi zao Nabii Yona aliwaambia wana wa Ninawi makosa yao na wakafunga n.k, Kwaresma imeanza baada ya kifo cha Yesu Kristo kama kipindi cha mfung kufanya toba mbele za Mwenyezi Mungu.
 
BARAZA la Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini Tanzania (TEC), limewataka Watanzania kuacha siasa za upendeleo na ubinafsi, kwa kuwa zinasababisha mfarakano katika kijamii.

Wito huo umetolewa na TEC kupitia ujumbe wake wa Kwaresma uliotolewa hivi karibuni, ukiwa na kichwa cha habari “Ingekuwa heri leo msikie sauti yake, msifanye migumu mioyo yenu…” (Zab 95:7-8).

Leo Jumatano, tarehe 17 Februari 2021, Wakristo wengi duniani wameanza ibada ya Kwaresma.

Kwenye ujumbe huo wenye kurasa 29, umehusisha maaskofu 33 akiwemo Rais wa TEC, Gervas Nyaisonga, umeelezea mambo mbalimbali ya kijamii, kisiasa na kiroho ukisema, kwa sasa dunia imeshuhudia manung’uniko na malalamiko kutoka kwa umma.

Malalamiko hayo ni juu ya baadhi ya viongozi wanaotumia mamlaka zao kufanya mambo kwa ajili yao na wanaowazunguka ama kikundi fulani, jambo linalokuza mashaka na kuondoa uaminifu.

“Licha ya hayo yote mema ambayo wenye mamlaka hususani ya kisiasa wamekabidhiwa, nyakati zetu hizi dunia, imeshuhudia manung’uniko na malalamiko kutoka kwa umma kwamba baadhi ya viongozi, wanatumia dhamana hiyo kwa ajili ya kujinufaisha wenyewe au kwa ajili ya manufaa ya kikundi fulani.”

“Siasa za namna hiyo, husababisha unyanyasaji wa baadhi ya watu au kikundi cha watu na hivyo kuondoa hali ya kuaminiana,” limeeleza baraza hilo la juu la Kanisa Katoliki.

Ujumbe huo umeeleza wazi kwamba, miongoni mwa mipasuko mikubwa ya kisiasa inayotokea katika jamii, huchagizwa na kutokana na kikundi cha watu fulani kujiona ni wa daraja la juu na bora kuliko kingine.

Na kwamba, kikundi hicho wakati mwingine kujiona kiko juu ya Katiba na Sheria mbalimbali za nchi na hivyo kuzivunja pasi na kujali.

“Matokeo ya haya yote ni kufarakana kijamii, lawama zisizoisha na hivyo kuhatarisha amani na usalama wa jamii husika,” umeeleza waraka huo.

Ujumbe huokutoka Kitabu cha Zaburi 95:7-8 ‘Ingekuwa heri leo msikie sauti yake, msifanye migumu mioyo yenu,’ umewakumbusha Watanzania kurudi kwenye misingi ya Mungu ili kuleta uongozi bora na siasa safi.

“Kati ya maeneo muhimu sana ya kipimo cha uongozi bora na siasa safi, ni namna kiongozi anavyoishi uadilifu wake wa uongozi tukitambua kwamba “Hakuna mamlaka (halali) isiyotoka kwa Mungu”(Rum 13:1). Kutokana na hilo, uongozi, madaraka au mamlaka yoyote ile inapaswa kuwa ni dhamana kutoka kwa Mungu.

“Dhamana hii anapewa kiongozi kama mwakilishi wa Mungu katika uongozi tukitambua Mungu ndiye kiongozi na mtawala pekee. Dhamana hii inapaswa kumkumbusha kiongozi kwamba, mamlaka aliyopewa si kwa ajili yake bali ni kwa ajili ya wote aliokabidhiwa,” umekumbusha waraka huo.

TEC limewataka Watanzania kusikia sauti ya Mungu kwa kufanya toba na kuilainisha mioyo yao, katika kuhakikisha haki inatendeka katika jamii.

“Ujumbe wa Kwaresima unatutaka kama jamii “tusikie sauti yake, tusifanye migumu mioyo yetu. Tutaisikia sauti ya Mungu kwa kuhakikisha kwamba haki inatendeka katika jamii.

“… na hasa haki za kikatiba za kujiendesha kisiasa zikiwemo kuheshimu uhuru wa mawazo mbadala, kama sehemu ya kudumisha demokrasia na hasa katika mfumo wa vyama vingi vya kisiasa ,” umeeleza ujumbe huo.

Chanzo: Mwanahalisionline
Kwa ujumbe huu hatajumuika kwenye kanisa katoliki kwa ibada ya kwaresma. Atajiendea kwa walokole au kkkt.
 
Upload waraka hapa tuusome😇
 
Ujumbe wa Kwaresima ulitakiwa ujikite kwenye imani zaidi mfano badala ya porojo za kisiasa ulitakiwa

1. Ueleze kipindi hiki kuwa cha maungamo kwa kila mtu kibinafsi kuacha mabaya na kutenda mema kama wafanyavyo waislamu kipindi cha mfungo wa ramadhani

2. Usisitize watu kujitoa kwa moyo wote kuhudumia wengine kama KRISTO alivyojitoa

3. Kuwahurumia wenye shida na mateso kama wagonjwa,yatima ,wahitaji wa chakula nk kama Yesu alivyosaidia wahitaji alipokuwa duniani

4. Kuomba Mungu atuepushe na janga la Corona .Yaani waraka umejaa porojo ina maana kuomba swala la Corona hawajakupa uzito!!!

5. Kuombea uchumi wa nchi na watu wake

Huo waraka umekaa kifarisayo kufunga wafunge wakatoliki halafu washambulie wanasiasa mfungo ni kujirudi mwenyewe ndani sio kuangalia huko kwingine nje kuna nini?
Usiwapangie
 
Back
Top Bottom