Team Visasi: Waliomunga Mkono Lowassa Niwasaliti Je Waliomunga Mkono Migiro, Membe na January

waliounga mkono membe, migiro, january, na wengineo isipokuwa lowasa, baada ya kupitishwa magufuli walikubali wakamuunga mkono na kuendelea na mwenendo mwema katika chama.

waliomuunga mkono lowasa hawakukubali kumuunga mkono magufuli, walibaki ccm kimkakati huku wakimuunga mkono lowasa na kuiba siri za chama ili kufanikisha ushindi wa lowasa huko alikokuwa chadema! hapo ndo dhana ya usaliti inapokuja! na msaliti unajua adhab yake, kama ingekuwa jeshini anauawa kabisa, ila kwenye chama anafukuzwa tu.

hata hivo sio wote waliomuunga mkono lowasa akiwa ccm wamefukuzwa! umeona kimbisa amebaki, inchimbi onyo kali, bashe bado yupo, msukuma yupo, na wengine wengi sana! walioendelea na usaliti ndo wametimuliwa.

sasa mleta mada acha kutumia hisia na kutafta huruma ya wasaliti! hii adhabu hata huko kwenu chadema ndo mlimpa zitto..
Mleta mada ni wale wale wanaopufushwa na mahaba kwa mtu badala ya kuangalia substance. Kilichofanyika Dodoma kama kikifanyika ndani ya CDM maana yake kitakuwa ni chama mbadala wa kweli wa CCM. Lakini hakiwezi kufanyika, sana sana gia zitabadilikia angani.
 
Najiuliza na kambi ya mwigulu tuwaitaje kama sio wasalitimaana hawa mabwana inaelekea walikuwa wanazi haswaa wa mh mwigulu yan nlikuwa naenda kwetu iringa nkakuta jina lake milima ya kitonga wamemsifia sana na nlipokuwa naenda arusha kupitia dodoma jina lake nililiona sana katika mawe makubwa na milima ya karibu na barabara!!!huyu nae bhas watu wake watumbuliwe...pia mbna mh mkubwa alionesha kuwa anahtaj ben ndio apite bhas na yy ni msaliti
 
wao ndio waliochunguza na kuona wanastahili hayo, haiishii wala kuanzia kwenye nyimbo.
Imani inatakiwa kufa baada ya kuchagua aliyepitishwa lakini bado mtu anaviziavizia upande wa adui kuendeleza imani upande wa pili.
Acha kuweweseka na kutetea kila kitu, nyoosha point yako ieleweke. .
 
ya ngoswe tumuachine ngoswe mwenyewe , lakini kuna hatari mtu kujiongezea muda wa kutawala time will tell maana bwana yule kalewa madaraka
 
Baada ya kufanya mambo ya maendeleo wao kutwa kufikiri ya kijinga na visasi tuu Nchi haiwezi kuendelea bila hata kupingwa hakuna kitu kama hicho ni mwisho wa kufikiri..
 
Sijaelewa hoja ya hao wanaoitwa "wasaliti" ndani ya CCM. Hivi kumuunga mkono mtu kwenye kura za maoni ni usaliti? Unapotangaza nia ya kugombea definatelly kuna watu watakuunga mkono na kukupigania. Baada ya kura za maoni kama jina lako halitapitishwa mtamuunga mkono aliyepitishwa. Sasa hapo usaliti unakujaje?

Mimi nilipotangaza nia ya ubunge Moshi (V) kuna watu waliniunga mkono, lakini baada ya mchakato wote kukamilika akapitishwa Mhe.Komu, na tukamuunga mkono. Nilifunga safari kutoka Songea kwenda Moshi kumuombea kura. Na waliokua wakiniunga mkono wakamssuport Komu. Sasa je Komu angewaita wasaliti kwa sababu hawakumuunga mkono kwenye kura za maoni?

Ninachokifahamu ni kwamba hao waliofukuzwa CCM walimuunga mkono Lowassa akiwa CCM wakati wa kura za maoni. Walipigana kuhakikisha jina la Lowassa linapitishwa kama jina la mgombea Urais kupitia CCM. Lakini baada ya Magufuli kupitishwa walimuunga mkono. Mfano mzuri ni Msukuma. Huyu alifunga safari kwa Helcopter hadi Arusha kumuunga mkono Lowassa wakati wa kutangaza nia. Lakini alipopitishwa JPM, akahamia upande wa JPM na kumnadi. Sasa mtu kama huyu anaitwaje msaliti?

Neno usaliti maana yake ni nini? Kwahiyo ndani ya CCM ni dhambi kuwaunga mkono wagombea wengine wakati wa kura za maoni? Yani unataka kwenye kura za maoni watu wote wamuunge mkono mtu mmoja tu. Hapo ndo itaonekana hamna usaliti?

Sasa naanza kuelewa kwanini 2020 wanataka apitishwe peke yake. Wakiriluhusu wagombea wengine, wafuasi wao wataitwa wasaliti tena.

Anyway, waliomuunga mkono Lowassa wameitwa wasaliti na kufukuzwa, vipi waliomuunga mkono Membe, Migiro, January etc. Hawa usaliti wao utajadiliwa lini na watafukuzwa lini? [HASHTAG]#TeamVisasi[/HASHTAG]
Kwanini mlimtimua Prof Kitila na Mwigamba?
 
Hili ni fundisho la wanasiasa kuacha unafiki umemuunga mkono mtu kwa kumuamini anaweza kuleta mabadiliko mfuate hata akihama chama
 
ndio maana mnaambiwa hamshirikishi ubongo unajua diplomasia wewe
Mnaoshirikisha ubongo ni nyinyi "mateja", mnaitwa mkapime mkojo mnakimbilia mahakamani kuweka zuio.

Nchi inakwenda kisayansi zaidi, mnabanwa kila kona na kwa sababu ile kitu imeshakula ubongo wenu, hamjui nini kinaendelea.
 
Mleta mada ni wale wale wanaopufushwa na mahaba kwa mtu badala ya kuangalia substance. Kilichofanyika Dodoma kama kikifanyika ndani ya CDM maana yake kitakuwa ni chama mbadala wa kweli wa CCM. Lakini hakiwezi kufanyika, sana sana gia zitabadilikia angani.
ukweli unawaweka huru watu wa visasi mzimu wa Lowassa unawatafuna sana
 
Mimi nawaza tu Magufuli hana kukumbukumbu na kama ana kumbukumbu ana kisirani sana na kundi hili la Lowassa.

Wakati wa kura ya maoni kundi hili lilimpa kura zote yeye je wangempa mwingine leo angekuwa pale? Kwa nini leo awaone hawafai? Jambo hili linaweza kuwa tatizo mbele ya safari kwa kuwa bado wapo wengi humo wanaweza kuamua kufanya hujuma rasmi wakiamini siku yeyote wanaweza kutumbuliwa.

Nyingine ni kwamba rais ana hofu kubwa sana mimi nashindwa kuelewa mtu aliyeshinda anaandaa watu wawe wanamwogopa badala kutumia weledi na sheria za nchii?

Yangu macho karibuni
Kinachomsumbua Magufuli ni hawa wafuasi wa Lowasa walimdindia Kikwete, sasa anahofu na yeye watam-outsmart ndiyo maana amekuja na hii layman solution.
 
Back
Top Bottom