Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
Sijaelewa hoja ya hao wanaoitwa "wasaliti" ndani ya CCM. Hivi kumuunga mkono mtu kwenye kura za maoni ni usaliti? Unapotangaza nia ya kugombea definatelly kuna watu watakuunga mkono na kukupigania. Baada ya kura za maoni kama jina lako halitapitishwa mtamuunga mkono aliyepitishwa. Sasa hapo usaliti unakujaje?
Mimi nilipotangaza nia ya ubunge Moshi (V) kuna watu waliniunga mkono, lakini baada ya mchakato wote kukamilika akapitishwa Mhe.Komu, na tukamuunga mkono. Nilifunga safari kutoka Songea kwenda Moshi kumuombea kura. Na waliokua wakiniunga mkono wakamssuport Komu. Sasa je Komu angewaita wasaliti kwa sababu hawakumuunga mkono kwenye kura za maoni?
Ninachokifahamu ni kwamba hao waliofukuzwa CCM walimuunga mkono Lowassa akiwa CCM wakati wa kura za maoni. Walipigana kuhakikisha jina la Lowassa linapitishwa kama jina la mgombea Urais kupitia CCM. Lakini baada ya Magufuli kupitishwa walimuunga mkono. Mfano mzuri ni Msukuma. Huyu alifunga safari kwa Helcopter hadi Arusha kumuunga mkono Lowassa wakati wa kutangaza nia. Lakini alipopitishwa JPM, akahamia upande wa JPM na kumnadi. Sasa mtu kama huyu anaitwaje msaliti?
Neno usaliti maana yake ni nini? Kwahiyo ndani ya CCM ni dhambi kuwaunga mkono wagombea wengine wakati wa kura za maoni? Yani unataka kwenye kura za maoni watu wote wamuunge mkono mtu mmoja tu. Hapo ndo itaonekana hamna usaliti?
Sasa naanza kuelewa kwanini 2020 wanataka apitishwe peke yake. Wakiriluhusu wagombea wengine, wafuasi wao wataitwa wasaliti tena.
Anyway, waliomuunga mkono Lowassa wameitwa wasaliti na kufukuzwa, vipi waliomuunga mkono Membe, Migiro, January etc. Hawa usaliti wao utajadiliwa lini na watafukuzwa lini? [HASHTAG]#TeamVisasi[/HASHTAG]