TCU yakiri dosari taarifa ya wanafunzi 8,357

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,885

  1. MONDAY, FEBRUARY 27, 2017 na Mwananchi online
    pic+TCU+yakiri.jpg



    Kwa ufupi
    • Taarifa kutoka TCU kwa vyombo vya habari imesema kuwa uhakiki wa sifa za wanafunzi ni kazi endelevu ya tume na kutokana na maombi ya wadau mbalimbali ,tume sasa itaendelea kuwasiliana moja kwa moja na vyuo katika kukamilisha zoezi hilo.

    Dar es Salaam. Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania ( TCU) imetoa ufafanuzi kuhusu wanafunzi 8,357 waliotajwa kuwa hawana sifa stahiki za kuendelea na elimu ya juu na kudai kwamba kulikuwa na dosari katika taarifa zao.

    Taarifa kutoka TCU kwa vyombo vya habari imesema kuwa uhakiki wa sifa za wanafunzi ni kazi endelevu ya tume na kutokana na maombi ya wadau mbalimbali ,tume sasa itaendelea kuwasiliana moja kwa moja na vyuo katika kukamilisha zoezi hilo.

    Taarifa hiyo imesema wanafunzi wote walioorodhesha katika taarifa iliyotolotewa awali wanaombwa kuwa watulivu na kuendelea na masomo yao ya kawaida.

    “TCU inapenda kuuarifu umma kuwa ,uhakiki wa ubora wa wanafunzi wa elimu ya juu hufanyika kwa mujibu wa kifungu 5(1)(b)c) cha Sheria ya Vyuo vikuu Sura ya 346 YA Sheria za Tanzania,’’imesema taarifa hiyo.
 
Baada ya wiki ndyo imekili? Kweli hii serkali imekabwa kila inapotaftia kiki panabums
 
Magu chukua hatua ktk hii wizara
Maana kuna watu walishaathirika na tamko la awali.
Onyo linatakiwa ili kosa kama hilo lisijurudie
 
Sasa waliosafiri kutoka mikoa mbalimbali kwenda vyuoni watarudishiwa pesa zao za nauli na kujikimu njiani?
 
TCU ni hopeless institution. Inaongozwa na maprofesa waliochoka kabisa. Magufuli vuruga hii TCU hakuna wanachojua. Wanakiri kosa baada ya kuchafua taswira ya elimu yetu kimataifa? Hii inatofautianaje na kile alichofanya yule wa NIMRI?
 
Do they know the damage they have caused to the country? Haya mambo ya "MATAMKO" yataigharimu nchi brand za vyuo vyetu zilijengwa kwa gharama kubwa sana, watu wanaona kutangaza ni jambo rahisi lakini ukweli ni kwamba tumeharibu taswira ya vyuo vyetu kimataifa, waliohusika wachukuliwe hatua kali za kinidhamu.
 
Back
Top Bottom