TCU yakifuta Chuo Kikuu cha Eckernford kwa kutokidhi vigezo vya kudahili

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,444
3,354
Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), Profesa Charles Kihampa amesema Chuo hicho kilichopo Mkoani Tanga kimefutwa kutokana na kushindwa kukidhi vigezo vya kudahili

Amesema hayo jana Julai 17 na kuongeza kuwa vyuo ambavyo havijatimiza vigezo bado vimepewa miezi sita ya kufanya hivyo ili viweze kufunguliwa na kufanya udahili

TCU imekifuta chuo hicho ikiwa ni miezi takribani kumi imepita tangu ilipokitangazia kusitisha utoaji mafunzo na kuamuru wanafunzi waliokuwa wakisoma chuoni hapo kuhamishiwa vyuo vingine

Aidha, baadhi ya vyuo ambavyo vilizuiwa kufanya udahili katika baadhi ya kozi ili viweze kufanya maboresho katika sehemu ambazo walikuwa na upungufu ikiwemo Wahadhiri wenye sifa, vimefunguliwa

Chuo cha Marian kimefunguliwa kozi mbili, Chuo cha United African for Africa kimefunguliwa kozi mbili na Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala (KIU) tawi la Tanzania kimefunguliwa kozi tano
 
Back
Top Bottom