Influenza
JF-Expert Member
- Jul 1, 2018
- 1,445
- 3,403
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), imesitisha udahili na kufuta baadhi ya Vyuo vilivyofungiwa mwaka 2017 na kutakiwa kufanya maboresho mbalimbali lakini hawakufanikiwa kurekebisha dosari hizo
Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Sebastian Kolowa kimeendelea kuziwa kufanya udahili kutokana na kutokidhi viwango vya Kitaifa na Kimataifa
Vyuo vilivyoruhusiwa kufanya udahili kwa baadhi ya masomo ni Chuo cha Umoja wa Waafrika Tanzania, Teofilo Kisanji (Mbeya), Chuo Kikuu Kishiriki cha Askofu Mkuu Mihayo na Chuo Kikuu cha Kampala-Tanzania
Vingine ni Chuo Kikuu Kishiriki cha Marian, Chuo Kikuu Kishiriki cha Uhandisi na Teknolojia cha Mt. Joseph, Chuo Kikuu Kishiriki cha Kikristo cha Tiba Kilimanjaro (KCMUCo) na Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Stefano Moshi (SMMUCo)
Vyuo vilivyofutwa ni Chuo Kikuu Kishiriki cha Askofu Mkuu Jacob, Chuo Kikuu Kishiriki cha Kadinali Rugambwa (KARUMUKO), Chuo Kikuu cha Teofile Kisanji (Dar), Chuo Kikuu cha Mt. Yohana Kituo cha Mt. Marko na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Arusha
Vingine ni Chuo Kikuu Kishiriki cha Josiah Kibira (JOKUCo), Chuo Kikuu cha Mlima Meru (MMU), Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Tiba na Teknolojia (IMTU) na Chuo Kikuu cha Bagamoyo (UoB)
Aidha, Katibu Mtendaji wa TCU, Profesa Charles Kihampa amesema Chuo Kikuu Kishiriki na Sayansi Shiriki cha Mt. Francis cha Ifakara (SFUCHAS) kimeruhusiwa kufanya udahili kuanzia mwaka 2020/21