TCU watoa mwongozo wa gharama za kufanya applications ya kujiunga chuo Kikuu 2017/18

mswahili93

JF-Expert Member
Apr 16, 2017
210
115
Mama Ndalichako ashasikia kilio chenu, pesa ya udahili inayotakiwa kutozwa ni sh.10,000/=

upload_2017-7-27_15-7-36.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa naona serikali inavitega vyuo binafsi na wanafunzi. Kutakuwa na maombi mengi yatakayo elekezwa vyuo vya umma kufuatia tangazo hili (simple economics) sasa vyuo binafsi vinaweza kuingia kwenye shida. Pili wanafunzi wakijazana vyuo vya serikali ambavyo havitoshi kuwadahili wote ushindani utaongezeka na hatari ya kukosa chuo itaongezeka.

La pili tujiuliza je kweli gharama halisi ni Shs 10,000? Kuna wakati TCU walisema wangetoa gharama elekezi hawakufanya hivyo. Chuo kinachoshika gharama ya chini ni kama UDSM, TIA 20, 000. Sasa hii ya 10 imetoka wapi? Ina faida na madhara gani kwa utoaji elimu kwa watanzania? Je italipa kwa vyuo binafsi kushusha gharama za usajili ili kuvutia waombaji zaidi?
 
Nini chanzo cha hii habari?Naomba mtupatie the original PDF na sio hizi picha ambazo uhalali wake unatia mashaka
 
Hii anuani ya Waziri wa Elimu inashangaza kwa kweli

"Koleji ya Humanities"
 
TCU imeagiza uongozi wa vyuo vya elimu ya juu kuwa gharama za kuomba kujiunga na chuo ni Tsh. 10,000/- tu kwa kila chuo.

Hii ni kutokana na utaratibu wa applications kubadilika na kuwa kila Mwanafunzi atatakiwa kutuma Maombi ya kujiunga na chuo moja kwa moja chuoni tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma!!

Binafsi nawapongeza TCU kwa kusimamia jambo hili mapema.

Msaada, Institute of Accountancy Arusha nayo inahusuka? au hiyo siyo University!
 
Back
Top Bottom