TCU: Wasiokuwa na Sifa Walipenyezaje CAS? Au walidukua mfumo?

Naisujaki Lekangai

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
1,340
1,377
TCU wametoa majina ya wanachuo waliodahiliwa vyuoni bila eti kuwa na sifa!
Udahili wote wa vyuoni ulifanywa na tcu kwa kupitia mfumo wao wa cas.Huwezi kuingia cas bila kuwa na index no. ya mtihani wa kidato cha nne na sita.Index namba hizo zinaonesha ufaulu wa masomo ya kidato cha nne na sita na hivyo kudahiliwa kwa ufaulu huo, angalau D nne kidato cha sita.
Sasa kwa mfumo wa cas, hao wasio na sifa wametokea wapi?Au kuna wajanja walidukua mfumo?
 
Unasoma miaka 3 ama 4 ama 6 mtu anaamka asubuh anakuambia tupa ulichosoma ...gharama ulizopoteza all wasted on deep sea.

Sielewi kwa kweli. Sielewi
 
Siku mbili zilizopita tume ya vyuo vikuu ilitangaza kuwaondoa vyuoni wanachuo waliodahiliwa na wao wenyewe kwa kosa la kwamba eti hawajatimiza vigezo...

Hadi sasa ni wanafunzo 8000 ambao inaonekana kutotimiza vigezo kwa mujibiwa wa waziri wa elimu Tanzania bibi ndalichako..

Sababu na maelezo ya kutosha hayajatolewa ingawa hapo mwanzo wanafunzi hawa walidahiliwa na tume yenyewe ya vyuo vikuu!

Swali muhimu la kujiuliza
1.ilikuwaje tume ilisajili wanafunzi wasio na vigezo.

2.ilikuwaje tume iliendelea kutoa mikopo kwa wanafunzi wasio na vigezo wa kusoma kozi husika.

Hayo ni maswali mawili muhimu sana ambayo kila mwenye akili timamu na aliesoma na anayetegemea kwenda kusoma chuo kikuu...

Wanafunzi wengi watakao athirika ni watoto wa masikini.Ambao wandugu zao serikali imewanyima ajira.

Kwa maana hiyo kama wataondolewa vyuoni serikali itakuwa imeongeza wimbi kubwa la watu wasio na ajira mitaani pamoja na kuongeza vifo visivyotarajiwa(wengi watajinyonga)..

Matatizo yaliyopo katika serikali yanayopelekea matatizo haya..
1.kuingiza siasa katika suala la elimu..
2.kufanya kazi au kutekeleza majukumu kwa sifa..
3.kutekeleza majukumu yao kwa shinikizo la aliye juu..
4.serikali kuwa kipofu(haitambu inakokwenda),hakuna mission and vision statements..
5.kufanyakazi kwa kumlizisha bwana mkubwa aliye juu kuliko wote Tanzania.
6.kutimiza majukumu kwa ajili ya kukomoani hatimaye wanaoathirika ni watoto wa masikini..
7.serikali kutokuwa na mission katika elimu.
8.baadhi ya watumishi vilaza walioteuliwa na bwana mkubwa wenye kutoa maamuzi yasiyo na kichwa wala miguu..(mfano.Daudi bashite,Hamisi kigwangalla n.k)
9.Kutokufuata ushauri wa wataalamu walipo katika ofisi zao(hasa ofisi ya ikulu)


Kutokana na hayo serikali itegemee yafuatayo..
1.maandamano makubwa ya wanafunzi wote wa vyuo vikuu..
2.maandamano ya waliosoma na kukosa ajira za umma..
3.kushuka kwa kiwango cha ufaulu katika shule za chini.
4.itegemee kupungua kwa nguvu kazi ya taifa(vijana watajinyonga)
5.itegemee chuki kutoka kwa wananchi wote hususani wazazi..
6.itegemee vurugu zitakazo anzishwa ilikufukuza wageni walichukua ajira za wazawa bila kuwa na vibali rasmi na serikali kuwatazama tu..
7.n.k

Ushauri kwa bwana mkubwa!
1.Baadhi ya watu katika serikali yako hawakufai(jaribu kuunganisha dots)
2.jitathimini wewe mwenyewe ujue wewe ni nani na unamchango gani katika jamii hususani ya wanyonge kama wewe ulivyokuwa unajigamba na unavyoendelea...
3.say what you mean and mean what you say(hasa hapa kwenye wanyowapinzani,ata ushauri wa wataalamu...(umoja ni nguvu,phd moja haijengi nchi kwa maamuzi ya phd moja)
5.punguza nguvu za kupambana na wapinzani jenga nchi..

Ushauri kwa wateule wa rais..
1.Mungu akusema siku wala saa ya kuchukua ulimwengu hivyo ivyo kwa upinzani kuchukua nchi.
2.Acheni kufanya kazi kwa kumrizisha rais.
3.Acheni sifa za kutoa matamko kila siku matokeo yake fanyeni kazi..
4.kumbukeni mnaishi na watoto wa masikini katika mazingira yenu..
5.leo kwao kesho kwenu kwamaana ya watoto wenu..
6.Jitathimini mapema kidha achia ngazi au endelea na kazi..

N.k

Mwisho...
By Coming President of united republic of Tanzania*.

Usinitukane mimi mtoa hoja,kwa sababu ukinitukana mimi utakuwa umeitukana familia yako..

Jadili kwa uangalifu bila uchochezi wamoja kwa moja au uliojificha..

Nimetumia haki yangu ya kujieleza kwa mujibu wa katiba ya URT.
Ahsante.
 
Wabongo mwapenda mishahara mikubwa lakin kwa kugushi vyeti, mafeliaz ndo mnaleta sifa chafu
 
Wana TCU yao chuoni..?? Anyway kuna kitu hujui ila serikli ya mwaka huu kazi IPO....
Hizi salakasi bado mabosi TCU wamekalia viti..
hivi kwenye list ya vyuo vyenye hao wanafunzi wasio na sifa, kuna chuo kimoja tu? mimi nimeona vyuo vyote vya Tz vipo, hadi UDSM.
hapa mimi naona TCU waje na majibu juu ya kuruhusu kwao wasio na sifa kudahiliwa, maana mwaka jana TCU walipiga marufuku kudahili vyuoni, hivyo vyuo vyote Tz vilidahili kupitia mfumo wa pamoja wa CAS.
 
Back
Top Bottom