TCU toeni tamko kuhusu honorary degree ya Musukuma

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,011
144,371
Kamisheni ya vyuo vikuu nchini(TCU), inapaswa kutoa tamko juu ya uhalali wa shahada ya heshima aliopewa Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Msukuma na si kukaa kimya kama hawahusiki ili hali jambo hili mpaka sasa teyari limezua mjadala mpana mitandaoni.

Tamko lao ni wazi litazua mjadala mpya iwapo kweli chuo hicho hakitambuliki lakini watakuwa wamemaliza utata uliopo na zaidi watakuwa wamesaidia wengine wasitapeliwe iwapo chuo hicho kweli ni cha kitapeli kama inavyodaiwa.

TCU timizeni wajibu wenu na tukio hili liwaamshe muweke mikakati kuhakikisha jambo hili halijirudii tena hapa nchini vinginevyo tutahisi na nyinyi ni sehemu ya tatizo.

Hili inawahusu either moja kwa moja au vinginevyo.

Screenshot_20211206-135354_Chrome.jpg
 
Kamisheni ya vyuo vikuu nchini(TCU), inapaswa kutoa tamko juu ya uhalali wa shahada ya heshima aliopewa Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Msukuma na si kukaa kimya kama hawahusiki ili hali jambo hili mpaka sasa teyari limezua mjadala mpana mitandaoni...
Acha wivu we we kwani msukuma amehakikiwa na anastahiri kuwa hata professor. TCU unataka wafanye nini nawakati waliomtunuku ni chuo kikuuu cha kimataifa ulimwenguni koteee. Kuanzia Leo anaitwa Dr. Msukumaaa.
 
Wivu ni kitu kibaya sana kwan mkuu unajuwa utoaji wa elimu kwa vyuo vya kimataifa kama hicho unachokipigia kelele! We unataka TCU Watoe tamko gani mkuu
 
Kamisheni ya vyuo vikuu nchini(TCU), inapaswa kutoa tamko juu ya uhalali wa shahada ya heshima aliopewa Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Msukuma na si kukaa kimya kama hawahusiki ili hali jambo hili mpaka sasa teyari limezua mjadala mpana mitandaoni...
Kama ya Gwajima na Mrema wanazitambua na hii ya Msukuma wataitambua. Sijawahi kuwasikia wakitoa comment yoyote kuhusu hizi PhD za kununua online
 
Anastahili tena sana, na bora aliishia darasa la 7a na ana manufaa sana kwa jimbo lake na taifa. Wako wengi wamesoma mpaka wamepata phd ya darasani lkn hawana msaada kwenye jamii na cv zao lundo, (big up joseph kasheku msukuma).

Kuna watu wana ma phd za darasani lkn hata ulkiwaiza wenyewe wana mchango gani kwa taifa watakwambia hawajuhi zaidi ya kuwafisha mitihani watoto wa wenzao.
 
Acha wivu we we kwani msukuma amehakikiwa na anastahiri kuwa hata professor. TCU unataka wafanye nini nawakati waliomtunuku ni chuo kikuuu cha kimataifa ulimwenguni koteee. Kuanzia Leo anaitwa Dr. Msukumaaa.
Wamwache bwana mbona profess maji mrefu walimuacha
 
Kama ya Gwajima na Mrema wanazitambua na hii ya Msukuma wataitambua. Sijawahi kuwasikia wakitoa comment yoyote kuhusu hizi PhD za kununua online
Hawana haja ya kuzitolea matamko. Hawa Jamaa wameamua kujiita hivyo. Ni kama ilivyokuwa kwa Professor Maji Marefu..... Hakuna tofauti...!!
 
Kwanini iwe kwa msukuma pekee wakati kina Jakaya nao waliwahi kupewa?

Tukubali tu dunia imebadilika, siku hizi kupewa udokta au vyovyote imekuwa rahisi sana, muhimu uwe unatambulika kisiasa.
 
Kuna muda huwa nafikiri u-dokta wa maana ni ule wa kutibu watu na wanyama huu u-dokata wa vitabuni wengi huwa ni madesa madesa hadi anaupata.
 
Back
Top Bottom