TCU mnaturudisha nyuma. Kwa mfumo wenu mpya wa udahili vyuoni, mnatuonea wananchi

Hauna haja ya kwenda kwenda kwenye chuo husika, kila kitu ni online tu
 
Watanzania wengi ni vilalamishi sana, mlikuwa mlialia kuhusu TCU, CAS, sasa mmeletewa mlichokitaka yowe tena mmeanza.

Huu mfumo, ndiyo utawakomesha wanaodharau vyuo vingine, ukikosa kile unachotaka ndiyo imekula kwako utasubiria hadi mwaka mwingine na ambapo uwezekano wa kudahiliwa unakuwa pia ni mdogo sana kwa sababu ya ushindani.

Japo, huu mfumo sasa utavigharimu vyuo vikuu ikitokea vikasajili wanafunzi vilaza au wenye vyeti feki.
 
Binadamu sisi, mungu mwenyewe ndo anajua. Rais wako alikuwa haipendi CAS , TCU wameivunja, what if CAS inakuchagua ktk chuo usichokipenda?
Hivi ni kweli kwamba wamezingatia utafiti kufanya Haya maamuzi au ni hisia tu maana kwa nijuavyo CAS ilikuwa nzuri wangedhibiti 10% kwa sasa uwezekano wa kuweka rushwa zaidi na uonevu kwenye kuchagua utakuwa mkubwa
 
Kwanza wewe mtoto unaogopaje gharama wakati atalipa mzazi au mlezi wako? Acha kila mtu atimize ndoto ya kusoma chuo anachokipenda ili vyuo viwe na ushindani wa kuboresha elimu na sio kusubiri kuhonga TCU
Narrow Thinking!

Sidhani kama mleta mada ni Mtoto.Pia Mwanafunzi anayemsaidia mzazi, mlezi wake gharama zisizo za lazima katika kujisomesha anapata baraka kwa Mola kuliko bingwa wa matanuzi yasiyo ya lazima.

Pia wapo wazazi pamoja na walezi wenye Uchumi mdogo sana.Mind you.
 
Kwa huu mfumo, vyuo vya private vitajizolea pesa nyingi sana.
Maana mambo yao yapo kipesa zaidi.
 
Ndio maana tutachewa kuendelea,yani mtu mmoja tu kwa utashi wake anabadilisha kila asicho penda.yalishatokea sana huko nyuma ila bado hatujifunzi.

Vyuo vinavyodaiwa kutokua na sifa kwanini viendelee kuwepo?.
Umenena vyema Mkuu.

Tunapenda sana kuremba vitu visivyo na ubora.Nadhani kama chuo hakifai basi kifutwe mazima na kisiendelee kutoa Elimu isiyokidhi vigezo stahiki kwa watoto wa kitanzania.

Tatizo linakuja pale ambapo Institute nyingi zinamilikiwa na wanasiasa kwa Miamvuli ya majina feki kama tulivyo humu Jamii Forums.

Nashauri Serikali itumia wataalamu katika masuala yanayohitaji utaalamu.La sivyo tutakuja kujuta baadaye.
 
Watanzania mbona tumekuwa vigeu vigeu sana mnataka nini juzi mumeshangilia sana rais magufuli aliposema Leo tcu wamesikio kilio chenu mnaanza kulia lia tena kweli sisi ni weusi kila kitu kulia lia tu haaaa
 
Kwa
Tatizo ndo linapokuja hapo, better kuwa na system moja ambayo ni unified kuliko kuwa na system tofauti tofauti. kumbuka kuna gharama za ku apply, ubora wa mifumo pia unatofautiana ..
Kwani CAS wanaapply bure ?
 
Inahuzunisha sana tena kwa wanaotoka familia Masikini... Ndio shida ya Siasa kuletwa kwenye Elimu
 
Hicho unachosema eti "kama chuo hakina watu wa kutosha basi TCU inajazia" ndio chanzo cha malalamiko na ndiyo sababu kubwa ya kutupilia mbali mfumo huu. Yaani unilazimishe nikasome degree ya "gender" sijui kitu gani eti Ustawi wa Jamii kwa lengo tu la kujazia chuo kilichopungukiwa wanafunzi? Vipi kuhusu career aspiration zangu, mfano nataka kusoma uchumi, ndiyo passion yangu na nimefaulu vizuri? Huu ni upumbavu na ndio sababu mojawapo ya umasikini. Kama chuo kimeanzisha kozi ambazo hazina soko wala mvuto kwa wanafunzi, chuo hicho kinapaswa kipate feedback kwa njia ya kukosa waombaji wa kozi hiyo, ndipo kitajirekebisha. Utaratibu wa 'kujazia' wanafunzi kwenye vyuo vyenye taaluma duni au kozi zisizo na soko haufai hata kidogo. Vyuo vitengeneze kozi zenye ubora na zinazohitajika sokoni, na vijijenge kitaaluma kuvutia wanafunzi, vikiwa na ranking nzuri watu watavichangamkia tu. Hongera JPM na Prof Ndalichako, kwa hapa mmefanya sahihi kabisa.
 
Kwa huu mfumo, vyuo vya private vitajizolea pesa nyingi sana.
Maana mambo yao yapo kipesa zaidi.
watapoke division 3 na 4 nying sana na gpa za 2 mpaka 2.9 nitaziona sana hivi vyuo st joseph imtu kairuki kiu teku tumaini na matawi yake jordan ruco
 
Elimu ya juu sio sekondari kua tcu ikupangie unatakiwa wewe uombe mwenyewe nafasi. Ni mfumo uliokuepo na ni mfumo unaotumika sehemu nyingi duniani. Tatizo watu mnapenda kufanyiwa maamuzi na watu wengine ni utamaduni mbaya ambao unaendekezwa sana africa
TCU hailikuwai kupeleka mtu sehemu asiyoichagua ukiona umechaguliwa ujue uwezo wako uliishia apo.

Ndo maana kulikuwa na round mpaka ya 5 kama ulishindwa kukidhi vigezo kwenye round za mwanzo. Labda kama haukupitia huu mfumo kuingia chuo.
 
Kuna vyuo uchwara walikuwa wanapewa wanafunzi kiubwete bila ushindani wa ubora ....sasa washindane ....chuo bora kipate wanafunzi bora ili ushindani halisi uwepo ....
Kuna impact pia...

Ni bora hiyo CAS ingeboreshwa na si kuifuta....Hapa Watoto wa maskini wameshaa...
 
Mfumo wa sasa unatoa mwanya kwa mwanafunzi kuchagua chuo na kozi aipendayo. Hakuna kitu chabure na rahisi dunia hii ya sasa. Unataka vyuo tayarisha fedha nenda kalipie applicatiob form
 
Kuna impact pia...

Ni bora hiyo CAS ingeboreshwa na si kuifuta....Hapa Watoto wa maskini wameshaa...
Kweli kabisa mkuu.

Vyuo vya private vitajichumia pesa nyingi sana kwenye usahili jambo ambalo litakuwa na athari kubwa kwa watoto wa masikini
 
Kweli kabisa mkuu.

Vyuo vya private vitajichumia pesa nyingi sana kwenye usahili jambo ambalo litakuwa na athari kubwa kwa watoto wa masikini
Halafu watu kupangiwa kozi wasizotaka litaongezeka maana competition itakuwa kubwa sana...

Ni bora kupangiwa chuo ambacho si chaguo lako lakini kozi iwe chaguo lako, kulikoni kupangiwa kozi ambayo si chaguo lako ila chuo ulikipenda...

Wata fail na watairudisha CAS....mark my word
 
Mfumo wa sasa unatoa mwanya kwa mwanafunzi kuchagua chuo na kozi aipendayo. Hakuna kitu chabure na rahisi dunia hii ya sasa. Unataka vyuo tayarisha fedha nenda kalipie applicatiob form
Wewe hujakaa chini na kutafakari madhara yake...ina madhara makubwa afadhali CAS
 
Halafu watu kupangiwa kozi wasizotaka litaongezeka maana competition itakuwa kubwa sana...

Ni bora kupangiwa chuo ambacho si chaguo lako lakini kozi iwe chaguo lako, kulikoni kupangiwa kozi ambayo si chaguo lako ila chuo ulikipenda...

Wata fail na watairudisha CAS....mark my word
JPM kaathiri sana wafanyakazi wake! Tuchume tu haya anayoyapanda maana watumishi wanapokea maagizo bila kutafakari faida na hasara zake, wanaishia kutekeleza hata kama roho zinawasuta.

CAS ingeendelea lakini kwa maboresho ambayo yangepunguza adha za watu walio wengi.
 
Back
Top Bottom