mirindimo
JF-Expert Member
- Nov 2, 2009
- 821
- 1,338
Hizi taasisi za serikali kuna haja ya kuzifumua na kuzijenga upya kwa kuweka watu ambao ni waadilifu na watakua tayari kuwatumikia watanzania. Tukianzia na TCU, hawa jamaa bado wana system ya business as usual yaani kama huna mtu unamfahamu hapa utasugua gaga mpaka utie akili.
Kuna mashirika watumishi wake wamesitishiwa mishahara yao kwa sababu hawajahakiki vyeti lakini ukiuliza watumishi hao wanakwambia wameshatuma vyeti vyao na taarifa zao kwenye mtandao wa TCU zaidi ya mwezi na jamaa wamekaa kimya hakuna anaehangaika kuhakiki. Hivi mnajua mnao watesa ni watanzania wenzenu, dada zenu kaka zenu mama zenu wadogo zenu. Kwani mna matatizo gani hapo ofisini?
Na ukifika pale utakuta wanacheza karata na game zingine kwenye kompyuta au simu zao. Wengine wamefungua site za udaku au wako snapchat au facebook.
Nafikiri kuna haja ya rais kuchapa viboko na kufukuza kazi siku moja watumishi wa aina hii.