kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 12,233
- 12,506
Vyuo vinachagua/dahiri wanafunzi wenye sifa kwenye vyuo vyao kwa idadi waliyopewa na TCU, lakini wanafunzi waliochaguliwa nao wana hiari ya kuukubali/confirm udahiri wa chuo kwa kutumia mtandao hadi dakika ya mwisho.
Mkanganyiko kwa vyuo uko hivi, vyuo havina uhakika ni wanafunzi wangapi watakwenda kusoma chuoni kwao, hivyo wataendelea kudahiri kwenye madirisha yote hadi mwisho wa udahiri madirisha yote yatakapofungwa.
Hivyo, kuna hatari vyuo vikazidisha idadi ya wanafunzi vyuoni wakati wa harakati za kupambana na wanafunzi waliopatiwa nafasi lakini hawataki ku confirm mapema kujiunga na chuo chao. Hii inavifanya vyuo visijue mapema idadi hali ya wanafuzi watakao kwenda kusoma kwao na kuvifanya vyuo vichague/upload majina mengi kufidia wale ambao ni not conformed kwenye madirisha ya nyuma.
Ushauri wangu, TCU tafuteni njia ya kutatua shida hii inayosumbua vyuo, wanafunzi na wazazi. Kwani watoto wanaokwenda form one, form six na vyuo vya kati wanachaguliwaje?