TCU hatimaye yatoa sintofahamu

KAFA.cOm

JF-Expert Member
Jun 22, 2013
1,301
738
TUME ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), imetoa ufafanuzi juu ya taarifa za kutoka kwa matokeo ya waombaji wa nafasi za kujiunga na vyuo vikuu hapa nchini, kwa mwaka wa masomo 2016/2017

Kwa siku tatu sasa, kumekuwepo na taarifa za TCU kutoa matokeo ya nafasi hizo huku wanafunzi wengi wakilalamikia kushindwa kuyaona matokeo hayo katika tovuti ya tume hiyo.

Akizungumza kwa njia ya simu jioni ya leo, Edward Mkaku, afisa habari mwandamizi wa TCU amesema, TCU tayari imeweka matokeo ya awali ya nafasi hizo lakini matokeo hayo ni awali tu na siyo rasmi mpaka pale yatakapothibitishwa.

“Tumetoa matokeo ya awali (provisional results), ambayo mwanafunzi anatakiwa kuingia katika akaunti yake ya TCU na kuona kama amepangiwa Chuo au la, lakini matokeo hayo siyo rasmi mpaka pale yatakapokuwa yamethibitishwa (approved),” amesema Mkaku na kufafanua zaidi kuwa.

“Katika matokeo ya sasa tuliyotoa, mwanafunzi hawezi kuona amepangiwa chuo gani wala kitivo au taaluma aliyopangiwa kusoma, ila tu anajulishwa kuwa amepangiwa kusomea kitu kimoja kati ya vile vitano alivyoomba.”

Akitolea ufafanuzi juu ya wanafunzi ambao wamekosa nafasi za kuchaguliwa katika hatua ya sasa, Mkaku amesema wanafunzi hao wanayo fursa ya kuomba tena nafasi hizo.
“Tayari zoezi la kuomba vyuo kwa awamu ya pili limeanza tangu jana (Jumatatu), wanafunzi waliokosa nafasi katika awamu ya kwanza wanaweza kuomba tena katika awamu hii ya pili,” amesema.

Uombaji wa nafasi kujiunga na vyuo vikuu unaofanyika mwaka huu, utakuwa chini ya vigezo vipya vya kujiunga na elimu ya ngazi hiyo tofauti na miaka iliyopita. Hii ni kufuatia mabadiliko yaliyotangazwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia chini ya Profesa Joyce Ndalichako.

Lakini pia uombaji wa mwaka huu, unafanyika wakati serikali ikiwa katika mchakato wa kuwasaka wanafunzi waliopo vyuoni pamoja na waliohitimu vyuo bila kuwa na vigezo. Vyuo vikuu mbalimbali visivyokidhi matakwa ya kitaaluma pia vimechukuliwa hatua.
 
Asante kwa taarifa. Ila hayo mambo ya kusubiri confirmation naona ni figisu nyingine isiyokuwa ya lazima. Sipendi mambo ya suspense.
 
mkuu ungemuuliza approval inachukua muda gani ingetufaa zaidi ili kuepuka stress zisizokua za lazima kwani wengine tumeomba vyuo vyenye competition kubwa.
 
Sasa Je kama MTU anasubiri comfimartion ya chuo husika halafu chuo kikamkataa na wamesharuhusu watu wengine second round then vyuo second round vikajaa hawaoni kwamba watakuwa wamemfanyia ukatiri huyu anaesubiri kua approval

Iv mbona hua wanaongea kama vile akili hazimo kichwani

Alafu mtoa mada umesema amezungumza Leo jioni wakati jioni bado

Kumbuka hapa ushatuongezea stress zingine tena na ni vizuri ukaweka source
 
Sasa Je kama MTU anasubiri comfimartion ya chuo husika halafu chuo kikamkataa na wamesharuhusu watu wengine second round then vyuo second round vikajaa hawaoni kwamba watakuwa wamemfanyia ukatiri huyu anaesubiri kua approval

Iv mbona hua wanaongea kama vile akili hazimo kichwani

Alafu mtoa mada umesema amezungumza Leo jioni wakati jioni bado

Kumbuka hapa ushatuongezea stress zingine tena na ni vizuri ukaweka source
Nashia kucheka tu maana hasira nilikua nayo naweza ata kumeza mtu.
 
Huu ni ubabaishaji uliopitiliza, kwa hali hii mazingira ya rushwa yaweza kuwa yanaandaliwa na ile ya kupangiwa chuo usichokitaka wala kukipenda.
Utaratibu wa kuomba moja kwa moja vyuoni ndio ulikuwa bora kuliko sasa. Na mbaya sana hata hizo website utafikiri hazina wataalam wa kuhudumia ubora wa network
 
Ni kwa nini wasiwe wanafanya hiyo approval kabisa ndo wanarelease au wanaandaa mazingira ya kupiga hela
 
Chenga bado tunaendelea ktk Elimu ya Tz Diploma of Engineering inanitosha naenda kujiongeza ktk nchi nyingine zilizo tengeneza mifumo mizuri ya Elimu mfano Kenya
Kweli kaka, Mungu akusaidie, nchi hii mambo hayajakaa sawa hasa kwenye elimu
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom