Mimi sikuwa member wa JF, ila baada ya kusoma huu uzi, hasa kauli
ya MKL post
#2 aliyotoa kwa muanzisha uzi na jina alilowabatiza waliochaguliwa TCU 4th round la
makapi, nilihisi nachomwa na kitu moyoni nikalazimika kujisajili JF ili nami nipunguze machungu yangu. Huyu
MKL kama kweli ni muungwana, bila kujali ana mamlaka gani au la ,
atengue kauli na kuomba radhi kwa maumivu aliyowasabishia aliowatukana.
@ MKL
JF si pahali pa kuropokea tu analojisikia mtu kufanya hivyo, hasa ktk jukwaa la elimu,jukwaa ambalo linahusisha watu walokwenda shule wakaelimika. Hizi kauli za
piga tu, hata wa-tz wale nyasi lazima rada inunuliwe, hivi vijisenti, nk zitaisha Tanzania yetu?
Kwa uzoefu wangu, kauli hizi hutoka kwa watu waliolewa madaraka. Je,hii ya makapi imetoka kwa mlevi wa madaraka gani? @ MKL
Kuna post ya mdau mmoja alikuwa amechambua vizuri sana kauli ya MKL, nashangaa leo imefutwa. Ilikuwa post #4 . Sijui kwa nini? Inaonekana jamaa aliguswa sana na kauli chafu ya MKL,akaamua kuichambua. @ alpha1