TCRA: Zoezi la kuzima simu bandia ni endelevu

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Innocent Mungy amesema kuwa mtambo wa kuzima simu bandia unaendelea na kazi kuhakikisha kuwa hata simu ambazo hazikuwa hewani zitakapowashwa hazitafanya.
Meneja-Mawasiliano-wa-TCRA-Innocent-Mungy.jpg


Alisema kuwa simu feki ambazo hazikuwa hewani usiku wa kuamkia juzi zitakapowasha hazitafanya kazi kwa kuwa mtambo wa kuzima Imei bandia unaendelea kuhakiki simu hizo.

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Innocent Mungy amesema jana kuwa mtambo wa kuzima simu bandia unaendelea na kazi kuhakikisha kuwa hata simu ambazo hazikuwa hewani zitakapowashwa hazitafanya.

“Kazi ya kuzima simu hizo ilianza usiku kumkia juzi saa sita usiku na kila kampuni ya mtandao wa simu ilipaswa kuzima simu za wateja wake ambazo ni feki na kazi ya mtambo ni kuhakikisha simu iliyozimwa inapowekewa kadi ya mtandao mwingine haifanyi kazi na kuhakikisha simu zote feki zitakazoingia nchini hazifanyi kazi,” amesema Mungy.

Baadhi ya wananchi waliozimiwa simu wameilalamikia Serikali kwa kuwasababishia hasara kwa madai ya kutokuwa makini katika kudhibiti uingizwaji wa bidhaa feki.

Pendo Mpomelo, mkazi wa Kimara jijini Dar es Salaam alisema simu yake ilikosa mawasiliano kuanzia saa saba usiku

Chanzo: Bongo 5
 
Haya mazoezi ya Serikali huwa yanaishia njiani tu.

Ulianza mkukuta ukafeli, mara mkurabita, mara kilimo kwanza, mara BRN, Mara ulinzi shirikishi,Mara kutumbua majipu, mara Sukari sasa hili la simu feki.

Yaani full sarakasi
 
Jamani serikali iwafanyie nini mridhike
Simu fake zimezimwa bado hamtaki

Mnataka nini mmeambiwa itakuwa muarubaini wa wezi
 
Najaribu kufikiria,hivi kwa mtu ambaye alinunua sinu fake na hakuiweka line mpaka hilo zoez la kuzma simu fake liishe' je si atakuwa amerukwa na zoez hilo?? Au zoez hilo na la kila siku!!!!
 
Tangu lini Innocent Mungy kawa Mkurugenzi wa TCRA? Rekebisheni hiyo taarifa haraka kabla ya kumchonganisha Mungy ambaye ni meneja mawasiliano wa TCRA na Mkurugenzi wake. Haya mambo ya kukosea title za watu msiyachukulie kirahisi rahisi kwani huko maofisini fitina uweza kuanzia kwenye vitu vidogo tu.
 
Mwanzo nilidhani TCRA wenyewe ndiyo wana mtambo wa kuzimia hizo simu feki. Lakini kulingana na taarifa hii kila kampuni ya mtandao wa simu ndiyo inayozima mawasiliano kwa simu feki za wateja wake. Au sijaelewa vizuri.
 
Back
Top Bottom