TCRA yazipiga faini ya Sh38.1 bilioni kampuni 6 za simu kwa kosa la kutofikia viwango vya ubora wa huduma

comte

JF-Expert Member
Dec 11, 2011
8,171
5,905
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imezipiga faini ya Sh38.1 bilioni kampuni sita za simu kwa kosa la kutofikia viwango vya ubora wa huduma kama ilivyoanishwa na kanuni za ubora wa huduma za mwaka 2018.

Hata hivyo, mamlaka hiyo imezielekeza kampuni hizo kutozipeleka fedha hizo TCRA badala yake wazitumie kuwekeza kuboresha ubora wa huduma ndani ya siku 90.

TCRA.jpg
===

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imezipiga faini ya Sh38.1 bilioni kampuni sita za simu kwa kosa la kutofikia viwango vya ubora wa huduma kama ilivyoanishwa na kanuni za ubora wa huduma za mwaka 2018.

Hata hivyo, mamlaka hiyo imezielekeza kampuni hizo kutozipeleka fedha hizo TCRA badala yake wazitumie katika kuwekeza kuboresha ubora wa huduma ndani ya siku 90.

Kampuni hizo na faini zilizotozwa kwenye mabano ni ni Airtel (Sh11.5 bilioni), Tigo (Sh13 bilioni), Halotel (Sh3.4 bilioni), Vodacom (Sh7.8 bilioni), Zantel (Sh1 bilioni) na TTCL Sh1.3 bilioni.

Mkurugenzi wa TCRA, James Kilaba amesema mamlaka hiyo ilipima ubora wa huduma za mawasiliano katika robo ya mwisho ya mwaka 2020 na kubaini watoa huduma hao hawakufikia baadhi ya vigezo vya viwango vya ubora.

Amesema kwa mujibu wa kanuni ya 20 ya kanuni za ubora wa huduma za mawasiliano, mtoa huduma anayeshindwa kufikia vigezo anatakiwa kulipa faini.

“TCRA imeazimia kwamba badala ya kulipwa fedha hizo, tuzielekeze kwa watoa huduma. Kila mtoa huduma atumie kiasi chake alichotakiwa kulipa, akiwekeze katika kuboresha huduma.”

“Tunatoa siku tisini na tumekubaliana kwa kusaini hati ya makubaliano maalum, mtoa huduma atakayefanya kinyume TCRA itachukua hatua zaidi za kiudhibiti na kisheria pasipo kutoa taarifa,” amesema Kilaba.

Chanzo: Mwananchi
 
Mmewapiga fine ila fine wasilipe wazitumie wenyewe kuboresha huduma. Hizi drama kwa nn zisiletwe mtaani huku?

kidadari apigwa fine ya bilion 6 kwa kukwepa kodi hivyo asilipe hizo hela bali azitumie kuboresha biashara zake na kulipa kodi stahiki
Watu bwana hawanaga zuri ni kutafuta udhaifu tuu, wange zichukua mnaua sekta binafsi maelekezo yametoka et drama sasa walete mtani kwa nani?
 
Makampuni ya simu wanasema laini za 4g lakini ni aibu kubwa kusema laini zenye kasi ya 4g ilhali speed ni kama kinyonga.
 
Tigo sitawasahau nimeweka kihela changu salio mmekilamba na wala sijajiunga na huduma yoyote yenu.
 
Hata wakipigwa billion 200 fine hawatalipa hiyo hela. Mlaji wa mwisho ndio mlipaji.

Na gharama za data zitaendelea kupanda kila siku.
Sasa hivi unaambiwa GB 10 unapewa kwa TZS 1,000 in a week na dakika almost 300 mitandao yote; na 30 GB per month kwa just 5,000. Ngoja hiyo mwezi Machi ifike haraka next week.
 
Nimehuzunika sana Halotel 3.4 billion kweli? Nilitamani hii namba kwa uchache angalau ingezidishwa Mara 4 tupate 12billion huko. Hawa Halotel ni miongoni mwa watesi wetu.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom