TCRA yazindua usajili wa simu wa kielektroniki, utahusisha watumiaji wa simu kupigwa picha

1000 x 27 millions peoples = 27,000,000,000 Du hii aikabaliki ,kila siku sisi wadanganyika ni kupigwa hela tu.Ee Mungu baba tuletee Daudi wetu apambane na Goliati nyonya damu zetu sisi waja wako
 
NIDA wameboresha nini maana sijapata kitambulisho pamoja na kupigwa picha tangu 2014 hapa Dar
 
Binafsi nimesajiri laini mpya ya voda juzi na nimesajiri bure kwa huo mtindo mpya na utasaini kwa kidole kwenye simu ya msajili.

HII NI NZURI ILA HAPO KWENYE 1000 NADHANI NI KWA WASAJILI WA MTAANI ILA UKIENDA VODA SHOP NI FREE.
 
Yani wote mliochangia hata hamjaelewa chochote juu ya hili jambo,mmekurupuka tu wengine bila hata kusoma post Bali kwa kufuata mkondo wa wachangiaji wengine...badilikeni jamani;

Kwa kifupi ni kwamba,sasa usajili wa line unabadirika kutoka ule mfumo wa kuwa na usajili wa awali ambao ulikuwa unafanywa na mawakala mitaani Kisha kuchukua fomu za usajili na kuzipeleka ofisi za mtandao husika kwa ajili ya kukamilisha usajili,mfumo sasa unakuwa ni kusajili Mara moja tu kwa kutumia simu maalumu ambapo papo hapo wakala atakamilisha usajili,kitambulisho cha mteja kitapigwa picha na kujaza fomu maalumu iliyopo katika "app" ya usajili kwenye hiyo simu maalumu ya usajili..na kisha kutuma mojamoja kwa moja mtandaoni kukamilisha usajili...
Hizo elf moja moja mnazo lalamika jamaa watapiga hata si hivyo bali hiyo ni malipo ya kawaida kwa yule wakala atakayekusajilia hiyo laini kama vile utaratibu ulivyo kwa sasa kwa mtu anayetaka kusajili laini analipa tena wengine mpka elfu mbili...hapo hii ni fursa kwa vijana kukamata hizo simu na kuanza kazi unapata buku kila mtu..pia kwa kila fomu utakayosajili kuna kamisheni utalipwa mwisho wa mwezi..
Wao kampuni watakapo fanya biashara katika hili ni pale wanapouza hizo simu kwa laki moja kwa wakala anayesajili..lakini ni simu za kawaida tu smartphone za Vodafone..zenye app ya usajili..waweza kutumia kwa matumizi mengine yoyote ya simu ya kawaida huku ukiendelea kufanyia usajili
 
Vipi kwa wale pacha waliofanana. Maana sura ya mtu sio alama za vidole. Na wahenga walisema duniani wawili wawili.

Mkuu hata kama mmefanana ishu inakuja kwenye kusaini maana utasaini kwa kutumia kidole kwenye screentach ya msajili na tukumbuke vidole havifanani.
Nimesajiri kwa huu mtindo mpya.
 
Back
Top Bottom