TCRA yazindua usajili wa simu wa kielektroniki, utahusisha watumiaji wa simu kupigwa picha

Travic

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
728
1,000
Mamlaka ya mawasiliano nchini, TCRA, makampuni ya simu na mamlaka ya vitambulisho, NIDA, imezindua zoezi la usajili wa simu kwa njia ya kielektroniki.

IMG_0312.jpg

Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Profesa John Nkoma akiongea na waandishi wa habari Jumanne hii

Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Profesa John Nkoma, amesema zoezi hilo litasaidia kupata taarifa sahihi za watumiaji wa simu nchini.

"Sasa hivi zoezi litakuwa kiteknolojia zaidi. Utakuwa ukipigwa picha na simu. Kwahiyo uso huwezi ukafeki," amesema Profesa Nkoma.

Ameongeza kuwa zoezi hilo litasaidia kupunguza kwa kiasi kikubwa udanganyifu uliopo kwenye matumizi ya simu nchini na hakutakuwa na urahisi wa mtu kutumia jina la bandia pamoja na picha isiyokuwa yake.

Profesa Nkoma amesisitiza kuwa zoezi hilo halimaanishi kuwa ni usajili mpya wa sim card bali ni uhakiki wa taarifa za watumiaji wa simu nchini na linamhusu kila mmoja.

Kwa upande wake Rene Meza ambaye pamoja na kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania, ni mwenyekiti wa chama cha watoa huduma za mawasiliano nchini, MOAT alisema zoezi la usajili wa simu nchini limeingia kwenye hatua nyingine ya juu zaidi.

IMG_0316.jpg

Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha watoa huduma za mawasiliano nchini, MOAT akiongea na waandishi wa habari.

"Ni kwa kutumia teknolojia, na tena ni kwa smartphone ambayo wakala wa usajili ataipata kwa si zaidi ya shilingi laki moja ambayo itamsaidia kuchukua picha ya mteja anayetaka kusajili sim card yake. Mchakato huo hautumia zaidi ya dakika tano," alisema Meza.

Meza amesema usajili huo utafanyika nchi nzima na wameifanyia uhakiki teknolojia hiyo kwa zaidi ya miaka mitatu na tayari kuna vituo zaidi ya 5000 vinavyofanya usajili huo mpya.

Wateja watatakiwa kuonesha vitambulisho vinavyokubalika kufanikisha zoezi hilo na utagharimu shilingi 1000 tu.

Kwa upande wake mamlaka ya vitambulisho nchini, NIDA, imedai kuwa vitambulisho vya uraia vitalazimika kutumika zaidi ili kupata taarifa sahihi za watumiaji wa simu.

NIDA imesema imeboresha pia utoaji wa vitambulisho hivyo wa Dar es Salaam ambapo wananchi wakiwasilisha viambatanisho vinavyotakiwa watakuwa wakivipata ndani ya siku 7.

 

Kapwela

JF-Expert Member
Mar 11, 2015
2,011
2,000
Kukurupuka!!

Wanapaswa wajue kuwa huwezi watambua watu kama hawana cha kutambulika, Kudhani kuwa utawatambua Watanzania million 45 kwa kupitia sura zao ni kutofikiria vizuri.

Nchi ambayo haina vitambuliho rasmi haiwezeani kuwatambua watu, walipaswa walijue hilo kabla.Na ata sasa bado watachemka, mtu hatambuliwi kwa sura, ni mpaka tutakapokuwa na vitambulisho rasmi vyenye taarifa iliyothibitishwa na inayohakikika ndipo zoezi hili litakapoleta matokeo ya maana.

By the way, kwa nchi masikini kama yetu hatuna anasa ya kuwa na vitambulisho vingi na hiyo kutumia gharama kubwa, kwa maoni yangu tungekuwa na vitambulisho vya taifa pekee ambayo ndivyo pia vingetumika kupigia kura.Hili zoezi linlofanywa na tume sasa lingekuwa sio kugawa vitambulisho bali ku-update eneo alipo raia huyo.
 

mizambwa

JF-Expert Member
Oct 8, 2008
4,422
2,000
Hakuna jipya ni njia ya kutafuta pesa tu hii.

Tshs. 1,000/= ni nyingi sana kwa mtumiaji wa simu. Serikali wanafuta kila mbinu ya kubana kila kona.

Huu ni mtaji / mradi wa watu wachache katika kupiga hizi pesa, wameshafanya mahesabu idadi ya wamiliki wa simu na kufanya mar 1,000/= ni pesa ndefu hiyo.


TANZANIA, TANZANIA, NAKUPENDA KWA MOYO WOTE, NCHI YANGU TANZANIA JINA LAKO NI NZURI SANA..... NILALAPO NAKUOTA WEWE, NITEMBEAPO NAKUWAZA WEWE TU, KILA SIKU UFISADI TU JAMANI.....MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 

SOGHOO

JF-Expert Member
Mar 25, 2015
1,268
2,000
Hi fiongosi wa Tanzania bure kabisa, wanajua kuna users wa phones zaidi ya 30 million piga mara elfu
30,000,000 x 1,000 = 30,000,000,000/
wakigawana kila mtu bilioni moja point six
30,000,000,000 / 1,600,000,000 watakua mafisadi kumi na kitu wametoka kabla ya 25.10.2015
Siku hizi kima cha chini cha wizi ni one point six billion.

BURE KABISA HAWA. HAWANIPATI
 

SOGHOO

JF-Expert Member
Mar 25, 2015
1,268
2,000
Kanuni ya uchumi au common sense inasema, anaefaidika na huduma ndio huyo ailipie.
iweje mimi mwenye simu sifaidiki na huu usajili wa kifisadi nilipie wakati wanaofaidika ni ccm ??????
 

Hossam

JF-Expert Member
Feb 10, 2011
3,390
2,000
Umeongea kwa huruma lakini lazma mkamuliwe vilivyo!

Kweli mkuu sina namna, ntawapa tu buku yao haki ya mungu ila wanatuonea sana jamani, yaani basi tu sina namna hapa! Huwa kila siku namwambia my wife wangu tuchange hela tuhamie commoro au hata rwanda hanielewi kabisa.
 

white wizard

JF-Expert Member
May 18, 2011
6,572
2,000
Huyu NIDA naye vipi?!! yakwake yamemshinda anaanza kurukia ya wengine!!! au ndio mzee wa featuring??
 

Kizoku

Senior Member
Apr 30, 2014
184
225
Vipi kwa wale pacha waliofanana. Maana sura ya mtu sio alama za vidole. Na wahenga walisema duniani wawili wawili.
 

Bavaria

JF-Expert Member
Jun 14, 2011
50,654
2,000
Tanzania ina shindwa nini kuwa na central system ya kuwa na details za wananchi wake wote?...
Kila mmoja anakuja na mradi wake wa kupiga pesa...
 

Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
112,266
2,000
Kweli mkuu sina namna, ntawapa tu buku yao haki ya mungu ila wanatuonea sana jamani, yaani basi tu sina namna hapa! Huwa kila siku namwambia my wife wangu tuchange hela tuhamie commoro au hata rwanda hanielewi kabisa.

Pitisha mchango hapa jamvini tutakuchangia mkuu ili uhamie huko kwa kagame.
 

Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
112,266
2,000
Kanuni ya uchumi au common sense inasema, anaefaidika na huduma ndio huyo ailipie.
iweje mimi mwenye simu sifaidiki na huu usajili wa kifisadi nilipie wakati wanaofaidika ni ccm ??????

Mkuuu inawezekana wanataka kupata ela ya kuongezea kwenye budget
 

ISLETS

JF-Expert Member
Dec 29, 2012
8,133
2,000
wakuu naomba kuuliza .. hivi kubadilisha uraia wa nchi inaghalimu kiasi gani? hasa kuamia nchi kama angola
 

Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
112,266
2,000
Tanzania ina shindwa nini kuwa na central system ya kuwa na details za wananchi wake wote?...
Kila mmoja anakuja na mradi wake wa kupiga pesa...

Mkuu wataalam waliomaliza vyuo vikuu wapo mitaani hawana ajira,walio kwenye vitengo husika wanazaidi ya miaka 60 wanaongezewa ajira kwa mkataba na utaalamu wao wa it ni kuchapa barua tu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom